Mtangazaji wa Clouds FM Radio leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast - Jicho la ng'ombe amesema ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.
Anasema kwa sababu wanajua wanaonekana basi mbwembwe, madoido, mihemko, mshawasha na mengine mengi yamekuwa yakifanywa na wabunge isivyo kawaida.
Anadai anashukuru kwa katibu wa bunge kuliona hilo.
Wazo langu:
Je, mtangazaji huyu anajua maana ya demokrasia? Haki za binadamu? Katiba ya jamuhuri ya Tanzania 1977?
Na anachoshabikia ni kwa maslai ya taifa? Je, anachokubaliana nacho ndicho walicholenga walioleta swala la kutoonesha bunge live?
Nasubiri kuona reaction ya vyombo vya habari na sisi wananchi!
Hivi bunge kuoneshwa live ni hisani? Tuache ujuha tena tulipaswa kukemea hili kwa nguvu zote!
Kuhusu Clouds tuwaache jamani tujadili hoja hakuna watu wenye akili timamu mle!
Masikini kwa hiyo hatutawaona waheshimiwa Ole Sendeka, Jenister Mhagama, Hamisi Kigwangala, Mwigulu Nchemba, Vuai n.k. Haki ya mwananchi kupata habari hapo inakiukwa.
someone, somewhere told me Tanzanians are stupid!!! i said what??????? ebu angalia hii mijitu kwenye thread hii
hakuna anayeilazimisha kusikiliza Clouds FM, wala hakuna anayewalazimisha lolote lile kuhusiana na hii radio
Yet mtu anaanzisha thread kuiponda!!!!
Clouds ni habari ya mjini, no. 1 in Tanzania inasikilizwa na wengi sana, mpende msipende
Let them reign pmbf nyie
serikali ndio inaamua bunge lionyeshwe ama la?Kuhusu kutorusha 'live' mijadala bungeni ni namna ya 'censorship' kwani serikali imeona inawapa wabunge wa upinzani umaarufu.Wanasema mijadala mingine bungeni inatoa 'picha mbaya' kwa jamii hivyo katika 'kukomesha' vitendo vya baadhi ya wabunge..