Chongolo uwe na amani, uchunguzi utafanyika na utatendewa haki. Chama kitaonesha ukubwa wake

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kwanza, tunamshukuru Mungu kwa kuzuia hujuma zisizo na huruma kwa CCM yetu baada ya kuepusha kupokwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu jana. Shukrani zetu, kama makada waandamizi na wazee wa chama, ni kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia S. Hassan kwa kutusikiliza tulipomshauri cha kufanya.

Hatimaye, Katibu Mkuu wa CCM atapatikana kiutaratibu wa kiustaarabu na adabu. Si majungu ambayo hata Mungu anayapiga rungu. Mwenyekiti wetu, kwakuwa aliomba na kupokea ushauri mashuhuri, amefanikiwa kuukwepa mtego wa kupokwa Ukatibu Mkuu wa CCM.

Uchunguzi umeagizwa ufanyike wakati nafasi hiyo ikikaimiwa na Komredi Anamringi Macha. Uchunguzi wa kina utafanyika kwenye tuhuma zilizoelekezwa kwa Katibu Mkuu Mjiuzulu Daniel Chongolo. Uchunguzi pia utazingatia maelezo yake aliyoyatoa na atakayoyatoa chamani.

Komredi Chongolo, just relax uwe na amani. Kwakuwa Kamati Ndogo ya Uchunguzi imeshaundwa na leo inaanza kazi yake, haki itatendeka. Katika sakata hili la Chongolo, CCM itaonesha ukubwa wake. Haitavumilia chama 'kutekwa' na waroho wa madaraka wenye haraka isiyo na baraka.

Walioratibu mpango dhidi ya Chongolo wanapaswa kujua jambo moja. Chongolo ni mwana wa Serikali na chama. Amefanya kazi ya kutukuka na kusifika Serikalini na chamani. Hawezi kuondoka bila kishindo kikubwa chamani. Ripoti itaanika kila kitu. Ukweli na usio ukweli. Heri au shari.

Katibu Mkuu hatapatikana hadi uchunguzi ukamilike. Wa kusafishwa atasafishwa na wakuwajibishwa atawajibishwa. Hakuna upendeleo wala video kwenye jambo hili. Narudi zangu Kilosa nikifurahi kuilinda nafasi ya Katibu Mkuu kwa ajaye au atakaporejeshwa huyu.

Gekul, yalikuwa ndiyo madaraka ya kulevya?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kuelekea Kilosa, Morogoro)
 
Kwanza, tunamshukuru Mungu kwa kuzuia hujuma zisizo na huruma kwa CCM yetu baada ya kuepusha kupokwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu jana. Shukrani zetu, kama makada waandamizi na wazee wa chama, ni kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia S. Hassan kwa kutusikiliza tulipomshauri cha kufanya.

Hatimaye, Katibu Mkuu wa CCM atapatikana kiutaratibu wa kiustaarabu na adabu. Si majungu ambayo hata Mungu anayapiga rungu. Mwenyekiti wetu, kwakuwa aliomba na kupokea ushauri mashuhuri, amefanikiwa kuukwepa mtego wa kupokwa Ukatibu Mkuu wa CCM.

Uchunguzi umeagizwa ufanyike wakati nafasi hiyo ikikaimiwa na Komredi Anamringi Macha. Uchunguzi wa kina utafanyika kwenye tuhuma zilizoelekezwa kwa Katibu Mkuu Mjiuzulu Daniel Chongolo. Uchunguzi pia utazingatia maelezo yake aliyoyatoa na atakayoyatoa chamani.

Komredi Chongolo, just relax...uwe na amani. Kwakuwa Kamati Ndogo ya Uchunguzi imeshaundwa na leo inaanza kazi yake, haki itatendeka. Katika sakata hili la Chongolo, CCM itaonesha ukubwa wake. Haitavumilia chama 'kutekwa' na waroho wa madaraka wenye haraka isiyo na baraka.

Wanatafutwa TROJAN ili waende kusumbua upinzani.
Siasa hazina uadui wala urafiki wa kudumu ni mwendo wa maslahi tu.
 
Hata mimi naona busara imetumika sana. Maana kampeni zilishaanza kupigana vikumbo. Hongera mh Rais na mwenyekiti wa chama. Hapa kuna watu wamenuna na leo wameamka na moody... wa mtaani wanasema 'limewashuka'
Suzy Elias . Vipi upepo unaelekea wapi kuhusu mtu wako kuwa KM? Nahisi umenuna leo
 
Ile sio barua ya kujiudhuru ya kumpelekea mwenyekiti. Ni barua ya kuweka public kujielezea kwanini anaachia nafasi with intentions za kuonyesha CCM hakuko sawa. Ndio maana habari zikafika mitandaoni kabla ya hata CCM kutangaza.

Barua ya kujiudhuru ni breaf kwa kumbukumbu tu za chama. Maelezo mengine yote yale yalitakiwa kuwa private talk kati yake na mwenyekiti.

Kama kuna mambo yalikuwa haya mfurahishi au anadhani kuna njama chafu juu yake KM anawezaje kulalamika mitandaoni kabla ya kupeleka kwa mwenyekiti wafanyie uchunguzi, apime reaction yao kama wapo upande wake au la.

Ni bad move if anything kuachia nafasi na kuweka info publicly kuna verify fikra za ‘bi tozo’ kuna kundi linamipango mengine na yake ndani ya CCM. Sasa mwenyekiti wa CCM na raisi wa nchi akiamua kutumia madaraka yake kawaida hakuna wa kumsumbua.

Watazamaji yetu macho to how this infighting drama will evolve leading up to the general election.

Alichobugi Chongolo ni kutaka jamii yote ijue, kabla ya CCM kutoa tamko, kuonyesha kuna mfarakano.
 
Hii issue ya Makonda kuhusishwa na ukatibu mkuu imenifungua macho kwenye mambo kadhaa...

- Kumbe hili kundi linaloitwa SG lipo, linaishi, na lina nguvu ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ndio maana kwa namna fulani linaweza kuwavuruga kila litapoamua kufanya hivyo, nanyi kujibu mapigo inawalazimu kuhitaji muda kujipanga.

- Samia kama mwenyekiti wa CCM ni dhaifu, hajui ashike wapi wala aende na nani, au amsikilize yupi na asimsikilize nani, yupo yupo tu, ndio maana haya makundi yanaendelea kumyumbisha licha ya kuonesha dalili ya kujipanga muda mrefu uliopita kwa kuwaondoa wakina Lukuvi na Kabudi barazani.

- Kuna wastaafu ndani ya CCM wasiochoka kuitafuna kila wapatapo nafasi, hawaaminiki na yeyote, hawa wakiona upepo unavuma upande wao watasimama na mwenyekiti wao, lakini wakiona upepo unavuma upande mwingine, hawakawii kumgeuka mwenyekiti, ni mafisi wasio na aibu na ndio wanaunda kundi lingine na watoto wao.

- Kuelekea 2025, Samia anaweza kujikuta analazimika kutafuta uungwaji mkono toka sehemu nyingine, endapo hataendana na kile wale aliowaamini mwanzo watakachokitaka, atajikuta analazimika kutafuta uungwaji mkono mpya, na hapa ndio atakuwa kwenye hali mbaya zaidi, kwani muda hautakuwa upande wake, hivyo asishangae ikitokea akipigwa chini.

- Kwa hali ya mambo ilivyo, bado naiona panga pangua kwenye chama na serikali kuelekea 2025. Samia lazima aendelee kuwachuja wale atakaokuwa na mashaka nao, na kuwasogeza karibu wapya atakaoamini wataweza kumfikisha kule anapotaka kwenda.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwanza, tunamshukuru Mungu kwa kuzuia hujuma zisizo na huruma kwa CCM yetu baada ya kuepusha kupokwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu jana. Shukrani zetu, kama makada waandamizi na wazee wa chama, ni kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia S. Hassan kwa kutusikiliza tulipomshauri cha kufanya.

Hatimaye, Katibu Mkuu wa CCM atapatikana kiutaratibu wa kiustaarabu na adabu. Si majungu ambayo hata Mungu anayapiga rungu. Mwenyekiti wetu, kwakuwa aliomba na kupokea ushauri mashuhuri, amefanikiwa kuukwepa mtego wa kupokwa Ukatibu Mkuu wa CCM.

Uchunguzi umeagizwa ufanyike wakati nafasi hiyo ikikaimiwa na Komredi Anamringi Macha. Uchunguzi wa kina utafanyika kwenye tuhuma zilizoelekezwa kwa Katibu Mkuu Mjiuzulu Daniel Chongolo. Uchunguzi pia utazingatia maelezo yake aliyoyatoa na atakayoyatoa chamani.

Komredi Chongolo, just relax...uwe na amani. Kwakuwa Kamati Ndogo ya Uchunguzi imeshaundwa na leo inaanza kazi yake, haki itatendeka. Katika sakata hili la Chongolo, CCM itaonesha ukubwa wake. Haitavumilia chama 'kutekwa' na waroho wa madaraka wenye haraka isiyo na baraka.

Walioratibu mpango dhidi ya Chongolo wanapaswa kujua jambo moja. Chongolo ni mwana wa Serikali na chama. Amefanya kazi ya kutukuka na kusifika Serikalini na chamani. Hawezi kuondoka bila kishindo kikubwa chamani. Ripoti itaanika kila kitu. Ukweli na usio ukweli. Heri au shari.

Katibu Mkuu hatapatikana hadi uchunguzi ukamilike. Wa kusafishwa atasafishwa na wakuwajibishwa atawajibishwa. Hakuna upendeleo wala video kwenye jambo hili. Narudi zangu Kilosa nikifurahi kuilinda nafasi ya Katibu Mkuu kwa ajaye au atakaporejeshwa huyu.

Gekul, yalikuwa ndiyo madaraka ya kulevya?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kuelekea Kilosa, Morogoro)
Uchunguzi kwani ana tuhuma gani? Msituzingue hapa
 
Back
Top Bottom