Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Status
Not open for further replies.
Wafu fm,radio nliyoacha kuisikiliza,kiukweli inaboa sana
 
hawa watangaji wanatafuta vyeo ccm hamuoni wakina muyingo sasa ni wakuu wa wilaya? wengine ni waandishi wa viongozi serikalini nk. so wanaendeshwa na tamaa hizo za kupata vyeo. binafsi radio na tv zilizobaki ni radio one na itv tu. wengine wote wanatumika tena bila mficho. maskini tanzania!
 
Ndo maana tume ya katibu iliwafukuza wandishi kumbe ni makanjanja na hawana msimamo wowote!
 
That's called faking.So,jitihada hapa ni kujenga fake image ya bunge. Ni nani atafanya editing na kuamua kwamba kitendo au hoja fulani itaharibu image ya bunge? If anything, kuoneshwa live kunaongeza nidhamu kwa sababu wananchi wote wanaona. Ukitaka kunielewa, tizama tabia yako ukiwa nyumbani na kwenye hadhara. Je ni sawa? Hii ni hatari jamani. Umeshalifikiria hili suala vizuri? Au ni ushabiki tu?

.......

Vema mkuu,editing???why editing???nchi hii wote tunafanywa majinga tu,fikra na mienendo yao ni kwenye mfumo wa zidumu fikra,wanasahau kuwa ni bunge la vyama vingi,kwani wabunge kutoka nje ya bunge wakati bunge likiendelea ni jambo lililozoeleka???tena mbele Raisi?

Mbona hawakusitisha kurusha live baada ya tukio hilo??Hiyo ndio silaha ya mwisho kwa mbunge anaeona hatendewi haki na spika.
 
"Eti wanajifanya wanamfanyia Birthday party Raisi" (Sugu).
 
KIBONDE analinda maslahi yake binafsi!!siunajua baba lizmoja amempa kipindi cha maisha ni nyumba!!. . . .

-Clouds yote ni makada wa CCM!!wewe angalia jinsi wanavyopewa shavu mfano:-mradi wa zinduka,jk aliwazawadia studio ya BURE!!.....siku ya kuzindua vitambulisho THT ilipewa shavu!!n.k

>>CLOUDS NI VIBARAKA WA CCM
 
Clouds FM sio wasemaji wa Watanzania bali hayo ni maoni yao ambayo hayapaswi kupuuzwa. Bunge Kutoonyeshwa live haina maana kutoonyeshwa kabisa, bali kuonyeshwa baada ya editing. Sehem ambazo wabunge walionyesha lugha zisizofaa au vitendo vyovyote ambavyo vingeweza kujenga negative image yai bunge kwa jamii vinaondolewa. Wananchi wataweza kuona jinsi wabunge wao wanavyowawakilisha japo sio LIVE.

.......

Tunataka Demokrasia,hii mambo ya kusema tunaangalia Bunge baada ya kufanyia editing ni dalili ya kutojiamini,afterall kama kuna mbunge anaboa it is better to see him live ili kama anachemsha inapofika kipindi cha uchaguzi tujue jinsi ya kumuhukumu.
 
Wanajf
kwani mmiliki wa hiyo clous fm ni nani?usikute ni riz 1 au mwigulu! Tbc na bunge ni mali ya watanzania,wasijaribu
 
Kwanza hicho kipindi sio tena Power Break fast bali ni Power Advertisment...Matangazo ni mengi kuliko huo uharo wanao ujadili...
 
Ahh,mie na familia yangu tulishaacha kuwasikiliza hao makanjanja siku miiiiiiiingi.NA ARUSHA WALISEMAGA HAWATAKI HAYO MAFIESTA YAO WAKIFIKA NI KUPOPOLEWA KWA MAWE.
 
Kwa mazingira ya kawaida kipindi chochote kurushwa live au kutangazwa ndio Maslahi ya Mwandishi wa habari na mtangazaji yoyote bila kujali kama anatoka radio ya wafu. Sasa inakuwaje hawa jamaa hawataki vipindi virushwe live au matukio kuripotiwa?? How comes mwandishi wa habari anaunga mkono unyimaji wa habari?? Kasomea chuo gani huyo mwandishi anayeshabikia wananchi kunyang'anywa fursa ya kupatiwa habari. This is too low hata kama ni njaa hapa zimezidi

Pasco hawa wenzako vipi????
 
In short Clouds FM kwa sasa inatumika na baadhi ya watu kwa manufaa yao sasa wanakoelekea ni wanajichimbia shimo kama hao watu wanaowatumia.
 
Mtangazaji wa Clouds FM Radio leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast - Jicho la ng'ombe amesema ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.

Anasema kwa sababu wanajua wanaonekana basi mbwembwe, madoido, mihemko, mshawasha na mengine mengi yamekuwa yakifanywa na wabunge isivyo kawaida.

Anadai anashukuru kwa katibu wa bunge kuliona hilo.

Wazo langu:
Je, mtangazaji huyu anajua maana ya demokrasia? Haki za binadamu? Katiba ya jamuhuri ya Tanzania 1977?
Na anachoshabikia ni kwa maslai ya taifa? Je, anachokubaliana nacho ndicho walicholenga walioleta swala la kutoonesha bunge live?

Tatizo la vijana wengi hasa Watanznia ni njaa,wao wanapenda sana Upambe akiwa na uhakika wa kupata viposho ili jioni nae akajitundike viti virefu,hawana ubunifu wa kazi gini afanye wao ni upambe na kupika majungu ili wapate posho za kuwawezesha kuishi Dar,Gerald Hando na Paulo James hawana tofauti na Juliana Shonza labda tofauti ni ndevu tu hivyo wao kujikomba kwa mtu mwenye hela kwa kutegemea kupewa kitu kidogo hawashindwi hao ndio wanaume kama mabinti wanamtumikia mtu anaewapa viposho ili nao wajione somebody mjini
Ila tahadhari genoside au yale mauaji ya Rwanda yalichochewa kwa kiasi kikubwa na aina ya watangazaji wapumbavu na wajinga wasiojua sababu ya wao kuwepo pale kama watangazaji wa Clouds FM wakiwemo na Gerald Hando na Paulo James,vyombo vya habari vilichochea yale machafuko kwa kiasi kikubwa sana wao sasa hivi wanacheka ila eleweni amani ikikosekana hata nyie hamtakuwa salama tena tutawatafuta na familia zenu zote endeleeni tu na kuongea ujinga wenu kwa kupewa viposho mnaacha taaluma yenu mnashabikia siasa
 
Kama clouds wanasema wanasupport kutorusha live bunge, basi wamwambie Kashililah ahakikishe hakuna kitu kinachopaswa kurusha live, hatutaka kuona hotuba ya waziri wa fedha wakati wa kikao cha bajeti inarushwa live, hatutaka pia hata JK alihutubie bunge halafu TV zimuonyeshe live, tutahitaji hotuba hizo nazo ziwe recorded ili huyo anayejiita Kashililah aweze kuziedit ili ajiriridhishe kuwa hotuba hizo hazikiuka kanuni za bunge ndipo ziruhusiwe kurushwa ili wananchi wazione, najua wanachofanya CCM hakitakuwa n'a tofauti n'a wakati ule alipouawa Mwangosi kwa kuzuia mikutano kwa kisingizio cha sensa wakati huo CCM wakiendelea n'a mikutano yao! kwa kuwa anachofanya Kashililah siyo kweli analinda kanuni bali anafanya kazi ya kukilindia chama chake cha magamba kutokana n'a wananchi kuendelea kukosa imani nacho kabisa kwa sasa!!
 
sikio la kufa halisikii dawa mbinu zote watatumia lakini 2015 ni mwisho wao.
 
Kumbe hii radio bado ipo eeh, king'amuzi changu hakiikamati kabisa....

Kama nchi hii ni ya kipumbavu kiasi kwamba tunashindwa kusimamia sheria na waandishi wa habari wanaunga mkono basi umaskini tulio nao ni halali yetu. Tuendelee humu humu kwenye vicious cycle. Bunge linazo kanuni na taratibu za kushugulikia wavunja kanuni, inakuwaje zisitumike hizo. Basi tuzuie madaladala yasitembee mjini kwa kuwa madereva wake wanavunja sheria za barabarani,,, hapana, atakayevunja sheria ashugulikiwe ipasavyo. Ndani ya bunge kuna spika dhaifu anayeshindwa hata kuwaadhibu wavunja kanuni za bunge, and in fact spika ndio bingwa wa kuvunja kanuni.

Hii radio watangazaji mabwabwa wengi, hawana uhuru wa kueleza wanachokiamini

Mkuu, hapo kwenye RED, Clouds hakuna waandishi wa habari, kuna waganga njaa tu!!!!

Tiba
 
Tatizo la vijana wengi hasa Watanznia ni njaa,wao wanapenda sana Upambe akiwa na uhakika wa kupata viposho ili jioni nae akajitundike viti virefu,hawana ubunifu wa kazi gini afanye wao ni upambe na kupika majungu ili wapate posho za kuwawezesha kuishi Dar,Gerald Hando na Paulo James hawana tofauti na Juliana Shonza labda tofauti ni ndevu tu hivyo wao kujikomba kwa mtu mwenye hela kwa kutegemea kupewa kitu kidogo hawashindwi hao ndio wanaume kama mabinti wanamtumikia mtu anaewapa viposho ili nao wajione somebody mjini
Ila tahadhari genoside au yale mauaji ya Rwanda yalichochewa kwa kiasi kikubwa na aina ya watangazaji wapumbavu na wajinga wasiojua sababu ya wao kuwepo pale kama watangazaji wa Clouds FM wakiwemo na Gerald Hando na Paulo James,vyombo vya habari vilichochea yale machafuko kwa kiasi kikubwa sana wao sasa hivi wanacheka ila eleweni amani ikikosekana hata nyie hamtakuwa salama tena tutawatafuta na familia zenu zote endeleeni tu na kuongea ujinga wenu kwa kupewa viposho mnaacha taaluma yenu mnashabikia siasa

Hapa tuko pamoja mkuu, ujinga wa hawa vijana haupashwi kuachwa bila kukemewa kwani baadae wanaweza kutuingiza kwenye matatizo ya kijinga. Kama ulivyosema, viredio uchwara kama hii ya Clouds vilichochea mauaji ya Kimbari Rwanda na hata hapo kwa majirani zetu wa Kenya redio zilichangia kuongeza moto kwenye ile post election violence ya 2007/2008. Ndio maana mtangazaji mmoja wa Redio yupo the Hague na akina Uhuru na Ruto.

Hawa ni vijana wadogo ambao tukiamua kuwathibiti mtaani, ni kazi ndogo.

Tiba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom