Jana kimkweche changu jana kiikuwa kibobu nikapanda lift gari ya rafiki yangu hivyo huwezi kumuwekea masharti redio ya kusikiliza, yeye ni mpenzi wa clouds ndio nilipomsikia huyo anayeitwa Kibonde akisema tena kwa dhihaka kwamba jumatano ya majivu ilishapita.
Kilichonishtuwa zaidi yeye hajui kwamba redio si kijiwe cha kahawa kwamba kuna wengine hawajui kinachoendelea hivyo redio ni moja ya fursa ya mtu kuhabarika, basi yeye akaishia kusema yeye hayuko kwenye imani hiyo ya majivu, am sure huu mdhaha aishie kuwafanyia Wakristo wenzanke ingawa nilichobaini yeye si Catholic lakini siku akithubutu kwa Waislamu basi atabakia kuwa Historia.
Kwa yule rafiki yangu yeye ni catholic ndipo nikamgeukiwa nikamuuliza sasa umeshaelewa ni kwa nini sipendi na wala huwa sisikilizi kabisa redio hii?
.......