PostGE2025 CNN, kwanini mmeleta report isiyokua na jambo jipya?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Inaweza ikawa mpya kwako, ila hizo tetesi zilikuwepo mda mrefu na tetesi nyingine ilihusisha kiwanda Cha Twiga cement,
Kuna Uzi humu JF ukahoji kwamba kwanini wajerumani wameruhusu kiwanda Chao kutumika kufanyia uovu?
Mkuu, issue ya To do Cemetery CNN walichofanya walichofanya ni kuonyesha picha ya satellite ya eneo husika before and after. Hiii ni kazi kubwa TBC hawawezi hii.
 
Kwa hilo nawapongeza CNN ndugu, ila kuhusu report yote kwa ujumla Bado najiuliza maswali mengi sana.
 
Inaweza ikawa mpya kwako, ila hizo tetesi zilikuwepo mda mrefu na tetesi nyingine ilihusisha kiwanda Cha Twiga cement,
Kuna Uzi humu JF ukahoji kwamba kwanini wajerumani wameruhusu kiwanda Chao kutumika kufanyia uovu?
Tupe ww taarifa mpya.

Hv unaelewa maana ya chombo kikubwa kama CNN kutangaza hiyo habari? Au unadhani CNN n TBC?
 
Inaweza ikawa mpya kwako, ila hizo tetesi zilikuwepo mda mrefu na tetesi nyingine ilihusisha kiwanda Cha Twiga cement,
Kuna Uzi humu JF ukahoji kwamba kwanini wajerumani wameruhusu kiwanda Chao kutumika kufanyia uovu?
Una picha ya satellite ya kabla na baada?
 
Tupe ww taarifa mpya.

Hv unaelewa maana ya chombo kikubwa kama CNN kutangaza hiyo habari? Au unadhani CNN n TB
Naomba hiyo elimu, nini maana ya chombo kikubwa kama CNN kutangaza hiyo habari?
By the way sijawahi dhani kwamba CNN ni TBC hata kidogo
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba CNN ni chombo kikubwa cha habari duniani chenye makao makuu kwenye nchi yenye teknolojia ya juu sana duniani Marekani.

Soma > PostGE2025 - CNN Evidence: Tanzania Police Killed Protestors

Nikirudi kwenye report yenu mliotoa Leo nilitegemea mngetoa report ambayo Ina taarifa zenye utafiti wa kina na Hali ya juu kuhusu mauaji ya kinyama yaliyofanywa na utawala huu uliopo nchini Tanzani, lakini nyingi ya taarifa mlizotoa ni zile ambazo tayari tulikua nazo kabla mfano jambo la makaburi ya halaiki, mochwari n.k

Nimeandika haya sababu inawezekana haya mauaji yaliyofanywa ni makubwa na mlicho toa report ni asilimia chache za ukweli wa kilichotokea kwenye mauaji ya vijana wetu.

Swali lingine ninalojiuliza, inakuwaje report itolewe Leo na siku hiyo hiyo anatokea mtu wa serikali ovu anasema kwamba wataitolea maelezo, je ni kwamba walishajiandaa na report aina hiyo?

Lengo langu sio kukejeli, kuikataa au kudogosha report yenu ila ni kujiuliza hasa malengo ya hiyo report kwenye wakati kama huu ambao taifa lipo kwenye wakati mgumu.

Mengi ya mambo mliyo report ni tayari yalikua yanazungumzwa katika namna mbalimbali, hivyo nilitegemea kwa uzoefu wenu mngeenda mbali zaidi na kutoa report ambayo Ina uchambuzi wa kiteknolojia ulio mkubwa na utafiti wa hayo mauaji makubwa yaliyotokea kwa watanzania.

Ndugu watanzania naomba tuelewane kwamba taifa lipo kwenye wakati mgumu sana, hivyo tuwe makini na taarifa zote zinazotolewa kipindi hiki,

pia ninawapongeza CNN kwa hicho walichoonesha kwa Dunia kuhusu mauaji ya kikatili kwa ndugu, jamaa na rafiki zetu, ila inawezekana walichoreport ni sehemu ndogo ya uhalisia wa ukatili, mauaji n.k yaliyofanyika kwa watanzania.
Mkuu wewe ulikuwq unajua,lakini je dunia ilikuwa inajua kilicho tokea?hii report kuruka CNN ni bonge ya jambo jipya,watawala walishazoea tuna piga kelele humu ndani yanaisha baada ya kuruka tu umeona girishoni tayari ameanza kuruka ruka huko.Na ndio kwanza shughuli ime anza.
 
Turst ni subjective term, usipotrust wewe au Trump haimaanishi hakisemi kweli wala wengine hawaamini pia! Kwani Tanzania hamna vyombo vya habari? Kama vipo wangapi wanavitrust? Je ni wote? So akisema mtu mmoja not trustable hayo ni maoni yake na sio standard watu wote wakubaliane naye kijana
Ni kweli bro Mimi habari ya tbc,Azam,itv,channel 10 wote wahuni TU hao ila Kuna mwingine ndio chanzo chake Cha habari
 
Ninachojaribu kufanya sio kutoa lawama, ila kujiuliza ni kwanini report Haina taarifa za utafiti wa kina?

Sababu kwa chombo kikubwa Cha habari duniani kama CNN kinachotumia teknolojia ya Hali ya juu na watendaji wenye uwezo mkubwa, hivyo sikutegemea kuona report kama waliyotoa
Ndo maana nikatoa uzi serikali iisshtaki cnn na kudai compensation ya dola bl 10 kwa uu uongo waliotoa cnn au unasemaje si tunashinda
 
Nimeandika kwamba kulikua na tetesi kuhusu mass grave huko kondo kunduchi, kwingine ni msitu wa mabwepande n.k
Mkuu ngoja nikueleze jambo ambalo wengi nadhani hawajakueleza.

CNN hawawezi kuja na jambo jipya zaidi ya yale yaliyotokea na uliyoyasikia.
Wao kama media wamehabarisha kilichotokea, hawawezi kuchukua kila kitu sababu vingine vitakosa uthibitisho.
 
Mkuu wewe ulikuwq unajua,lakini je dunia ilikuwa inajua kilicho tokea?hii report kuruka CNN ni bonge ya jambo jipya,watawala walishazoea tuna piga kelele humu ndani yanaisha baada ya kuruka tu umeona girishoni tayari ameanza kuruka ruka huko.Na ndio kwanza shughuli ime anza.
Upo sahihi ndugu, binafsi nimewapongeza CNN katika hili,
Ila Kuna mda ni muhimu kutafakari hizi report hasa malengo yake kama ni heri au Shari na sio jambo baya kuhoji ili tuweze kuvuka huu mkwamo.

Kilichotokea kwa ndugu zetu kuuwawa kikatili namna ile ni jambo la kutisha hivyo inawezekana na propaganda nyingi zikawepo.
Hivyo tuwe na tahadhari
 
Mkuu ngoja nikueleze jambo ambalo wengi nadhani hawajakueleza.

CNN hawawezi kuja na jambo jipya zaidi ya yale yaliyotokea na uliyoyasikia.
Wao kama media wamehabarisha kilichotokea, hawawezi kuchukua kila kitu sababu vingine vitakosa uthibitisho.
Ni sahihi, nakubalia na wewe katika hilo,
Ila tahadhari muhimu kipindi kama hiki hasa kwenye hii Dunia ya kibepari
 
Vyomba vya habari vya Tanzania vimekaa kimya havijazungumzia mauaji ya Kimbari yaliyofanywa na Utawala wa Samia, ni.aibu sana.

Tukitaka tupate ripoti iliyokamili ikionyesha idadi ya watu waliokufa na majina yao na wale waliojeruhiwa Serikali inapaswa ilete Timu Huru ya Uchunguzi waliobobea kama mambo ya uchunguzi kama vile Scotland Yard.
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba CNN ni chombo kikubwa cha habari duniani chenye makao makuu kwenye nchi yenye teknolojia ya juu sana duniani Marekani.

Soma > PostGE2025 - CNN Evidence: Tanzania Police Killed Protestors

Nikirudi kwenye report yenu mliotoa Leo nilitegemea mngetoa report ambayo Ina taarifa zenye utafiti wa kina na Hali ya juu kuhusu mauaji ya kinyama yaliyofanywa na utawala huu uliopo nchini Tanzani, lakini nyingi ya taarifa mlizotoa ni zile ambazo tayari tulikua nazo kabla mfano jambo la makaburi ya halaiki, mochwari n.k

Nimeandika haya sababu inawezekana haya mauaji yaliyofanywa ni makubwa na mlicho toa report ni asilimia chache za ukweli wa kilichotokea kwenye mauaji ya vijana wetu.

Swali lingine ninalojiuliza, inakuwaje report itolewe Leo na siku hiyo hiyo anatokea mtu wa serikali ovu anasema kwamba wataitolea maelezo, je ni kwamba walishajiandaa na report aina hiyo?

Lengo langu sio kukejeli, kuikataa au kudogosha report yenu ila ni kujiuliza hasa malengo ya hiyo report kwenye wakati kama huu ambao taifa lipo kwenye wakati mgumu.

Mengi ya mambo mliyo report ni tayari yalikua yanazungumzwa katika namna mbalimbali, hivyo nilitegemea kwa uzoefu wenu mngeenda mbali zaidi na kutoa report ambayo Ina uchambuzi wa kiteknolojia ulio mkubwa na utafiti wa hayo mauaji makubwa yaliyotokea kwa watanzania.

Ndugu watanzania naomba tuelewane kwamba taifa lipo kwenye wakati mgumu sana, hivyo tuwe makini na taarifa zote zinazotolewa kipindi hiki,

pia ninawapongeza CNN kwa hicho walichoonesha kwa Dunia kuhusu mauaji ya kikatili kwa ndugu, jamaa na rafiki zetu, ila inawezekana walichoreport ni sehemu ndogo ya uhalisia wa ukatili, mauaji n.k yaliyofanyika kwa watanzania.
Taarifa ya uchunguzi ikitolewa na chombo mahiri kama CNN kwa Dunia inakuwa CREDIBLE na sio UDAKU! Hufanya kazi zao kwa umakini na sio kubabaisha.
 
Tahadhari kwa maana ipi mkuu? Tahadhari kwenye kitu gani? Kwenye hiyo habari au kwenye Nini?
Tahadhari kuhusu malengo ya report mbalimbali zilizotoka au zitakazotoka kuhusu mauaji ya ndugu zetu.
Kuna report zinaweza kutoka kwa mlengo kama ni habari ya kawaida ila kumbe ndani yake ni kulifanya hilo tukio la mauaji lionekane dogo kwenye jumuia za kimataifa na hatua stahiki zishindwe kuchukuliwa.
Nimeandika haya sababu inawezekana walichoreport CNN ni sehemu ndogo ya ukubwa wa maafa yaliyowapata wa Tanzania wenzetu.
 
Nafikiri sasa tupo kwenye mtazamo sana na wewe ndugu,
Hao CNN sio watu wakuaminika 100%.
Binafsi sisemi report Yao mbaya ila, inawezekana kilichotokea kuhusu ukatili, mauaji n.k kwa watanzania ni kikubwa kuliko hiyo report ya CNN
Kwani we jamaa unataka Nini mbona hueleweki? Mara report waliyotoa wewe mwenyewe unakili sio mpya kwako then tena unasema pengine Wana lengo la kutochonganisha mara hukutarajia report iwe ndogo hivyo sasa wewe ulitakaje??naona wewe umetumwa kupima kitu Fulani..........
 
Relax Mzee, soma taarifa yote mwanzo utanielewa, pia nikuweke sawa kwamba hamna sehem niliyosema kwamba wanalengo la kutuchonganisha
 
Back
Top Bottom