Akili na Mageuzo Yenye Maendeleo Duniani

Philo_Sofia

Member
Oct 4, 2023
60
94
Dunia yetu inapitia mageuzo mbalimbali yenye maendeleo. Kuanzia mifumo ya kijamii, uchumi na maendeleo mpaka teknolojia.

Kwa hakika, tangu kuanza kwa dunia takribani miaka bilioni nne hivi, wanadamu wamekuwa wakishuhudia mageuzo na mabadiliko mbalimbali katika kila zama.

Wote tunakubaliana kwamba duniani kuna mabadiliko mengi sana, na maendeleo makubwa sana katika elimu; na katika teknolojia. Swali hapa ni: mambo haya yote yanaletwa na nani? Nani anaruhusu mambo haya yanatokea? Mambo haya yanatoka wapi; na nini maana ya mambo haya yote?

Swali kwamba mambo haya yote yanatoka wapi au yanaletwa na nani linaweza lisifahamike na wote lakini ni dhahiri kwetu wote. Haya yote ni mambo ya akili. Yanatoka kwa akili na yanaletwa na akili. Ni akili ndio inaleta teknolojia, ndio pia inatupatia elimu.

Akili ndio imeleta haya yote: elimu na teknolojia; na maendeleo yake yote. Ndio hiyo hiyo akili imeweka na kuanzisha ulimwengu. Ndio akili hiyohiyo imemweka mtu duniani, ambapo ndio yenyewe inahusika na mageuzo yote yenye maendeleo.

Kwa hiyo haya maendeleo ya teknolojia katika viwango vyake vyote ni akili yenyewe ndio imeruhusu yawe hivyo, yatokea, na yaeendelee. Akili ndio imemweka mtu duniani na ndio anatoka kwake, na teknolojia inatoka kwake pia; na ndio yenyewe imeruhusu maendeleo ya elimu na teknolojia.

Swali hapa ni: kwa nini watu wanahofu juu ya mambo ya akili, ambayo pia ndio chanzo chao? Nini watu wanahofu juu ya teknolojia au maendeleo yake? Kwa nini watu wanahofu kwamba teknolojia inakuja kuchukua nafasi ya kazi ya mtu?

Kosa kubwa ni matumizi ya mambo ya akili na kuelewa dunia kadiri ya mpango wa akili yenyewe. Hakuna mambo ya akili au maendeleo yake, ambayo ni hatari kwa mtu isipokuwa matumizi ya elimu au teknolojia hiyo.

Tofauti na viumbe wengine duniani, mtu amepewa akili ambayo ameipata kutoka kwa akili yenyewe. Kuhusu akili maana yake ni kufikiri, kuchunguza, kufuatilia na kuamua.

Asiye na akili ni mtu yule anaekosa hali ya kufikiri, kuchunguza, kufuatilia na kuamua, na kwa kuwa hivi mtu anakuwa bora ya mnyama.

Watu kwa sababu ya kutokufikiri, kuchunguza, kufuatilia na kuamua wanashindwa kukabiliana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani kwa kuwa hawakujiandaa.

Kwa sababu watu wengi hawamiliki tena akili, kwa hiyo wanaona maendeleo ya teknolojia yanatishia usalama wao; kwa kuwa wengi hawakuwa wamejiandaa kwa mabadiliko au maendeleo hayo.
 
Akili inauwezo wa kuwasiliana na roho au nafsi
 
Back
Top Bottom