Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Status
Not open for further replies.

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Posts
4,071
Reaction score
1,381
Mtangazaji wa Clouds FM Radio leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast - Jicho la ng'ombe amesema ni sahihi kabisa kwa bunge kutooneshwa live kwa sababu wao wanaamini ndio sababu ya wabunge kuvunja kanuni za bunge kwa kupoteza muda kujadili mambo yasiyo ya msingi na kuacha yale ya msingi.

Anasema kwa sababu wanajua wanaonekana basi mbwembwe, madoido, mihemko, mshawasha na mengine mengi yamekuwa yakifanywa na wabunge isivyo kawaida.

Anadai anashukuru kwa katibu wa bunge kuliona hilo.

Wazo langu:
Je, mtangazaji huyu anajua maana ya demokrasia? Haki za binadamu? Katiba ya jamuhuri ya Tanzania 1977?
Na anachoshabikia ni kwa maslai ya taifa? Je, anachokubaliana nacho ndicho walicholenga walioleta swala la kutoonesha bunge live?


Leo asubuhi nimesikiliza na kufuatilia kipindi cha power breakfast kinachorushwa na radio clauds fm ya jijini Dar na imeshangazwa sana na kietndo cha watangazaji wake yaani Gerald Hando na Paul James (PJ) kushabikia kitendo cha katibu wa bunge kutangaza kwamba vipindi vya bunge haitarushwa tena live!!!!!

Binafsi sikuamini kwamba watangazaji hawa wenye dhamana kubwa ya kutoa elimu kwa watanzania na kukosoa serikali na jamii pale inapokosea wanaweza kushabikia na kumpongeza katibu wa bunge kwa upuuzi wa namna ile!!

Najaribu kujiuliza waha watangazaji uchwara wanafanya hivyo ili kutetea ajira yao ama ndio wale wale wanaopewa vibahasha vya kaki na serikali ili kutetea hata mambo ya kijinga kabisa ambayo yalitakiwa kukemewa kwa nguvu zote!!!!!

Kimsingi ukiangalia sababu zinazotolewa na bunge kuzuia kurusha vipindi vya bunge live ni za kitoto na za kipuuzi kabisa na hazina mantiki yoyote kwa maendeleo ya taifa

Mimi nashangaa sana yaani mbunge kutoa hoja binafsi ya kutafuta namna ya kusolve tatizo sugu la maji mkoani dar es saam au kuboresha elimu ya watoto wetu ni kosa??!!! eti wabunge wanafanya fujo kwa sababu wanaonekana live na wananchi kupitia runinga!!!!! Kwani kama mbunge amekiuka kanuni za bunge hakuna sheria za kumuadhibu mbunge husika????? matokeo yake eti bunge ndio linakuja na hoja hafifu kabisa ya kuwanyima wananchi haki yao ya msingi kabisa ya kujua chombo hiki cha juu kabisa cha kutunga sheria na kudhibiti serikali japo hakifanyi hayo kwa sasa namna kinavyofanya kazi!!!!!

Radio Clauds jirekebisheni maana kwa taarifa zetu watu wengi sana siku hizi wameacha kusikiliza vipindi vyenu kwa sababu mmekuwa too biased kutetea na kushabikia mambo ya kipuuzi yanayofanyika nchini particularly na serikali

Naomba nitaje vipindi vilivokuwa mahiri sana vya radio clauds ila siku hizi vimepoteza kabisa mwelekeo kutokana na watangazaji uchwara walioingizwa kuendesha vipindi hivyo tofauti na waanzilishi wake na nafikiri hii inachangiwa sana na hawa watangazaji kuendekeza njaa kali na kujikomba kwa watun fulani badala ya kufuata kanuni za profession zao!!!

1. Power Breakfast imeharibiwa sana na anayejiita Gerald Hando na Paul James tofauti kabisa na wakati ambapo kipindi hiki kilipokuwa kinaendeshwa na Masood Kipanya

2. Jahazi. Kipindi hiki kimeharibiwa kabisa kwa uwepo wa Ephraim Kibonde kwa kuendekeza unazi wake na njaa zake kwa kujikomba kwa ccm tofauti kabisha na mtangazaji Gadna Habash ambaye alikimudu haswa kipindi hicho before

Kwa namna hii sijui itachukua miaka mingapi kwa watanzania kukombolewa kifikra
 
sijui huwa wanawakilisha mawazo yao au ya watanzania
 
kwangu mimi naona hawa ndio wachochezi wa baadhi ya mambo yasiyo ya msingi.
tena alikuwa anaongea kwa mbembwe au katumwa
 
Kumbe hii radio bado ipo eeh, king'amuzi changu hakiikamati kabisa....

Kama nchi hii ni ya kipumbavu kiasi kwamba tunashindwa kusimamia sheria na waandishi wa habari wanaunga mkono basi umaskini tulio nao ni halali yetu. Tuendelee humu humu kwenye vicious cycle. Bunge linazo kanuni na taratibu za kushugulikia wavunja kanuni, inakuwaje zisitumike hizo. Basi tuzuie madaladala yasitembee mjini kwa kuwa madereva wake wanavunja sheria za barabarani,,, hapana, atakayevunja sheria ashugulikiwe ipasavyo. Ndani ya bunge kuna spika dhaifu anayeshindwa hata kuwaadhibu wavunja kanuni za bunge, and in fact spika ndio bingwa wa kuvunja kanuni.

Hii radio watangazaji mabwabwa wengi, hawana uhuru wa kueleza wanachokiamini
 
kwani wao sio watanzania?au unaposema watanzania unakusudia nini?

wao wakiwa watanzania je wana wanahaki ya kuusema uma kwa jambo hili? kwa sababu hili ni swala la maamuzi. hichi wanachofanya sio kupaza sauti za wanyonge. ila kugandamiza sauti za wengine angeruhusu simu na kuweka hoja kujadiliwa ningeona sahihi yeye katoa majumuisho yake na kukubaliana na jambo moja kwa moja.
hapa ndipo nilipoona alipokosea.
ni mtazamo wangu. kuwa kwa kweli kakosea
 
wao wakiwa watanzania je wana wanahaki ya kuusema uma kwa jambo hili? kwa sababu hili ni swala la maamuzi. sio kupaza sauti za wanyonge.
unaposema umma unakusudia nini? unakusudia watu wenye mawazo flani tu ndio umma?
 
Nasubiri kuona reaction ya vyombo vya habari na sisi wananchi!

Hivi bunge kuoneshwa live ni hisani? Tuache ujuha tena tulipaswa kukemea hili kwa nguvu zote!

Kuhusu Clouds tuwaache jamani tujadili hoja hakuna watu wenye akili timamu mle!
 
Nitajie chombo kimoja kiwe cha habari au chochote kile kinachowakilisha au kuwasilisha mawazo ya watanzania wote!

tupe maoni yako;unaona ni sawa bunge kusitisha kuonyesha "live"vipindi vya bunge?
 
tuna kazi Tanzania!!! :confused2: tuna kazi kubwa kweli
 
yani ccm wameona ni heri kutuficha yanayoendelea ili upinzani wakija kusema wanaonewa spika aseme waongo hao kwa vile hatutaona hatutakuwa katika position ya kuamini au kutoamini.
 
hivi kuwa mtangazaji unatakiwa kuwa na elimu ya aina gani?
 
tupe maoni yako;unaona ni sawa bunge kusitisha kuonyesha "live"vipindi vya bunge?
mimi naona ni sahihi ili wabunge kama akina ....... waache sifa za kijinga.Lakini pia bunge linaweza kuendelea kuoneshwa live lakini pawe na kanuni kwamba mtu akileta ujinga anakatwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom