Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Status
Not open for further replies.
watu wanataka kuona wabunge wao wanawawakilisha vipi!wao wanaona si kitu cha maana,wanayoyaona ya maana ni hayo mafiesta yao yanayowaharibu vijana wetu.. lakini siwashangai sana maana pale wote watangazaji ni makanjanja

Acha ushamba Bwana ile sio redio ya shirika la umma wapo kwa kutafuta pesa bana mbunge mbunge kitu gani
 
Watu wengine hawastahili kuchukuliwa serious kiasi hicho. Mimi naisikiliza clouds fm kama nimeboreka nataka kitu cha kunichekesha ndipo naisikiliza.

Hando anajua nini kuhusu demokrasia na haki za kiraia hadi watu muumize vichwa kujadili utumbo anaoutangaza? Bora kumsikiliza Loveness Love kuliko Hando
 
Bado kukomboleka kifkra tunahtaji muda mrefu ila hawa muda c mrefu watakuwa wachochez yatukute ya KENYA 2007 vyombo vya habari ka hivi wananchi tuvikemee
 
Nchi hii wachumia tumbo wapo kila kona. Kwa mchango huo anajua atapata ukuu wa wilaya. Foleni ni ndefu atasubiri sana.
 
juu ya mtangazaji wa redio hii,hili saa nyingine ni tatizo binafsi,inawezekana akawa ni mpwa wa katibu wa bunge so akaona ampe maflag bila kujali nini katoa,
vile vile tukumbuke kuwa kuna watu ambao ni vilaza,kuchangia hoja hadi asikie michango ya watangulizi sasa leo kakurupuka kutangulia kuchangia kwa uelewa na uwezo wake,
kwa upande wake yeye binafsi hapendi kuona vipindi live tena akiwa mwandishi na mtwangazaji,hii inaonyesha anatumia cheti cha shemeji kazini
,
 
niameacha kuisikiliza redio hii ya kimbwisi kitambo baada gadner G habash kuihama na nahic alihama kwaajili ya mambo hayo tu!!! Hamna redio mle zaidi ya kuipigia mikampeni chama cha jembe na nyundo!!! Kibonde usitake umaarufu kwa kukandia vyama vingine utaolewa mbwisi wewe
 
Clouds inatumiwa na serikali kueneza propaganda flani ambayo serikali inataka kuipitisha.

Watangazaji wenyewe hawapendi, ila wanaagizwa kufanya ivo, wakati tayari cheque inakua ishatumwa marketing.
 
Jana kimkweche changu jana kiikuwa kibobu nikapanda lift gari ya rafiki yangu hivyo huwezi kumuwekea masharti redio ya kusikiliza, yeye ni mpenzi wa clouds ndio nilipomsikia huyo anayeitwa Kibonde akisema tena kwa dhihaka kwamba jumatano ya majivu ilishapita.

Kilichonishtuwa zaidi yeye hajui kwamba redio si kijiwe cha kahawa kwamba kuna wengine hawajui kinachoendelea hivyo redio ni moja ya fursa ya mtu kuhabarika, basi yeye akaishia kusema yeye hayuko kwenye imani hiyo ya majivu, am sure huu mdhaha aishie kuwafanyia Wakristo wenzanke ingawa nilichobaini yeye si Catholic lakini siku akithubutu kwa Waislamu basi atabakia kuwa Historia.

Kwa yule rafiki yangu yeye ni catholic ndipo nikamgeukiwa nikamuuliza sasa umeshaelewa ni kwa nini sipendi na wala huwa sisikilizi kabisa redio hii?
M2 mwenyewe anaitwa kibonde,wazaz wake waliona ili toto sio rizki...kibondeeeeeeeeee chichman-dodo wewe....
 
Vyombo vya habr vina very crucial role to mobilize and educate the mass towards truth!and always truth is what works!Poor Kashilillah,poor clouds fm!shame on them!ptuuuuuh.
 
kwangu mimi naona hawa ndio wachochezi wa baadhi ya mambo yasiyo ya msingi.
tena alikuwa anaongea kwa mbembwe au katumwa

I am of the same opinion. Baadhi ya Radio Rwanda zilisupport Interhamwe kufanya genocide.
 
Tatizo hapa mnapondea, lakini jioni kwenye offa za bia na mpira mnawachekea na kuwapongeza kwa ulopokaji wao, badala ya kuonyesha sura ya kazi.
 
Wazo langu:Je, mtangazaji huyu anajua maana ya demokrasia? Haki za binadamu? Katiba ya jamuhuri ya Tanzania 1977?Na anachoshabikia ni kwa maslai ya taifa? Je, anachokubaliana nacho ndicho walicholenga walioleta swala la kutoonesha bunge live?[/QUOTE]Wewe unajua maana ya demokrasia,haki za binadamu na katiba 1977?Mtangazaji katoa maoni yake na mtazamo wake na si Clouds Fm,ambao ni haki yake kama mtanzania nayetumia demokrasia yake.ulitaka aseme mawazo yako ili uikubali clouds fm?Kinachofanywa na wabunge ni kwa maslahi ya Taifa?
 
Bwana Kusaga awe makini, kuchanganga biashara na siasa si busara sana, na hasa pale inapotokea kuwa unaowaudhi ni wateja wako. Hawa watangazaji wa Clouds FM wanamuandalia mkosi.
 
Ifike hatua tasnia hii ya habari iangaliwe upya make ni kama imeingiliwa na mamluki. mtu analala na anakurupuka tu bila kufikiri kwa kina juu ya kile anachokwenda kukiungumza kwa watu, Hivi kama bunge linaonyweshwa "LIVE" tunaona madudu haya, likiachwa kuonyeshwa itakuaje; kimsingi huyu mtangazaji naweza kusema anapungukiwa na elimu ya demokrasia na kama anajua basi niungane na waliozungumza hapo juu kwamba anatumiwa.
 
Jahazi, Power Breakfast KWISHNEI! Long time... Siku hizi huwa nasikiliza kile kipindi cha milad ayo na Sports extra! Hawa vijana wa Gordon Brown akina Kibonde, Gerald Hando na Paul James hawana uwezo wa kufikiri zaidi ya umbali wa pua yao...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom