Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans, limeingia hatua mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, kusema mawaziri wawili waliompinga Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutangaza serikali kuilipa kampuni hiyo, walikiuka utaratibu wa serikali.

  Aidha, amewataka mawaziri hao, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuacha kutoa maelezo ya sekta zisizowahusu kwani si utaratibu wa utawala bora na ni kuwachanganya wananchi.


  Akifafanua kuhusu kauli zilizompinga Waziri Ngeleja, Chikawe alisema mawaziri hao walipaswa kufuata utaratibu wa kufikisha hoja zao kwa Mamlaka husika, au wajiondoe serikalini kabla ya kupingana na waziri mwenzao.


  Alisema Waziri Sitta ni mzoefu na wa siku nyingi, hahitaji kufundishwa, kwa kuwa ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na anafahamu namna za kutoa maoni kwa mawaziri bila kuathiri utaratibu.


  Kuhusu Mwakyembe, alisema ingawa ni mpya katika uwaziri, lakini ni mwanasheria wa siku nyingi na anajua utaratibu wa sheria ulivyo, hivyo pia hakuhitaji kufundishwa kuhusu namna ya kutoa mawazo yake kuhusu Dowans wakati akiwa serikalini tena Naibu Waziri.


  "Umefika wakati Sitta na Mwakyembe waache kuendesha mambo kisiasa, bali waangalie sheria zaidi katika suala la Dowans," alisema Chikawe.


  Alisema kitendo cha mawaziri hao kumkosoa Waziri Ngeleja, kutokana na kutangaza hadharani kuilipa kampuni hiyo Sh bilioni 94, kimetoa picha kuwa kuna mgongano ndani ya Baraza la Mawaziri.


  Alisema jambo zito kama hilo, halikupaswa kutolewa maelezo magazetini, bali wangetumia utaratibu wa kumfuata waziri husika na kutoa maoni na ushahidi walionao na iwapo wangeona waziri huyo hawatilii maanani, wangekwenda kwa Waziri Mkuu au Rais.


  "Unajua Rais wetu ni mwepesi sana kuwasikiliza mawaziri wake wakati wowote, sasa iwapo wangeona waziri husika hawasikilizi, wangepeleka hoja yao kwake ambaye kama angeridhishwa na hoja zao, angeitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kutoa uamuzi wa pamoja," alisema Chikawe.


  Chikawe alisema kuna utaratibu wa aina mbili, ambao waziri anaweza kuutumia kutoa uamuzi wa Serikali; kwanza ni kutoa uamuzi unaohusu wizara yake na mwingine, uamuzi wa pamoja.


  Alifafanua kuwa waziri wa sekta husika, ana jukumu la kutoa uamuzi wowote wa wizara yake bila kuingiliwa na akiona kuna jambo zito linaloathiri sera za nchi, ndio hupeleka kwenye Baraza la Mawaziri ili lijadiliwe kabla ya kutoa uamuzi wa pamoja.


  Chikawe alisema Waziri Sitta na Naibu Waziri Mwakyembe, walikuwa na nafasi ya kumwona Rais na kutoa ushahidi wao na iwapo Rais angeona kuna umuhimu wa kuitisha Baraza la Mawaziri, angefanya hivyo na si kutoa siri za Baraza kuwa hawajalijadili suala hilo.


  Alisema maoni binafsi kwa mawaziri hao si tatizo, ndiyo maana katika Baraza la Mawaziri, kikao kinaweza kujadili suala moja kwa siku nzima mpaka wanafikia uamuzi wa pamoja, lakini kuyazungumzia hadharani ni kosa, kwa kuwa wamekiuka utaratibu wa utawala bora kwa kutoa siri za Baraza hilo.


  Chikawe alimtetea Ngeleja kuwa inawezekana hakuona sababu ya kupeleka suala la kuilipa Dowans kwa Baraza la Mawaziri kwa kuwa alishirikisha wataalamu mbalimbali wa sheria na

  kujiridhisha katika kufanya malipo kwa kampuni hiyo.

  Wiki iliyopita, Waziri Sitta alipinga tamko la Waziri Ngeleja la kuilipa kampuni ya Dowans na kusema kuwa inashangaza waziri kutoa tamko hilo kabla hata Baraza la Mawaziri halijalijadili.


  Juzi pia Naibu Waziri Mwakyembe, aliibuka na kusema anashangaa kusikia kampuni hiyo aliyoiita ya kitapeli, inalipwa kwa madai kuwa ilirithi mkataba wa kufua umeme kutoka katika kampuni hewa ya Richmond LCC Ltd.


  Katika Bunge lililopita chini ya Spika Sitta, Mwakyembe aliongoza Kamati Maalumu iliyochunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond hata kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, kujiuzulu kutokana na kashfa ya kampuni hiyo.


  HabariLeo | Dowans ‘yawatafuna' Sitta na Mwakyembe
   
 2. m

  maselef JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ni mtazamo wa "Samaki mmoja akioza wote wameoza"
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa Chikawe na wewe si ungewaambia kimyakimya wao wenyewe mbona na wewe umeenda kwenye vyombo vya habari sasa!!!!

  Ungewaita na uwape ushauru huo kimyakimya!!!kwa mtazamo wangu na wewe umetereza au umetumwa uwasafishe watu kwa mjadala huo!
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kwa maoni ya huyu chikawe ni kwamba wananchi wengi wetu hapa hatujiwezi kiakili kwenye kufikiri? Wawafukuze basi hao waliokiuka tuwaone
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wacha ziumane!
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kumbe kila waziri yuko kivyakevyake hata ktk malipo makubwa kama haya?
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.
   
 8. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Yawezekana walitoa matamko mapema kweli,lakin sasa siri iko hadharani??unataka kutwambia ni halali kuwalipa hawa mafisadi?? Mkuu hapo umenoa??
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Safi sana; yeye atasema hiyo kanuni haimuhusu!
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu kwani kuna form wlioijaza kuomba huo uwaziri?
  Sii walitunukiwa tu hizo ofisi na mkulu wa kaya kama kiziba mdomo? Sasa bahati mbaya kwa serikali na ni nzuri kwa umma wa watanzania jamaa hawafungwi mdomo kwa rushwa ya cheo.
  Hii itakuwa imekula kwa mafisadi mazima!
  .
   
 11. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni sahihi kabisa watu wa namna hivi waonywe kwa namna ileile na wengine wanaofanana wasirudie hako kamchezo vinginevyo hakatakoma.
   
 12. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati mbaya hawakulazimishwa na walikuwa na bado wanahaki ya kukataa nafasi zile. Hizi kauli zao zinatofauti gani na wafanyakazi wanaomwibia mwajiri wao? Au marketing officer anayachafua bidhaa za kampuni aliyoajiriwa. Upuuzi wa namna hii haupo. Hapa ninasisitiza aidha watoke serikalini au wafunge midomo yao.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  JK awatoe basii kwani wao wanabembeeleza kuwemo serikali chafu??wewe chikawe unakiuka kiapo chako cha uwt???unasafisha upuuzi...mamama weee nchi imekwisha ona Membe alivyokuwa shujaaa....kumbuka kiapo chenu kimoja nyie usije ukayalamba matapishi yako siku ifikia??
   
 14. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ushujaa upi wa Membe wakati na yeye yupo kwenye serikali ya Kikwete?
   
 15. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Sasa Sitta na Mwakyembe wamshauri nini Kikwete, wakati taarifa nzima ya Richmond, na Dowans rais anaijua, kwa kuwa matukio yote yametokea kwenye utawala wake, TISS wanampa taarifa kila siku, wakati kesi inaendelea hapo movenpick alikuwa anajua, maoni ya wananchi kupitia vyombo vya habari anayasoma.

  Sitta alishatoa maoni yake binafsi mapema kabla ya waziri Ngeleja, kwa hiyo kama busara hiyo ndio utaratibu wa baraza la mawaziri, basi Ngeleja angemtafuta Sitta na Mwekyembe ili apate undani wa suala la Dowans kabla ya kubariki hayo malipo.
   
 16. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Rais Mwizi aende Chalinze kucheza mdundiko atuachie wenyewe tuijenge nchi yetu.
  Tuwasafishe mafisadi papa na aiache Tanzania kama ambavyo aliikuta.
   
 17. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yeye nchi yake ni ipi? Kudumisha tamaduni zetu ni tatizo? Tujadili hoja iliyopo kwenye thread hii
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  duh.. sasa Chikawe na yeye hajui kuwa kuna baraza la mawaziri? au ndio kajipa Uwaziri Mkuu kwa vile ndiye anasimamia usalama wa taifa?
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Fisadi mwingine huyu aliyeweka maslahi ya Rostam mbele kuliko yale ya nchi! Yaani anaweza kuwakemea Mawaziri ambao wanatetea maslahi ya Tanzania na Watanzania! Aaaaarrrrrgggghhhhhh!

   
 20. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wa JF,

  Habari Leo limetoka na habari kuwa waziri wa utawala bora mathias chikawe amepingana na kulaumu kauli za mhe. Sitta na mhe. Dr. Mwakyembe za kutaka serikali isiilipe Dowans kwani ni kampuni ya kitapeli.

  Anachosema kina mantiki kwamba wao kama mawaziri wana channels zao za kufikisha uamuzi wowote wanaoupinga ndani ya serikali badala ya kutumia vyombo vya habari.

  Binafsi siwalaumu mzee sitta na dr. Mwakyembe kwani pamoja na uelewa wao wa taratibu zinazozungumzwa na chikawe lakini wameshindwa kuvumilia kukaa kimya kutokana na uzalendo kwa nchi yao. Wote wawili wanalifahamu vizuri suala la Dowans na wana uhakika kuwa ni utapeli tena mbaya zaidi unaofanywa na watanzania wenzetu. Suala la Dowans linatia uchungu tena mkubwa sana.

  Kwa mtazamo wangu, ni bora viongozi wetu hao (sitta na mwakyembe) ili kulinda heshima yao kwa kujiondoa kwenye serikali inayotetea na kusimamia maamuzi ya kunyonga wananchi wao maskini.
   
Loading...