Clouds TV acheni kumtetea Makonda ni mkosaji

Clouds TV acheni kumtetea Makonda ni mkosaji

nimeshtushwa sana na watangazaji wa clauds tv asubuhi, wameonyesha dhahiri kumtetea makonda, jamani ata kama ni ukada sometimes muwe mnauweka pembeni hasa kwenye mambo ambayo yako dhahili, kwa mtu mwenye akili ata awe kada hawezi tetea jambo lile.

wakuu kiu kweli.clouds tv na radio ni kama zimepoteza muelekeo kwa kujipendekeza kwa viongozi na kuacha misingi ya kitaaluma ya kutoa huduma bora kwa walaji bila kujali hitikadi maana walaji kila mtu ana itikkadi yake sasa uielemea upande 1 itakula kwako. Kwa sasa clouds tv na radio ni kama mdogo wa tbc maana hata watangazaji wao wanashindwa kuficha ukada wao.hasa kipindi cha [360%] kinachorushwa.kila siku asubui clouds tv na watangazaji ni. Na makada no 1 ni [1]kija[2]samwel sasari[3]hudson kamoga:hawa jamaa ni makada dam dam kipindichao ni hovyo hovyo.nadhani wanatafuta ukuu wa wilaya.
 
Kazi ya Warioba ilishakwisha zamani sana mara baada ya kukabidhi rasimu ya pili ya katiba swali linakuja Warioba kazi anayoanya kapewa na nani? Je anatumia gharama za nani kuendesha hizo shughuli zake?

Je tumtambue yeye kama mpinzani wa gvt inayomlisha na kumlea ? Maana hainingii akilini mtu unayelelewa na gvt kama waziri mkuu mstafu anafanya kampeni ya kutaka kuiangusha gvt yako. je anayempa kiburi hicho ni nani na analitakia nini taifa hili ?

Well said mkuu, hayo ni maswali ya muhimu kujua majibu yake kuhusu huyu Mzee warioba.
 
Ila kumbe kuna watu wanahitaji msaada kifikra!mnataka Tanzania iwe nchi ya watu wa ndio tu!
Huyu mzee mnataka mawazo yake ayaelezee kwa nani?
Jameni naona kuna damu inanukia kama mawazo ya watawala ndio Makonda anayafanyia kazi.
 
Warioba anachokifanya sasa ni kuchochea machafuko. Hana nia njema na mustakabali wa nchi yetu.
 
Machafuko kuwaelimisha wananchi.!? Kama hao ndugu zako wanajidai wanashindana kwa hoja kwa nn jana walishindana kwa fujo.
 
Jaman clouds tv naamini kabisa kuna baadhi ya vipindi ni vizur tena sana na vinafundisha sana achen kuiponda vitu msivyo vijua
 
Jana kupitia kipindi cha jahazi Musa akiwa katika mahojiano na Paul anayetuhumiwa kwa kumrushia chupa Mzee Jaji Walioba, alitumia lugha ambayo kimsingi inaaina ya uchochezi na ukosefu wa maadiri ndani yake. Hii ilimtoka baada tu ya kuhojiana na Makonda na kuripot kuwa juhudi za kumpata Mzee Jaji Walioba ilikuthibitisha tukio hilo ziligonga mwamba na kudai clouds inaendelea kumtafuta Jaji walioba kuthibitisha kama kweli "ALIKULA MAKOFI".....sidhani kauli kama hii Musa kama anaweza kumbwambia Babu yake tena kupitia chombo kinachosikilizwa na jamii ya watu wengi.

Ni kauli iliyo tuchefua hadi wote tuliokuwa tunasikiliza kipindi hicho kuzima radio. Ushauli wangu kwa Musa Kama ulitereza tafadhari, kawithdraw kauli yako. hiyo kauli sio nzuri kwa mtu anaye habarisha jamii juu ya mambo yanayo izunguka.
 
Mussa niwa kumsamehe bure nilimuonaga arusha anavyotembea huwezi amini ni jinsia ya kiume.
 
ukada unawatoa ufahamu hata hawajui walitakalo wanataka linalotakiwa na watawala. Ukiwa na njaa ya akili ni shida sana ubongo umelishwa upotofu kutojitambua.
 
Tv clouds wamesema wanachokijua, huo udhahiri wa kilichotokea si ukiweke wewe tuone badala ya kumtetea mzee Waryoba aliyepagawishwa na watu wasioitakia mema Tanzania.

Wanakijua nini ? Yaani kumsikiliza Mtu mmoja makonda ni kusema wanachokijua?wabalance Habari wampe nafasi Mzee Warioba naye asema anachokijua, Tambua Mzee Warioba hajapagawishwa na Mtu Bali kasimama kwenye Ukweli tu, kumbuka siku zote Ukweli huwa unauma.
 
Jaman clouds tv naamini kabisa kuna baadhi ya vipindi ni vizur tena sana na vinafundisha sana achen kuiponda vitu msivyo vijua

Kwani watu wanaviponda vipindi vyote? Watu wanalaani kumpa nafasi Makonda pasipo kubalance Habari toka kwa Mzee Warioba .
 
Warioba anachokifanya sasa ni kuchochea machafuko. Hana nia njema na mustakabali wa nchi yetu.

Wewe unashangaza kweli ! Nia njema ni ipi? Hivi kulea Uchakachuaji,mafisadi,wafanyakazi hewa na sasa unaletewa Katiba ya kubambikiwa kijanja janja sanjari na kuchakachua kura za maoni hiyo ni nia njema na mustakabali wa Nchi hii? Hivi mnataka watu waishi kwa unafiki mpaka lini? Hii dhana ya kudhani Kuwa kila linalochakachuliwa na ccm ni bora ndiyo sumu ya mustakabali wa Nchi hii.
 
Njia bora ya kuleta Habari ni kubalance pande zote si kuleta Habari ya Upande mmoja pekee kisha ukasema ni Habari kamili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom