Chonde chonde Rais Samia, Kipengele cha Dini kwenye sensa ni muhimu sana kwa sababu hii

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,836
Rais wetu usifungwe kwa miiko, watu wengi ikiwemo wewe wameleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa kuvunja miiko, tuangalie faida na hasara zake sio kwa kuwa halikuwahi kufanyika

Hili suala haina haja ya kulichukulia kwa shari na kutokuaminiana, tujadili kwa utulivu na kwa reason

Dini imekuwa sehemu muhimu sana ya maisha ya mtanzania na kwa maana hiyo utamaduni wa Watanzania wengi umeathiriwa na dini waliyo nayo

Na utamaduni una effect kubwa kwenye maendeleo ya mtu, jamii na taifa

Mfano mikoa ambayo ipo percived kuwa na waislam wengi, nasema percived kwa sababu hakuna takwimu rasmi

Mikoa hii ni kama Kigoma, Lindi, Tanga, Mtwara na wilaya za mkoa wa Pwani zilizo mbali na Dar, mikoa hii kumekuwa na umasikini mkubwa na huduma za kijamii kama Hospitali, shule, barabara pia ni duni, sasa tunataka kujua kuna uhusiano wowote kati ya maendeleo ya mkoa huu na dini (ambayo ina infuence culure yake?) au ni mikoa ambayo Serikali ilijisahu kwa bahati mbaya tu kupeleka maendeleo kama mikoa mingine?

Na kama haina maendeleo kwa sababu ya kusahaulika na serikali, basi tuseme umasikini wao umechangiwa na culture yao ambayo kwa kiasi kikubwa inaathiriwa na Dini? Basi ikionekana utamaduni/dini ndio imechangia, basi Serikali ina kazi ya kufanya maana Dini ya Kiislam haimaanishi kukataa maendeleo, maana mataifa yaliyoendelea zaidi Afrika kama Egypt na Morocco ni ya Kiislam

Hii ni analysisi ya muhimu inayotakiwa kufanywa na Serikali kama serikali ina nia ya dhati ya kuleta kuondoa umasikini kwa usawa maeneo yote TZ


So hapa ndipo kipengele cha Dini kinakuwa cha muhimu,

Na sio hapa tu, pia serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi za kidini za Kikristo na Kiislam kwenye maendeleo na ustawi wa Tanzania, kwa hiyo kuwa na takwimu kuhusu waumini wa imani fulani na ku share takwimu hizi na taasisi hizo za kidini ambazo zinashirikiana nao, italeta manufaa mengi kwa pande zote

Mfano Bakwata, Balozi za mataifa mbalimbali, na watu binafsi wamekuwa wakishirikiana na Serikali kujenga visima na misikiti kwenye maeneo yenye Waislam, hivyo serikali ingetupa takwimu tukajua maeneo ambayo yangepewa kipaumbele.


Pia soma: Rais Samia: Sensa haitauliza kuhusu Dini ya mtu
 
Kipengele cha dini hakina tija yoyote. Kuna wengine hatuna dini je itakuwaje?

Pia kipengele cha kabila nacho hakina tija. Mimi baba yangu ni Mmasai na mama ni Mchaga ila nimezaliwa na kukulia uchagani mpaka nimekuwa mtu mzima na hata kwa baba yangu huko Nainokanoka sijawahi kufika.

Najua mila na tamaduni za kichaga na lugha ya kichaga naijua pia ila kimasai sikijui.

Je mimi ni Mmasai au ni Machagga?
 
Kipengele cha dini hakina tija yoyote. Kuna wengine hatuna dini ne itakuwaje?

Pia kipengele cha kabila nacho hakina tija. Mimi baba yangu ni Mmasai na mama ni Mchaga ila nimezaliwa na kukulia uchagani mpaka nimekuwa mtu mzima na hata kwa baba yangu huko Nainokanoka sijawahi kufika...
Nimeorodhesha sababu kadhaa hapo sijui umesoma au umekimbilia tu kujibu
 
Wa kundi fulani kujiona wako wengi na wengine labda wachache, unadhani miaka yote kwanini serikali huwa haiweki hiki kipengele cha dini?
Lengo sio hilo, nimeweka faida nyingi tu hapo, mnaodhani lengo ni hilo ndio mnaoliangalia suala hili kishari
 
Ulisoma historia?

Mbona sasa hiyo study unaweza kuifanya mwenyewe tu bila hata kuingizwa kwenye sensa?
jiulize kwanini shule za kata/wazazi zilianzia Kilimanjaro ?

Kwanini watu wa Hai hawazungumzii changamoto za maji kama watu wa Mwakidira TANGA/KABUKU nk?
 
Watu wanajua kuvaa kanzu, kufuga ndevu na majini maendeleo watayatafutaje?
Punguza chuki mkuu...

Katika vitu ambavyo vimeshakuwa na uwezi kuvibadili tena, tukisema wote tuwe na akili kama zako...
Ata umoja wa kitaifa usingekuwepo na sababu ikiwa ni vitu tulivyoletewa tena ikiwa sio asili ya mwafrica!

Tumikia unachokiamini, lakini usiwe mtumwa wa imani kwa kuhisi wewe ndo huko sawa..!
 
Kipengele cha dini hakina tija yoyote. Kuna wengine hatuna dini ne itakuwaje...
Kama hujawahi kwenda kwa baba yako na wala hujui lugha wala utamaduni wake unataka sisi tukusaidieje? Je wote nchini ni kama wewe? Hilo swali linakuhusu wewe mwenyewe ujitafutie jibu. Kwa kifupi mtoa mada ameeleza japo kwa kiasi faida za uwepo wa kipengele cha dini.

Sasa nawe unayekataa ulipaswa kueleza kwa mifano hiyo atahari ya uwepo wa takwimu za waumini wa dini na madhehebu mbalimbali ni zipi? Wewe kutokujua kabila lako n.k sio athari ya kuwepo kipengele au uhitaji wa kuwa na takwimu za waumini.
 
Hakuna haja ya kujua dini ya mtu...
Hasa katika mambo ya kiserikali, kwani tulishakubaliana serikali aina dini!
Serikali hana dini, ila watu wake wanadini na serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu hao. Na ndio maana mtumishi wa serikali akifa itashughulikia maziko yake kwa mujibu wa imani yake. Au hata wewe ukikutwa leo mfano umekufa na ukasachiwa mfukoni ukakutwa na kitamburisho unaitwa John Richard (Mkristo) utazikwa kwa imani hiyo. Huoni kuwa serikali inauhitaji wa kufahamu dini yako? Ukizungumzia mipango ya maendeleo aidha kijamii, uchumi, nk huwezi kuepuka matumizi na uhitaji wa takwimu sahihi. Utachekesha.
 
Ngoja nione kama nimekupata vizuri...., Kwamba kuna Mikoa ambayo ipo nyuma kimaendeleo na ni Masikini..., kwahio hapo kama common denominator ni Dini / Imani Fulani tuweze kujua ili kusaidia....

Mfano unagundua tatizo ni Imani potofu (kama baadhi ya makabila ya ukeketaji) je utaanza kuwaambia / kuwafundisha au kuwaabia hao watu waachane na Imani yao ? Kama hio Imani ipo intertwined kwenye Dini huoni itakuwa ni kazi kubwa ?

Kwanini shortcut isiwe kuondoa umasikini, ujinga na maradhi popote unapoonekana be it mkoa gani au watu wengi ni wa Imani gani...

Sababu hayo matatizo hayachagui Imani, na kama kuna Imani potofu ni jukumu la kila raia na hata viongozi wa hio Imani kuweza kuinyoosha hio Imani...,
 
Back
Top Bottom