SoC02 Chuki, ubinafsi na unafiki, ndio vinachelewesha maendeleo ya nchi yetu

Stories of Change - 2022 Competition

politicians

Senior Member
Apr 8, 2018
154
124
Utangulizi:nchi yetu ina utajiri mkubwa wa rasilimali lakini ina umaskini wa maendeleo, watu wengi wanajiuliza swali kwa nini? Sababu zipo nyingi ila tatizo kubwa ni fikra na mitazamo ya kimaskini iliyopo kwa wananchi walio wengi inayosababisha vitu hivi (chuki,ubinafsi na unafiki) ambavyo vinapelekea kuchelewesha maendeleoi kama ifuatavyo.

Chuki: Chuki ni moja ya adui mkubwa katika nchi yetu anayeitafuna jamii na kusababisha umaskini mkubwa,
katika nchi yetu kuna wimbi kubwa la watu wanaopenda chuki na kuisambaza chuki kwa watu wengine na
kwa bahati mbaya watu hao wapo kila sehemu maofisini mpaka uraiani, kwa mfano, unakuta mtu yupo mtaani hafanyi kazi yoyote ila amekalia kusambaza chuki dhidi ya viongozi wake wa serikali anabaki kusema
mara mbunge mbaya, diwani, mwenyekiti au kiongozi fulani mbaya, sasa unajiuliza je wewe ni mwema?

Wanafalsafa wanasema "maisha ya maskini yametawaliwa na chuki na lawama", ukijiona wewe unapenda
kuchukia na kulalamikia watu ovyo ujue unaukaribisha umaskini wa kudumu kwa sababu chanzo cha utajiri ni fikra, mitazamo chanya na kuzitumia changamoto katika jamii yako kama fursa, raisi wa zamani wa marekani
J.F.Kennedy aliwahi kusema "usiniulize mimi nitaifanyia nini marekani bali jiulize wewe utaifanyia nini marekani"
kabla hujawalaumu viongozi wako wameifanyia nini jamii yako,jiulize kwanza wewe umeifanyia nini jamii yako?

Mfano mwingine,maofisini napo kuna chuki sana,unakuta ofisini wafanyakazi wanachukiana kwa sababu ya kugombania vyeo au unakuta mfanyakazi anamchukia boss wake na boss nae ana mchukia mfanyakazi wake, kuna wakati mwingine inatokea boss anakataa mawazo mazuri ya mtendaji wake wa chini hata kama ni mazuri na yenye tija kwenye tasisi, lakini kwa sababu yametolewa na mtu ambae anamchukia yanaonekana hayana maana, hali kama hiyo hudhoofisha tasisi kimaendeleo.

Mfano mwingine, baadhi ya watu kuwa chukia matajiri hasa vijana, jamii yetu inamtazamo hasi dhidi ya matajiri wazawa kuna kundi kubwa la watu wanaamini kila tajiri ni mshirikina, ukiwa tajiri katika nchi yetu halafu kijana watu wataanza kukupakazia umetoa kafara ya mtu, unauza madawa ya kulevya, jambazi n,k, jambo ambalo pengine si kweli, na hayo maneno yote hutokana na chuki, vijana wa kitanzania wanapomuona mwenzao amefanikiwa badala ya kumfuata na wenyewe wakajifunze mbinu za mafanikio,wanakalia kusambaza uongo uliojaa chuki na wivu wa kijinga.

Mfano mwingine, ndani ya jamii yetu kuna mambo ya ajabu sana, yani kuna watu wana chuki binafsi na
mtu mpaka wanamuombea kifo, hii inanikumbusha hadithi ya kijiji kimoja "siku moja alitokea simba usiku akamtafuna mtu mbaya waliokuwa wanamchukia pale kijijini na akatokomea kusiko julikana kesho yake
asubuhi wana kijiji walipo kuta mifupa ya yule bwana wakashangalia sana na wakajisahau kuwa na wao
wapo hatarini, usiku huohuo simba karudi tena kwa bahati mbaya akamtafuna mtu mzuri waliokuwa wanampenda sana hapo kijijini, kesho yake asubuhi wanakijiji walipoona mifupa ya yule mtu wampendae
walilia na kuomboleza sana,baada ya hapo wakachukua silaha kwenda kumsaka simba porini" funzo la
hadithi hii ni nni?, tusichukiane mpaka kufikia hatua ya kuombeana kifo kwa sababu kila mtu atakufa.

Ubinafsi: Ni moja kati ya sababu inayozorotesha maendeleo ya nchi,kwa mfano,kwenye swala la ajira ndani ya nchi hii imeshakuwa kama utamaduni bila kumfahamu mtu kwenye tasisi flani huwezi kupata ajira, swala la
ujuzi na weledi limeshawekwa pembeni ,mfano wa pili,yani unakuta boss anampatia mtu kazi kwa kuangalia
maslahi yake binafsi badala ya maslahi ya tasisi hata kama ni ya umma. Na hii ipo kwenye maeneo mengi hata kama ni mashindano, tumeshuhudia hata kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya muziki wale wanaoshinda huwa hawafiki mbali lakini wanaoshindwa baadhi yao hufika mbali na mziki,hii ni kwa sababu nchini kwetu tunatatizo kubwa la utamaduni wa "michongo" kuliko vigezo na hii inatokana na ubinafsi.

Mmfano wa tatu, nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa ajira, lakini ukiwaambia vijana waunde vikundi ili wafanye shughuli ya pamoja wengi hawataki na hata wakiunda kikundi haitachukua mda mrefu
kitakufa, unajua kwa nini?, vijana wengi wana tabia ya ubinafsi yani kila mtu anataka afanye chake, hii inatokana wengi hawajui faida za kufanya kazi kama kikundi, makampuni makubwa yote duniani yalitengenezwa na timu ya watu wenye malengo na maono yanayo fanana ,walifanya kazi kwa bidii kwa pamoja mpaka kufanikiwa.

Mfano wa nne, unakuta mtu amemuona mtu flani anafanya biashara flani na ina mlipa na yeye kwa sababu
anapesa anakimbilia haraka kuanzisha biashara kama ile bila kufanya utafiti wa kutosha matokeo yake
baada ya kupata faida kwenye hiyo biashara anapata hasara, watanzania wengi wamekariri kufanya
biashara mpaka uanzishe biashara yako na wakati kumbe unaweza ukawekeza kwa mtu mwenye biashara
unayoipenda na ukapata faida zaidi ya mwenye biashara hiyo,ubinafsi katika jamii yetu huwafanya watu
wengi kutowekeza kwenye biashara za watu wengine na kuchelewesha maendeleo katika taifa.

Unafiki: Ni tatizo la watu wengi kwenye jamii yetu, kwa mfano, unakuta boss wa tasisi flani anapokuwepo
ofisini kila mfanyakazi anajitahidi kumsifia hata kama anakosea, siku huyo boss akija akiondolewa ofisini kwa
kwa tuhuma za utendaji mbovu, akishaondoka tu wote wanaanza kusema walijua ataondelewa tu kwa sababu alikuwa sio mtendaji mzuri, sasa unajiuliza wenyewe si ndio wasaidizi wake walishwindaje kumshauri vizuri kama waliya ona hayo? Unafiki upo sana hata kwa baadhi ya wandishi wa habari kutoa taarifa za kumsifia mtu akiwa ofisini ila akishatoka ofisini wanaanza kutoa maovu yake,unafiki una didimiza maendeleo ya nchi kila eneo

Mfano mwingine: Kuna baadhi ya watendaji wa idara flani unakuta wanaficha hadi matatizo yaliyopo
kwenye idara yao au jamii yao pale yanapoibuliwa na wandishi wa habari au wanaharakati fulani, na
unakuta watendaji hao wanasimama hadharani kukanusha taarifa hizo za kweli kwa lengo la kulinda ajira
zao, kuna usemi mmoja unasema "hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"
wahenga wana msemo wao "mficha maradhi kifo humuumbua", Unafiki, unafiki ni kitu kibaya sana

Hitimisho: Jamii inapaswa ibadilike iachane na (chuki, ubinafsi na unafiki)usio na maana, badala yake
isambaze (upendo, umoja na ukweli)kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom