Kwa hali ya Uchumi wa Tanzania ilivyo hivi sasa, jumuiya ya kimataifa ikituminya, wananchi jiandaeni kula nyasi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,752
218,339
Ni dhahiri kwamba yanayoendelea Nchini Tanzania kwa sasa yanaiinua Jumuiya ya Kimataifa kuitupia macho nchi hii, Ubambikizaji wa kesi za uongo za Uhaini kwa wazalendo wapigania Mali za Nchi umefika kwa wafadhili wa nchi ambao wamekwisha jiridhisha kwamba kesi hizi ni kwa ajili ya kuwalinda Waarabu.

Kwa kadri ya macho yangu, Uchumi wa Tanzania kwa sasa UMEKUFA, hakuna mzunguko wa hela, dola imepanda na hata maisha ni ghali sana kutokana na Mfumuko wa bei, hali inatisha kwenye soko la Kariakoo, biashara zote zimeanguka kabisa.

Sasa kwa hali hii ikiwa Wazungu na watoa hela wengine wakitupuuza kutokana na huu ukamataji wa kijinga wa wale waliotushinda kwa hoja, sina wasiwasi wabongo wataanza kula nyasi, hofu kubwa ni kuhusu Wakati wa kiangazi, je watakula nini?
 
Tatizo la dola ni la dunia nzima. Kuhusu Mama Samia usiwe na hofu kwa sababu hata CHADEMA wanajua ni rais mpenda demokrasia hadi kumuita awe mgeni rasmi kwenye shughuli yao. Mwenyekiti Mbowe akiwa Mwanza pia nae alishawakemea wote wanaobeza utawala wa Dr Samia. Wewe mleta uzi usiwe na wasiwasi wowote kuhusu hali ilivyo.
 
Mbona Nchi yenu inaitegemea jumuiya hiyo kuwapa hela ?
Topic yako mkuu inahusu kutetewa na jumuiya za kimataifa kutokana na hao watatu waliopewa kesi kunyimwa misaada.

Ndio nikakujibu kutegemea jumuiya za kimataifa ni ujinga.pia unaweza kuchunguza kwa kina DP World ni ya Dubai nyuma yake zipo au ipo nchi ipi ya Ulaya!.
 
Back
Top Bottom