Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Status
Not open for further replies.
Clouds FM sio wasemaji wa Watanzania bali hayo ni maoni yao ambayo hayapaswi kupuuzwa. Bunge Kutoonyeshwa live haina maana kutoonyeshwa kabisa, bali kuonyeshwa baada ya editing. Sehem ambazo wabunge walionyesha lugha zisizofaa au vitendo vyovyote ambavyo vingeweza kujenga negative image yai bunge kwa jamii vinaondolewa. Wananchi wataweza kuona jinsi wabunge wao wanavyowawakilisha japo sio LIVE.

Hahahahah sasa ufanyie editting ili iweje??kwani imekuwa movie ile???nidhamu za uwoga hazihitajiki mzeiyaaa
 
Kumbe hii radio bado ipo eeh, king'amuzi changu hakiikamati kabisa....

Kama nchi hii ni ya kipumbavu kiasi kwamba tunashindwa kusimamia sheria na waandishi wa habari wanaunga mkono basi umaskini tulio nao ni halali yetu. Tuendelee humu humu kwenye vicious cycle. Bunge linazo kanuni na taratibu za kushugulikia wavunja kanuni, inakuwaje zisitumike hizo. Basi tuzuie madaladala yasitembee mjini kwa kuwa madereva wake wanavunja sheria za barabarani,,, hapana, atakayevunja sheria ashugulikiwe ipasavyo. Ndani ya bunge kuna spika dhaifu anayeshindwa hata kuwaadhibu wavunja kanuni za bunge, and in fact spika ndio bingwa wa kuvunja kanuni.

Hii radio watangazaji mabwabwa wengi, hawana uhuru wa kueleza wanachokiamini

sidhani kama clouds kuna mwandishi wa habari pale aliyesomea fani hii.
 
naomba namba yake nimtukane....................!!!!! anyway sugu kashasemaga hiyo redio haina watangazaji wote waganga njaa tu!!!!!!!!!!!! k..nina zao. huyo naye eti ni mwandishi nonsense!!!!!!!!!!
 
Clouds FM sio wasemaji wa Watanzania bali hayo ni maoni yao ambayo hayapaswi kupuuzwa. Bunge Kutoonyeshwa live haina maana kutoonyeshwa kabisa, bali kuonyeshwa baada ya editing. Sehem ambazo wabunge walionyesha lugha zisizofaa au vitendo vyovyote ambavyo vingeweza kujenga negative image yai bunge kwa jamii vinaondolewa. Wananchi wataweza kuona jinsi wabunge wao wanavyowawakilisha japo sio LIVE.

That's called faking.So,jitihada hapa ni kujenga fake image ya bunge. Ni nani atafanya editing na kuamua kwamba kitendo au hoja fulani itaharibu image ya bunge? If anything, kuoneshwa live kunaongeza nidhamu kwa sababu wananchi wote wanaona. Ukitaka kunielewa, tizama tabia yako ukiwa nyumbani na kwenye hadhara. Je ni sawa? Hii ni hatari jamani. Umeshalifikiria hili suala vizuri? Au ni ushabiki tu?
 
Mawazo ya kiazi mmoja hayawezi shindana na ya watu timamu 10,muache aendelee kupayuka tu,labda anafukuzia ukuu wa wilaya.
 
Pia ni halali kabisa kwa haka kastation uchwara/blauze female kufungiwa,kuanzia na madame mchovu,kibonde,zero n.k wanaipotosha jamii
 
Tatizo siyo clouds bali wewe ndio tatizo, kama unatakusikia habari za maana kuna Redio one, redio Tumaini, wapo Fm meza ya busara & likes, sioni msingi wa malalamiko yako ni sawa na mtu kuja hapa kulilalamikia gazeti la Shigongo kwamba linapotosha jamii wakati wao ndio lengo lao la kuundwa kwake, mtu kama mimi ni lazima nitakuuliza kwani magazeti kama Mwananchi na Nipashe hamuyaoni?
 
Clouds ni mazuzu,yaleyale ya kuifagilia serikali kabla ya kutafakali kwa kina athali zake,mfano unapoondoa tv kurusha live vikao vya bunge kwasababu tu kulitokea mzozo,aliyeanzisha mzozo huo kwa maana ya spika ameadhibiwa???na kwa wanaolala bungeni je???waendelee kulala bila kuumbuliwa na tv???bora kuwa kilema wa viungo vya mwili kuliko kuwa kilema wa akili.Yaani hapo ndio mwisho wao wa kufikiri nina amini utawala ukibadilika kila kitu hadharani.
 
Kwa ni kwanin walianzisha kurusha Bunge Live?!
Na kwa nin hoja ya kutokurusha Live itokee kipind hik ambapo
>Kit cha spika kinalaumiwa sana kwa kupendelea serikal?! Na kwanin wabunge wavunje kanun kipind hik cha Makinda na sio cha spika Sitta ama wengne waliopita?!
>Mawazir wamebanwa mbavu?!

Kwan hakuna kanun za kumwajibisha Mbunge asiefuata kanun, isipokuwa kutokurusha Live?!

Mbunge asiefuata taratibu anaonekana mtovu wa nidham, vip kuhusu Spika ama naibu wake wasipofuata taratibu?!

Rushen bunge live kama kawaida sis wananch ndo 2taamua nan ni nan, nyie viongoz wa bunge waswas wenu kitu gan?!
 
Leo asubuhi nimesikiliza na kufuatilia kipindi cha power breakfast kinachorushwa na radio clauds fm ya jijini Dar na imeshangazwa sana na kietndo cha watangazaji wake yaani Gerald Hando na Paul James (PJ) kushabikia kitendo cha katibu wa bunge kutangaza kwamba vipindi vya bunge haitarushwa tena live!!!!!

Binafsi sikuamini kwamba watangazaji hawa wenye dhamana kubwa ya kutoa elimu kwa watanzania na kukosoa serikali na jamii pale inapokosea wanaweza kushabikia na kumpongeza katibu wa bunge kwa upuuzi wa namna ile!!

Najaribu kujiuliza waha watangazaji uchwara wanafanya hivyo ili kutetea ajira yao ama ndio wale wale wanaopewa vibahasha vya kaki na serikali ili kutetea hata mambo ya kijinga kabisa ambayo yalitakiwa kukemewa kwa nguvu zote!!!!!

Kimsingi ukiangalia sababu zinazotolewa na bunge kuzuia kurusha vipindi vya bunge live ni za kitoto na za kipuuzi kabisa na hazina mantiki yoyote kwa maendeleo ya taifa

Mimi nashangaa sana yaani mbunge kutoa hoja binafsi ya kutafuta namna ya kusolve tatizo sugu la maji mkoani dar es saam au kuboresha elimu ya watoto wetu ni kosa??!!! eti wabunge wanafanya fujo kwa sababu wanaonekana live na wananchi kupitia runinga!!!!! Kwani kama mbunge amekiuka kanuni za bunge hakuna sheria za kumuadhibu mbunge husika????? matokeo yake eti bunge ndio linakuja na hoja hafifu kabisa ya kuwanyima wananchi haki yao ya msingi kabisa ya kujua chombo hiki cha juu kabisa cha kutunga sheria na kudhibiti serikali japo hakifanyi hayo kwa sasa namna kinavyofanya kazi!!!!!

Radio Clauds jirekebisheni maana kwa taarifa zetu watu wengi sana siku hizi wameacha kusikiliza vipindi vyenu kwa sababu mmekuwa too biased kutetea na kushabikia mambo ya kipuuzi yanayofanyika nchini particularly na serikali

Naomba nitaje vipindi vilivokuwa mahiri sana vya radio clauds ila siku hizi vimepoteza kabisa mwelekeo kutokana na watangazaji uchwara walioingizwa kuendesha vipindi hivyo tofauti na waanzilishi wake na nafikiri hii inachangiwa sana na hawa watangazaji kuendekeza njaa kali na kujikomba kwa watun fulani badala ya kufuata kanuni za profession zao!!!

1. Power Breakfast imeharibiwa sana na anayejiita Gerald Hando na Paul James tofauti kabisa na wakati ambapo kipindi hiki kilipokuwa kinaendeshwa na Masood Kipanya

2. Jahazi. Kipindi hiki kimeharibiwa kabisa kwa uwepo wa Ephraim Kibonde kwa kuendekeza unazi wake na njaa zake kwa kujikomba kwa ccm tofauti kabisha na mtangazaji Gadna Habash ambaye alikimudu haswa kipindi hicho before

Kwa namna hii sijui itachukua miaka mingapi kwa watanzania kukombolewa kifikra
 
hawa clouds wengi wao ni makanjanja kwaiyo tusihangaike kuwajadili. hasa huyu kibonde amenifanya nisiipende kabisa hii radio na nimeacha kabisa kuisikiliza.
 
Akili zake fupi huyu mtangazaji
Jana kimkweche changu jana kiikuwa kibobu nikapanda lift gari ya rafiki yangu hivyo huwezi kumuwekea masharti redio ya kusikiliza, yeye ni mpenzi wa clouds ndio nilipomsikia huyo anayeitwa Kibonde akisema tena kwa dhihaka kwamba jumatano ya majivu ilishapita.

Kilichonishtuwa zaidi yeye hajui kwamba redio si kijiwe cha kahawa kwamba kuna wengine hawajui kinachoendelea hivyo redio ni moja ya fursa ya mtu kuhabarika, basi yeye akaishia kusema yeye hayuko kwenye imani hiyo ya majivu, am sure huu mdhaha aishie kuwafanyia Wakristo wenzanke ingawa nilichobaini yeye si Catholic lakini siku akithubutu kwa Waislamu basi atabakia kuwa Historia.

Kwa yule rafiki yangu yeye ni catholic ndipo nikamgeukiwa nikamuuliza sasa umeshaelewa ni kwa nini sipendi na wala huwa sisikilizi kabisa redio hii?
 
mimi naona ni sahihi ili wabunge kama akina ....... waache sifa za kijinga.Lakini pia bunge linaweza kuendelea kuoneshwa live lakini pawe na kanuni kwamba mtu akileta ujinga anakatwa.

Bado hujielewi.................
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom