Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Clouds FM (Power Breakfast): Ni sahihi kabisa Bunge lisionyeshwe LIVE!

Status
Not open for further replies.
gesi mbona ipo tayari Temeke
watu wa kasulu wana radi zao za sh 20 tu ukiwaona wanaituma fasta inapiga kimnara chao kiherehere chao kitakoma

QUOTE=K.Msese;5690664]......na siku ikitokea jiji la Dar likawa na gesi, na gesi hiyo serikali ikaamua ipelekwe mkoa mwingine kwa bomba...sisi wakazi wa Dar katika maandamano yetu ya kupinga hilo bomba......na katika choma choma (kama Mtwara).....hakika kituo cha redio cha Clouds.......ni chakukichoma moto chote![/QUOTE]
 
Watanzania tu watu wa ajabu sana.

Ukifuatilia sana hapa JF, Katika section ya media, Clouds FM inaongoza kwa kulalamikiwa na kupondwa lakini cha kushangaza hawahawa wanaoiponda wanafahamu mpaka vipindi na muda wa vipindi vyake. Sijui hii ndiyo nini kama siyo ulimbukeni wa hali ya juu.

Tanzania kuna radio nyingi na media ziko nyingi pia. Kwa nini mnaendelea kusikiliza Radio ambao achilia mbali vipindi vyake, hata watangazaji wake hamuwapendi.

Watu wanashindwa kuelewa kama kwa vipindi vya mitafuruku kama hivyo, ndivyo vinayoifanya Clouds kusikilizwa na section ya jamii ambayo inailenga.

Kupiga kelele hapa ni kuonyesha ni jinsi gani usivyo na uelewa wa neno UHURU wa kupata news and entertainment.

FOR GOD'S SAKE, THAT'S PRIVATE RADIO.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwa wale wanaoangalia tvs za kimataifa say CNN, BBC nk watakubaliana nami kwamba vikao nyeti ka vya kamati za Senate na Bunge (House of Commons) vinaonyeshwa ''live'' na hata kama wanajadili mambo nyeti ya nchi zao mpaka hata watu wa Manzese, Butakya, Masiwani n.k tunapata habari. Iweje bunge letu.

Hawataki waoneshwe vile maojority hawana hoja. waameingia mle kwa kupi...trees. Lakini kwa KATIBA mpya inayokuja this may be temporary issue.
 
Everyone has a right to be stupid although some abuse the privilege
 
hebu wekeni contacts zao hapa niwapigie simu na kuwaeleza kiungwana wanachofanya siyo sahihi.
 
Mimi mwenzenu napata shida sana na watu kama hawa na kunisababishia maswali mengi sana..
1. Bunge kwao ni nini
2. Kazi za bunge ni nini?
3. Hicho wanachotaka tusikione bungeni ni ili nani akione?
4. Wanauchukuliaje uelewa na mtazamo wa watanzania kisiasa?
5. Ni kweli vile vinavyotokea bungeni sisi watanzania hatuvipendi kuviona?
6. kwa nini hawa wafanyafujo bungeni wanapotuita kuwasikiliza kwenye mkutana ya hathara tunajaa sana?
7. kama bunge halita oneshwa live ndo salaama ya hao wanaowatetea?
8. Democrasia kwao ni nini?
9. Ni kweli zile fujo za bungeni watanzania hawazipendi?
10. Ni kweli zile fujo za kina John hazina masilai chanja kwa watanzania
maswali ni mengi sana...

Conclusion
Tanganyika ilitawaliwa na wajerumani muda wao ukaisha wakaja waingereza muda wao ukaisha wakaja TANU muda wao ukaisha wakaja sisiemu muda wao utaisha...... na kinachotokea bungeni ni ishara ya mwisho wa hawa ndugu zetu asilaumiwe mtu wala chama wala kitu chochote ni nature ina take place...
 
Wameajiliwa si sababu ya taaluma yao ya utangazaji lakini ni kwaajili ya vipaji vyao maneno hayo yameshawahi semwa na mkurugenzi wa clouds Joseph Kusaga wao kipaji zen taaluma na elimu baadaye ndio maana hawaoni taabu kuropoka wanavyojisikia uhuru wa kujua kinachoendelea bungeni ni wetu sote ikiwemo wao sasa wajadili huku wanaficha kwani wao wachawi watangazaji hao pia wametumwa na akili zao mgando
 
Kumbukeni kumekuwepo na utaratibu wa wanahabari siku hizi kupewa fulsa mbali mbali ktk uongozi ambapo hujiona watawala. Yawezekana ni ktk harakati hizo za kujiandalia mazingira yatakayo saidia kuwa miongoni mwa wajao hata kama hajatumwa. Na ktk malengo kama hayo lazima unafiki uchukue nafasi yake.
 
yani ccm wameona ni heri kutuficha yanayoendelea ili upinzani wakija kusema wanaonewa spika aseme waongo hao kwa vile hatutaona hatutakuwa katika position ya kuamini au kutoamini.

Madam wala usiumize kichwa juu ya hili la Huyu mpuuzi Kashilila, kuna sababu kuu Tatu zinazo pelekea kuchukua hiyo hatua ya kutorusha mijadala la bungeni live; naomba kueleza;

  • Wameshtukia mziki wa CHADEMA bungeni wanavyotetea maslahi ya taifa, na kwa vile watanzania siyo vipofu wanasubiri kwa hamu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ufike ili waweze kuwaadhibu magamba kwa tabia yao ya kushabikia upuuzi usiokuwa na tija. Ni dhahiri hoja ya kutorusha mijadala ya bunge live inasukumwa ni kile kinacho julikana kama wabunge wachache wa CHADEMA kuwafunika wabunge wengi wa CCM. Hivyo basi wanaamini kwa kufanya hivyo wananchi hatutaona mapambano ya makamanda wetu wa CHADEMA huko mjengoni, na hatimaye kutuacha watanzania na sintofahamu kuhusiana na uwakilishi wa wapendwa wetu.
  • Sababu nyingine inayo chochea hatua ya kutorusha mijadala ya bungeni live ni kutaka kuficha udhaifu wa Bi Kiroboto na Mshehereshaji mwenzake mzee Yusuph (Ndugai )
  • Sababu nyingine inayo chochea hatua ya kutorusha mijadala ya bungeni live ni kutaka kuficha madudu ya Muishiwa Dhaifu yanayo tekelezwa kupitia huu mhimili wa Bunge.
 
Yani wakati dunia inaena na mfumo wa Digital wao wanaturudisha kwenye analogy!!
 
Watanzania tu watu wa ajabu sana.

Ukifuatilia sana hapa JF, Katika section ya media, Clouds FM inaongoza kwa kulalamikiwa na kupondwa lakini cha kushangaza hawahawa wanaoiponda wanafahamu mpaka vipindi na muda wa vipindi vyake. Sijui hii ndiyo nini kama siyo ulimbukeni wa hali ya juu.

Tanzania kuna radio nyingi na media ziko nyingi pia. Kwa nini mnaendelea kusikiliza Radio ambao achilia mbali vipindi vyake, hata watangazaji wake hamuwapendi.

Watu wanashindwa kuelewa kama kwa vipindi vya mitafuruku kama hivyo, ndivyo vinayoifanya Clouds kusikilizwa na section ya jamii ambayo inailenga.

Kupiga kelele hapa ni kuonyesha ni jinsi gani usivyo na uelewa wa neno UHURU wa kupata news and entertainment.

FOR GOD'S SAKE, THAT'S PRIVATE RADIO.

.........
Ahaa! Kumbe kuna haki ya kupata habari kama hizi wanazo zisimamia kidete na tena kwa habari zinazo husu maendeleo ya mtanzania na tanzania ijayo tupokonywe.

Si kila habari inayoletwa basi inastahili kupewa umhimu,ndiyo maana tukapewa akili ili tuweze kupembua mbichi na mbivu.
 
Anajua ila wanatumwa na mabwana zao waliowaajiri na kigezo cha kuajiriwa redio za kipuuzi kama hizo ni umahiri wa kubana pua na kupaka carolight

Aijue katiba ya Tanzania wakati hajui neno lenyewe "katiba" lina maana gani!!??
 
Nasubiri kuona reaction ya vyombo vya habari na sisi wananchi!

Reaction ya vyombo vingine vya habari itakuwa very positive.

Kuonyesha Bunge live ilikuwa inawanyima soko vyombo vya habari hasa magazeti.

Kwa hiyo, sasa magazeti yatapata soko zaidi maana ndiyo yatakakuwa yanaandika yaliyojiri bungeni jana yake.

Kuhusu reaction wananchi, kwani ni wangapi huwa wanaangalia Bunge live?

Hata kama wapo wanaongalia Bunge live, sidhani kama watachukua hatua yoyoye.

Kwa kuangalia tuu matukio ya nyuma reaction wananchi ilikuwaje?

Mfano watu wengi wanaipiga madongo Clouds FM na kudai kuwa hawasikilizi tena hiyo radio lakini wao ndio wa kwanza kuleta habari za Clouds FM hapa.

Sana sana wachache watalalamika kama baadhi wanavyolalamika hapa na baada ya hapo ni business as usual.

Wengine we won't see the difference because hakuna kilichobadilika tokea bunge lianze kuonyeshwa live.

No body care in this country either mbunge or mwananchi.
 
Ahaa! Kumbe kuna haki ya kupata habari kama hizi wanazo zisimamia kidete na tena kwa habari zinazo husu maendeleo ya mtanzania na tanzania ijayo tupokonywe.

Si kila habari inayoletwa basi inastahili kupewa umhimu,ndiyo maana tukapewa akili ili tuweze kupembua mbichi na mbivu.

Malalamiko yangeeleweka angalau kidogo kama nchi ingekuwa na Radio moja bila kujali kama niya binafsi au la. Haya malalamiko yanaletwa kudai Radio inajichulia majukumu ya watanzania wote ni kuonyesha jinsi mlalamikani asivyoitumia haki yake aliyopewa kikatiba ya kuwa na CHOICE katika maisha. KWA NINI ANANG'ANG'ANIA KUSIKILIZA RADIO HIYO HIYO WAKATI KUNA RADIO ZINGINE. Hajui kuilazimisha Radio kusema kile anachotaka kusikiliza ni kuinyima Radio Cloud's FM haki yake ya kimsingi kama ilivyoainiswa ndani ya katiba.

Mawazo ya mleta mada yamekaa kidikiteta dikiteta
 
Watanzania tu watu wa ajabu sana.

Ukifuatilia sana hapa JF, Katika section ya media, Clouds FM inaongoza kwa kulalamikiwa na kupondwa lakini cha kushangaza hawahawa wanaoiponda wanafahamu mpaka vipindi na muda wa vipindi vyake. Sijui hii ndiyo nini kama siyo ulimbukeni wa hali ya juu.

Tanzania kuna radio nyingi na media ziko nyingi pia. Kwa nini mnaendelea kusikiliza Radio ambao achilia mbali vipindi vyake, hata watangazaji wake hamuwapendi.

Watu wanashindwa kuelewa kama kwa vipindi vya mitafuruku kama hivyo, ndivyo vinayoifanya Clouds kusikilizwa na section ya jamii ambayo inailenga.

Kupiga kelele hapa ni kuonyesha ni jinsi gani usivyo na uelewa wa neno UHURU wa kupata news and entertainment.

FOR GOD'S SAKE, THAT'S PRIVATE RADIO.

Umeona eh. Watu wanaiponda Clouds FM lakini wanaisikiliza kila siku.

Kuna na wengine wanaiponda TBC na kudai hawakumbuki siku ya mwisho walipoangalia TBC lakini ndiyo wa kwanza kabisa kupinga Bunge kutoonyeshwa live na TBC.

Kama mtu haangalii TBC ina maana alikuwa hangalii bunge live. So, kuonyesha au kutoonyesha bunge live will not make a difference to that sort of person.
 
Mimi nadhani tu hitimisho ni kwamba Sikiliza Redio Clouds at your own risk, tumeshachoka na kelele kuhusu clouds Fm.
 
Umeona eh. Watu wanaiponda Clouds FM lakini wanaisikiliza kila siku.

Kuna na wengine wanaiponda TBC na kudai hawakumbuki siku ya mwisho walipoangalia TBC lakini ndiyo wa kwanza kabisa kupinga Bunge kutoonyeshwa live na TBC.

Kama mtu haangalii TBC ina maana alikuwa hangalii bunge live. So, kuonyesha au kutoonyesha bunge live will not make a difference to that sort of person.

Mkuu EMT

Kwa mawazo na matendo kama haya, siyo ajabu hata washauri wa serikali(Rais) ambao ndani yake kuna wataalam wa psychology wanajua vilivyo mental functions na behaviors ya watanzania. Siyo ajabu kuona kuna mambo mengine serikali inadiriki kusema ni upepo tu na utapita. Ni kweli baada ya muda, kila kitu kinakuwa kimesahaurika na business back as usual

Misimamo ya watanzania wengi ni kama bendera isiyo na direction maalum. Huku wengi wakiwa ni two faces.

Mfano huu unatupa mantiki kuwa, Hawa hawa wanaoipiga mandongo CCM, ndiyo wa kwanza kuipa kura.

Tanzania siyo kama tuijuavyo.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom