Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS

kama tuna zungumzia utawala bora, basi chikawe na aliye mtuma wamekosa hiyo sense ya utawala bora, na wanatakiwa waelewe maana ya kuwepo kwa kikao cha baraza la mawaziri.
kiwango cha pesa kinacho ongelewa ni juu ya uwezo wa waziri husika kukiongelea bila kukipeleka kwenye baraza la mawaziri, ila ikiwa nia ni kujaribu maji ya moto ya baridi, kwa maana nyingine ikiwa kuna nia mbaya ndio utaratibu kama huu hutumika.
hii ni sawa sawa kwenye kampuni kuna level ya kusaini shs 10m, halafu 100m na kuendelea mpaka issue ya bodi nk nk.
jingine je utawala bora ulifuatwa katika kuingia huu mkataba? sheria zilifuatwa? au utawala bora unakuwepo pale mtawala/watawala wanapo waibia wananchi?

Heshima mbele Mkuu...........

Utawala bora pia una-support UWAZI NA UKWELI..............Mr. Chikawe hebu tuambie kuwa HATUIBIWI NA DOWANS............nitakuwa wa kwanza kukuunga mkono na kauli zako.......kwani its part of UTAWALA BORA.........kutunza siri za yaliyotokea kwenye serikali ambayo wewe ulikuwa Waziri wa Sheria na Katiba..............
 
Ndugu zangu wa JF,

Habari Leo limetoka na habari kuwa waziri wa utawala bora mathias chikawe amepingana na kulaumu kauli za mhe. Sitta na mhe. Dr. Mwakyembe za kutaka serikali isiilipe Dowans kwani ni kampuni ya kitapeli.

Anachosema kina mantiki kwamba wao kama mawaziri wana channels zao za kufikisha uamuzi wowote wanaoupinga ndani ya serikali badala ya kutumia vyombo vya habari.

Binafsi siwalaumu mzee sitta na dr. Mwakyembe kwani pamoja na uelewa wao wa taratibu zinazozungumzwa na chikawe lakini wameshindwa kuvumilia kukaa kimya kutokana na uzalendo kwa nchi yao. Wote wawili wanalifahamu vizuri suala la Dowans na wana uhakika kuwa ni utapeli tena mbaya zaidi unaofanywa na watanzania wenzetu. Suala la Dowans linatia uchungu tena mkubwa sana.

Kwa mtazamo wangu, ni bora viongozi wetu hao (sitta na mwakyembe) ili kulinda heshima yao kwa kujiondoa kwenye serikali inayotetea na kusimamia maamuzi ya kunyonga wananchi wao maskini.

Kwa Mh. Sitta na Mwakyembe kulipwa kwa Dowans ni sawa na kuchwapwa kofi la kelbu na Rostam, kwa kweli hata ningelikuwa mimi ningezoza tuu. Hebu tusubiri mimi natabiri mwisho wa uwaziri wa either Sitta na Mwakyembe au Ngeleja, Ushindi wa Dowans na Muanguko wa CCM na Kikwete au Ushindi wa wanatz
 
Kwa bahati mbaya hawakulazimishwa na walikuwa na bado wanahaki ya kukataa nafasi zile. Hizi kauli zao zinatofauti gani na wafanyakazi wanaomwibia mwajiri wao? Au marketing officer anayachafua bidhaa za kampuni aliyoajiriwa. Upuuzi wa namna hii haupo. Hapa ninasisitiza aidha watoke serikalini au wafunge midomo yao.[/QU


kilichopeleka wao kuongea ni baada yakuona suala ilo linaendeshwa kinyemela bila kushirikisha baraza la mawaziri wala bungu.
 
Chikawe,Tanzania hailindi sheria,sheria ndo zinailinda Tanzania. Tunaka wenye akili timamu ndo waongee. Chikawe,usishindwe na wanafunzi wa kidato,Loleza,juzi nilisikia wakimdiscuss Mwakyembe kwenye daladala pale mwanjelwa wakidokeza kuwa mwakyembe ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ktk kuichunguza kikundi cha wahuni-Richmond kwa iyo ana haki ya kuendelea kulinda mapendekezo ya kamati mpaka yatakapokuwa mameshughulikiwa,hata angeukosa ubunge alipaswa kuendelea kuileza jamii hata kama angekuwa ameanza kulima mpunga huko kyela baada ya kuukosa ubunge. Sasa chikawe tukulinganishe na nani? Pia mzee 6 ni mbunge aliyewahi kuwa spika,unajua maana ya spika! Huwezi kujua siri za serikali wewe chikawe zaidi ya spika,sio saizi yako!
 
Sitta, Mwakyembe matatani serikalini
• Kauli zao dhidi ya Dowans zawaponza

na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, wanaweza kupoteza nafasi zao za uwaziri kutokana na hatua yao ya kuibua mjadala dhidi ya mawaziri wenzao nje ya Baraza la Mawaziri kuhusu uamuzi wa serikali kukubali kuilipa Kampuni ya Dowans Holdings SA, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezinasa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya serikali zinaeleza kwamba, hatua ya Sitta na Mwakyembe kutoa kauli zinazoonyesha kupingana na hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, zimeleta mkanganyiko mkubwa serikalini.
Mkanganyiko huo unaelezwa ndio ambao umesababisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, Mathias Chikawe, kutoa matamshi makali ya karipio kwa mawaziri hao wawili.
Ukali wa matamshi hayo ya Chikawe uliongezwa na tamko lake la kuwataka Sitta na Mwakyembe iwapo wanataka kuendeleza malumbano hayo nje ya utaratibu wa kawaida wa mawasiliano wa mawaziri kujiondoa serikalini.
Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili inazo zinaeleza kwamba Chikawe ametoa karipio hilo baada ya kupata baraka za kufanya hivyo kutoka mamlaka za juu.
“Kwa utaratibu wa kawaida, Chikawe asingeweza kutoa matamshi yale mazito dhidi ya Sitta na Mwakyembe iwapo angekuwa hajapata baraka za Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda,” kilieleza chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na gazeti hili ambacho kiko karibu na Ofisi ya Rais.
Habari zaidi zinaeleza kuwa pamoja na karipio hilo la Chikawe kumekuwa na mjadala wenye mwelekeo wa kutaka mawaziri hao waandikiwe barua ama za karipio au za kutakiwa kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni hatua yao ya kukiuka misingi ya uwajibikaji wa pamoja.
Mbali ya kosa hilo, kama alivyonukuliwa akisema Chikawe katika gazeti la serikali la Habari Leo toleo la jana, Sitta kwa upande wake anakabiliwa na tuhuma nyingine zaidi za kutoa siri za Baraza la Mawaziri.
Chikawe amekaririwa akisema, kitendo cha Sitta kumtuhumu Ngeleja kwamba alitangaza kulipwa kwa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa katika Baraza la Mawaziri kinakwenda kinyume cha miiko ya uwaziri kinachomtaka kutotoa siri za baraza.
Kwa mujibu wa Chikawe, Waziri Ngeleja kwa mamlaka aliyonayo kama waziri mwenye dhamana na masuala ya nishati alikuwa na mamlaka ya kutoa tamko alilotoa baada ya kufanya mashauriano na wataalamu mbalimbali wa masuala ya sheria serikalini.
Chikawe alisema iwapo Sitta na Mwakyembe walikuwa hawajaridhishwa na uamuzi wa Waziri Ngeleja walikuwa na njia za kuwasilisha hoja zao pasipo kutumia vyombo vya habari.
Kwa upande wake, Mwakyembe ameingia matatani kutokana na kunukuliwa na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akieleza kushangazwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICC) iliyoipa ushindi Dowans dhidi ya serikali na kutakiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 94.
Katika hatua inayoonyesha kwamba, hatua hiyo ya Sitta na Mwakyembe imetikisa ngome za uongozi ndani ya serikali, juzi katika kikao cha Kamati ndogo ya mawaziri uliibuka msuguano wa hoja kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Werema na Waziri Sitta.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata kutoka ndani ya kikao hicho ambacho kilifanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, zinaeleza kuwa Jaji Werema alieleza kusikitishwa na matamshi ya Sitta katika vyombo vya habari.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimemkariri Werema akieleza kushangazwa na hatua ya Sitta kuwashambulia yeye na Ngeleja huku akijua kuwa walichofanya na kuamua kilikuwa ninagusa moja kwa moja mamlaka yao ya kiwajibu na kimamlaka.
Jaji Werema amekaririwa akimweleza Waziri Sitta kwamba iwapo kweli alikuwa ana uchungu na suala hilo la Dowans, basi wakati kesi ikiendelea alipaswa kuisaidia serikali katika kuwasilisha utetezi dhidi ya malalamiko 17 yaliyokuwa yamewasilishwa na kampuni hiyo.
Habari zinaeleza kwamba hatua ya Sitta ambaye alikuwa akitambua fika namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendelea kutochangia jambo lolote wakati shauri hilo likiwa ICC na badala yake kusubiri hadi serikali ishindwe ndipo aanze kutoa matamshi katika vyombo vya habari ilikuwa ni ya kuchochea hasira za wananchi dhidi ya viongozi pasipo sababu zozote.
Tanzania Daima Jumapili limeelezwa kuwa wakati Jaji Werema akimshushia lawama Sitta kwa muda usiopungua dakika 15, Waziri Mkuu Pinda alikuwa kimya muda wote.
Baada ya kumaliza hoja yake, Waziri Mkuu aliwataka wajumbe wa kamati hiyo ya mawaziri iliyokuwa ikijadili kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi unaotarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lijalo kuendelea na mjadala.
Awali kabla ya Werema kuzungumza, Sitta alichangia kuhusu muswada huo na akaeleza haja ya kuwekwa kwa masharti magumu zaidi katika muswada huo ili kuzuia uwezekano wa makampuni ya kitapeli kuweza kujipenyeza nchini na kuigharimu serikali mamilioni ya fedha.
Mtoa habari aliyezungumza na gazeti hili alisema hatua ya Sitta kusisitiza kwa zaidi ya mara moja haja ya kuwekwa kwa sheria zitakazobana makampuni ya nje ya kuzuia serikali kupatwa na kadhia ya kulipa faini kubwa pasipo kutaja jina la taasisi yoyote ndiyo iliyoonekana kumkera Werema.
Inaelezwa kuwa Werema aliposimama alimtaka Sitta kutotafuna maneno na badala yake kueleza wazi kwamba hoja yake hiyo ilikuwa ni mwendelezo wa ajenda yake ya Dowans aliyoanza kuizungumza kupitia katika vyombo vya habari.
Juhudi za Tanzania Daima Jumapili kuzungumza na Sitta ili kueleza kuhusu tamko la Waziri Chikawe dhidi yao ikiwa na kujua undani wa sakata lake na Werema hazikuzaa matunda kwani muda wote alipotafutwa simu yake ilikuwa imezimwa.
Kwa upande wake, Mwakyembe alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu kile alichokuwa akitafutiwa na gazeti hili alimweleza mwandishi wetu kwamba alikuwa yuko msibani na akakata simu.
Awali Mwakyembe alimuuliza kwanza mwandishi iwapo alimpigia simu kwa ajili ya kumpa pole ya msiba na baada ya kuambiwa kile alichokuwa akitafutiwa alikata simu yake na juhudi za kumpata baada ya hapo hazikufanikiwa.
 
JK akiwafuta kazi Sitta na Mwakyembe tutajua kweli yeye ni fisadi namba moja hapa nchini kama Dr. Slaa alivyotutonya wakati wa kampeni za Uraisi............................................
 
Pameanza kuwa patamu. Ukiangalia kwa makini hoja ya Sitta na ya wananchi wengine si hasa suala la serikali ya Tanzania kushindwa katika kesi bali ni maswali kama haya: ilikuwaje Richmond ilyokuwa kampuni hewa ikarithisha mkataba wake kwa Dowans Tanzania? mmiliki wa Dowans ni nani? kama ambavyo Ngeleja alitaja kuwa Dowans Costarica ni mbia mkubwa katika Dowans Tanzania, mbona Dowans Costarica tulishaambiwa kuwa hawapo katika faili la msajili wa Kampuni kule Costarica?Mbona hukumu hiyo hatujaambiwa kuwa imesajiliwa mahakam kuu ya Tanzania?

Hayo maswali madogo madogo hayajibiwi bali tunang'ang'ania kwenda kwenye maswali magumu ya kisheria. Hili suala limeendeshwa kisiasa kweli. Hata hao wanaomtuhumu Sitta na Mwakyembe hawajibu hoja zao wala za Watanzania bali wanaongeza maswali. Wanarukia suala la kuwalipa Dowans kabla hata hukumu haijasajiliwa mahakama kuu wala serikali kufanya jitihada zozote ya kujitetea.Hata kama nchi tumeshindwa katika kesi hiyo, bila kuwawajibisha waliotufikisha hapo tunataka kuwafanya Watanzania kuwa ni mazezeta.
 
Kikwete ni Mawana Demokrasia namba moja na ndio maana unaona Serikali, ikijadiliwa vya kutosha na yeyote yule atakae. Hakuna sababu za msingi za kuwaondoSitta na Mwakyembe, wamesema wanayoona wao sawa mradi hawakuvunja shria, iwapo wamevunja kanuni za baraza la mawaziri, hili ni jambo ambalo litashughulikiwa ki kanuni.
 
Ndugu zangu wa JF,

Habari Leo limetoka na habari kuwa waziri wa utawala bora mathias chikawe amepingana na kulaumu kauli za mhe. Sitta na mhe. Dr. Mwakyembe za kutaka serikali isiilipe Dowans kwani ni kampuni ya kitapeli.

Anachosema kina mantiki kwamba wao kama mawaziri wana channels zao za kufikisha uamuzi wowote wanaoupinga ndani ya serikali badala ya kutumia vyombo vya habari.

Binafsi siwalaumu mzee sitta na dr. Mwakyembe kwani pamoja na uelewa wao wa taratibu zinazozungumzwa na chikawe lakini wameshindwa kuvumilia kukaa kimya kutokana na uzalendo kwa nchi yao. Wote wawili wanalifahamu vizuri suala la Dowans na wana uhakika kuwa ni utapeli tena mbaya zaidi unaofanywa na watanzania wenzetu. Suala la Dowans linatia uchungu tena mkubwa sana.

Kwa mtazamo wangu, ni bora viongozi wetu hao (sitta na mwakyembe) ili kulinda heshima yao kwa kujiondoa kwenye serikali inayotetea na kusimamia maamuzi ya kunyonga wananchi wao maskini.
Hapa hakuna kuondoka kama Mrema, hadi kieleweke, kama alikuwa anataka kuwaziba midomo limekula kwake, swala la common decesion, kwa mawaziri wangesubiri wangesutwa ndani ya baraza lao chafu la akina makongoro, ni vizuri walivyofanya ngereja amemwaga mboga(kutosubiri uamuzi wa mawaziri na kutangaza) watetezi wa nchi wakamalizia ugali wakaweka peupe wadanganyia wasome namba wajue ninichakufanya.
Mwneye lawama zote mkulu suji, anatakiwa akalishe chini baraza lakw wajue kulipa ni hatari zaidi kuliko kukubali kukaidi kulipa kwani hakuna uv=bishi wanao tetea malipo wanamaslahi binafsi lkn wawili kwa maslahi ya nchi,
Katiba ya chama inausemi mmoja '' nitasema kweli daima, uongo kwangu mwiko'' je walichosema ni uongo au wametimiza ahadi ya chama?
Waacheni wenye uchungu na nchi wafenao humohumo kwenye chungu wakiwalazimisha kung'oka tutawauliza je kwa kusema ukweli nikukosea au wanaotetea uongo ndiyo watoke?
Mjenga nchi ni mwananchi na mvunja nchi ni mwananchi, je yupi anastahili kupewa sifa auvunjae kama mafisadi au Maprofesa wa mafanikio ya nchi yetu?
Mungu wangu walinde sn hawa ndugu ambao ni wawakilishi wa kweli wa wananchi.
Mungu ibarki Tanzania.
 
Ndugu zangu wa JF,

Habari Leo limetoka na habari kuwa waziri wa utawala bora mathias chikawe amepingana na kulaumu kauli za mhe. Sitta na mhe. Dr. Mwakyembe za kutaka serikali isiilipe Dowans kwani ni kampuni ya kitapeli.

Anachosema kina mantiki kwamba wao kama mawaziri wana channels zao za kufikisha uamuzi wowote wanaoupinga ndani ya serikali badala ya kutumia vyombo vya habari.

Binafsi siwalaumu mzee sitta na dr. Mwakyembe kwani pamoja na uelewa wao wa taratibu zinazozungumzwa na chikawe lakini wameshindwa kuvumilia kukaa kimya kutokana na uzalendo kwa nchi yao. Wote wawili wanalifahamu vizuri suala la Dowans na wana uhakika kuwa ni utapeli tena mbaya zaidi unaofanywa na watanzania wenzetu. Suala la Dowans linatia uchungu tena mkubwa sana.

Kwa mtazamo wangu, ni bora viongozi wetu hao (sitta na mwakyembe) ili kulinda heshima yao kwa kujiondoa kwenye serikali inayotetea na kusimamia maamuzi ya kunyonga wananchi wao maskini.
Hapa hakuan kutoka kama Mrema, mpaka kieleweke, kukubaliana kufanya uchafu eti uamuzi wapamoja haiwezekani kukumbatia ubaya eti jirani yangu, Mwaki na Sitta wamefanya vizuri sn, kama alifanya kwa kushauriwa na mafisadi awape madaraka ili kuwaziba midomo limekula kwake, ninauhakika akina Kingunge walimshauri wakali wa ufisadi wazibwe watakoma wao, haiwezekani uone jambo lililo pitishwa na Bunge linarudi eti alipwe kama nani? Je Downs wamerithi nini, mitambo na nini, je kama wamekubali kurithi mikoba ya Richmonduli ukweli ulioonekana juu ya kampuni ya mfukoni umetupwa wapi? tusiwalaumu wapiganaji wa kweli juu ya upuuzi wa maamuzi ya pamoja ya kuwaumiza wadangajika.
Nasema kama wa TZ wenyekufikiri sawasawa, tuwasurport Vingunge wa kusema ukweli mpaka huyo downs awe chini sana kama jina lake.
Kwani Bunge la tisa akina tukae(Chikawe) hawakuwepo? hawakusikia nini kilipitishwa kwa mstakabari wa nchi?
NakuambiaTukae usithubutu kuonge zaidi history itakushitaki tukij shika nchi siku zijazo.
mjenga nchi na mvunja nchi ni mwananchi ndiyo yanayotukuta leo kuwakunbalia kama RZ kuwaita wajenga nchi kumbe ndityo kwanza wanajenga kwao wamesahau wajibu kuwasaidia akina DR. Mwaki na Professor Sitta aliotekeleza ahadi mojawapo ya chama isemayo "Nitasema ukweli daima uongo kwangu mwiko" walichosema kule mjengoni 2010 hakiwezi badirika eti sasa anapew lesso wazibe midomo kama ilikuwa ni mpango wa Mingunge watasoma namba ya nyakati. "ukweli utabaki kuwa ukweli hata ukiupaka matondofi, ole wao wasemao uongo history itawashitaki.
Nawkilisha jamvini
 
Kisimsingi "DOWANS" ni majambazi/mafisadi wanaojulikana Tanzania-na ni viongozi wenye heshima. Sasa hapa limekaa vibaya sana kwao na njia pekee ni kumtisha yeyote anayejua hali halisi ili afyate mkia kuzungumuzia kadhia hiyo-maana ndo njia pekee ya kuficha majeraha na kuwaburuza watanzania waliowengi ambao hawajui kwa undani. Kuzuia maandamano na mikutano ni moja ya strategy kuzuia watu wengi wasijue kadhia hili!! Wakilogwa kumfukuza 6 na mwakyembe hapo ndo vita itakuwa nzuri!!
 
Mathayo/Mateus kama wewe ni kiongozi mahiri mwenye kusimamia Utawala Bora, basi ungekuwa mwadilifu/kama wewe ni muadilifu basi unachotakiwa kumshauri Raisi na Waziri Mkuu ni kwamba hili suala linatakiwa kwanza kujadiliwa na Baraza la Mawaziri, Pili litolewe kauli na Raisi lakini huyu kwa sababu anazo zijua mwenyewe hataki au ana penda kuwapa wenzie basi ampatie Pinda asome hilo azimio la Cabinet. Na ili kulitolea uamuzi mahari basi wanatakiwa wawapatie hao mawaziri nyaraka zote zinazo uhusiana na kadhia hiyo ili waweze kuchangia vizuri.
Baada ya hapo ndipo Sitta na Mwakyembe nk wakubali kubanwa na hiyo collective responsibility au wenyewe waamue kuachia ngazi au mwenye mamlaka ya uteuzi aamue kufanyia restructuring baraza lake la mawaziri.
Maana jambo hili ni kubwa ambalo linaleteleza taifa kingia kwenye deni kubwa/ au kupelekea shirika kufilisiwa ukifuatia maoni au ndio njia ya kutotaka hilli jambo lisiingie kwenye budget, waziri wa nishati anasema Deni hilo lilipwe na Tanesco sio Serikali. rejeas taarifa ya kwamba kitengo cha sheria cha Tanesco hakifai.
 
Siri gani hizo za kuangamiza wananchi Werema anazotaka tusizijue? Ikumbukwe kuwa Karamagi aliilazimsha tanesco kusaini mkataba akiwa Canada kwa matapeli tunaoambiwa kuwa ndio wamiliki wa dowans.
Siku wanaachia ngazi, Msabaha alisema wao ni bangusilo tu, lakini kilongola mwenyewe yupo. Huyu Kilongola naanza kuhisi kuwa anaweza kuwa mkuu wa kaya kwani nguvu inayotumika dowans walipwe inatisha!
 
Kikwete ni Mawana Demokrasia namba moja na ndio maana unaona Serikali, ikijadiliwa vya kutosha na yeyote yule atakae. Hakuna sababu za msingi za kuwaondoSitta na Mwakyembe, wamesema wanayoona wao sawa mradi hawakuvunja shria, iwapo wamevunja kanuni za baraza la mawaziri, hili ni jambo ambalo litashughulikiwa ki kanuni.
system at work
 
Huyu Chikawe anawasema Sita na Mwakyembe kwamba hawakufuata utaratibu, je yeye amefuata utaratibu? maana alipaswa kuwasubiri kwenye baraza la mawaziri ndo awaseme kuwa hawakufuata utaratibu, pia naye amechangia kutuonesha kuwa baraza la mawaziri limepasuka zaidi.
Sitta na Mwakyembe hawakutokea tu na kuanza kusema ila waliulizwa na waanndishi wa habari maoni yao. Na yeye huyo mpuuzi mwingine Ngeleja kwa nini hakushirikisha baraza la mawaziri ili wawe na say moja? akatoa tamko peke yake na swala hilo kwa sasa haliihusu wizara yake tu ni pesa ya kutoka wizara zote yaani serikalini.
Acheni kutisha watu walioelimika Chikawe.
 
Naona kama CHIKAWE amesahau kuwa SITTA alikua speaker wa bunge lililogundua kuwa HAPAKUWA NA MKATABA KATI YA RICHMOND NA DOWANS, likashauri watu wawajibishwe... CHIKAWE amesahau kwamba MWAKYEMBE alikua MWANAKAMATI HIYO YA BUNGE. Hiyo ni Historia ya SITTA na MWAKYEMBE ambayo haitaweza kusahaulika hata wakipewa URAISI, so swala lolote linalohusu Richmond na Dowans, ni lazima kupata maoni yao. Sasa ndo nahisi kumbe waliwapa uwaziri ili ikifikia hii hatua ya kuwalipa DOWANS, wasiongee? ha ha ha. Nina mashaka kwamba wakishalipwa DOWANS, wataondolewa kwenye baraza la mawazir. anyway wafukuzeni, heshima waliyoipata inathamani sana kuliko hata mali zote za ROSTAM AZIZ.
 
Nipeni hii nchni kwa dakika tano (dK.5) nairudisha kwenye mstari; wanaosumbua hapa ni wawili tu Kikwete na Rostam basi!
 
Kikwete ni Mawana Demokrasia namba moja na ndio maana unaona Serikali, ikijadiliwa vya kutosha na yeyote yule atakae.

Hivi kweli ni mwana demokrasia au Mwoga????.

Maana kampeni zake na matukio ya baada ya uchaguzi yanakinzana na dhana ya demokrasia.

Demokrasia inasemaje pale aliyekabidiwa bunduki anaamua kuua waliomkabidhi hiyo bunduki??
Matukio ya watu kuuawa shinyanga, mbeya, kimara, wachimba madini wa mahenge n.k mauaji ya arusha siongelei maana documentary tuliyoonyeshwa inasema waliouawa na wavamizi wa kituo cha polisi hawakuwa wananchi wema.
 
Kikwete ni Mawana Demokrasia namba moja na ndio maana unaona Serikali, ikijadiliwa vya kutosha na yeyote yule atakae. Hakuna sababu za msingi za kuwaondoSitta na Mwakyembe, wamesema wanayoona wao sawa mradi hawakuvunja shria, iwapo wamevunja kanuni za baraza la mawaziri, hili ni jambo ambalo litashughulikiwa ki kanuni.

Crap!
 
Back
Top Bottom