Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

HE IS NOW ON TWITTER...

10649770_1147268211980060_475816109661111715_n.jpg

samahani..lakini hii inaburudisha sana jamani..ha ah ha ha aha ha..
hii timu inakoenda siko eeh? itakuwa historia tu..cc.RRONDO.

1409087768304_Image_galleryImage_The_scoreboard_showing_th.JPG
 
kamjibu kiutu uzima..ha haha shabiki wa man kimyaaaaaaaaaaa..alaf jana wakachezea 4-0..kina RRONDO na wenzake Nzi wa chooni..ha haha ..:wacko:

After receiving abuse from a Manchester United fan on Twitter, Petr Cech ruined him with this brilliant reply. Well played!

53fb279d59f8c.jpg
The Sport Bible
 
article-0-005D1BFB00000258-638_634x402.jpg

NYUMBANI DARAJANI HAPA...MSIMU WA 2002/2003..ilikuwa CHELSEA v CHARTON

CHELSEA FC ilishinda 4-1..baadaye hawa madogo walikata rufaa kwamba u
uwanja ulikuwa mbovu ndo maana wakafungwa chelsea ilitozwa faini paundi za kutosha tu...

tunakumbushana zamani...
 
WAHESHIMIWA WOTE WA CHELSEA FC.

KWA HESHIMA 'MLIYONIPA' ACHENI TUANZE UCHAMBUZI WETU KUELEKEA MECHI YETU YA JUMAMOSI.

CHELSEA FC vs EVERTON...
SEHEMU YA KWANZA - UIMARA WA EVERTON FC.

Katika idadi ya mechi za chelsea vs everton...chelsea fc imeshinda mara nyingi zaidi.
hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni vijana hawa wa mjini Liverpool; na ambao ndo walioizaa Liverpool fc wamekuwa wagumu sana kufungika. Kama mjuavyo tumekuwa tukishinda kwa tofauti ndogo sana ya magoli kwenye mechi zetu vs Everton fc.

mfano: msimu ulopita walitunga kwao na sisi tukawafunga kwetu. Ikumbukwe kwamba katika msimu ulopita CHELSEA FC haikufungwa na timu yoyote ya top 5 isipokuwa Everton.

Everton hii ya Roberto Martinez ni tofauti sana na Everton ya d.Moyes..
Huyu kocha Martinez ni kocha mjanja, anajua jinsi ya kudhibiti timu kubwa tofauti sana na Moyes.

Mfano 2. r.Martinez alipokuwa kocha wa Wigan Athletic alichukua ubingwa wa kombe la FA. timu yake ilishuka daraja na kombe lao la FA.

Everton fC, inacheza mpira mzuri wa haraka na wanatumia sana mashambulizi ya pembeni. Kinachowasaidia sana ni wepesi wa wachezaji wao wa mbele hasa Kevin Mirallas na Steven Naismith..bila kusahau 'mwili nyumba' Romelu Lukaku, jamaa ana zaidi ya kilo 100. 'the big # 9.'

Everton Fc, wanacheza mfumo wa 4-3-3..kule mbele wanakuwa Lukaku,Naismith na Mirallas..
Katikati wanasimamaa; Gareth Barry, James Mc Cathy, na Steven Pienaar..

mabeki: Baines{kushoto}, Coleman{kulia}, kati Jagielka na Distin...
kipa wao uwezo wake unajulikana..Tim Howard..

Mechi ya jumamosi itakuwa na ushindani wa kutosha...

CHELSEA FC vs EVERTON - SEHEMU YA 2.
UDHAIFU WA EVERTON.

1. Umri wa mabeki wa kati: Jagielka miaka 32, na Distin miaka 36. Ingawa umri kwa mabeki wengi huwa si tatizo kubwa; lakini kwa Everton ni tatizo kwa sababu hawa 'wazee wawili' ni wazito wa kufanya maamuzi ya maana. Jambo ambalo litakuwa faida kubwa kwa CHELSEA FC hasa ikiwa tutafanya mashambulizi mfululizo kwenye goli la Everton.

Mfano: Everton ilicheza vizuri ikiwa ugenini kwa LEICESTER CITY lakini matokeo yalikuwa 2-2 mwisho wa mchezo. waliruhusu magoli 2.

Mfano wa 2. mechi ya Everton vs Arsenal..Everton walianza vizuri sana; na kufanikiwa kutawala mchezo. walitangulia kwa magoli 2-0..lakini ajabu ni kwamba zikiwa zimebaki dakika 10 tu magoli yote yakarudi.

goli la Girroud lilikuwa 'ushahidi' tosha wa jinsi ambavyo mabeki wa timu hii wanajisahau sana.

UDHAIFU WA ENEO LA KIUNGO...{EVERTON FC}

mtu mzima BARRY alikuwa mchezaji wa MAN CITY ..lakini JAVIER GARCIA alimweka benchi na hivyo akaletwa kwa mkopo EVERTON..sasa msimu huu wamemchukua moja kwa moja.

Hata hivyo udhaifu wa uchezaji wa BARRY ni kwamba ni mchezaji anayetumia zaidi nguvu kuliko akili. Ukiangalia CHELSEA kwenye kiungo kuna mafundi wengi ..hivyo naona 'harufu' ya kadi nyekundu au kadi nyingi za njano kwa wachezaji wengi wa Everton..

Ikumbukwe pia kwamba Steven Pienaar{Msauzi} aliumia kwenye mechi ya Arsenal kwa hiyo jumamosi hatocheza. Huenda wakamwazisha mtu mzima Neil Osman au Ros Barkley..
 
Asante mkuu Viol; nimeweka hivyo kwa makusudi..najua tupo ugenini..inapaswa kuwa kinyume hiyo picha.

Lakini kwa sababu tunautaka ubingwa lazima tuwe na uwezo wa kushinda nyumbani au ugenini, kushinda kwa mpira mzuri au hata mpira 'mbaya'....

tayari nimeshaanza 'uchambuzi' kuelekea hiyo mechi ya jumamosi..mimi nitakuwa hapa kila siku kuzungumzia hiyo mechi yetu vs Everton...ondoa hofu mkuu Viol..

mkuu hiyo picha umeweka chelsea vs everton,ila ikiwa Everton vs Chelsea hapo inakuwaje,hebu nipe ujuzi hao Everton wakiwa nyumbani sisi ugenini,ni kati za mechi nazoogopa
 
WAHESHIMIWA WOTE WA CHELSEA FC.

KWA HESHIMA 'MLIYONIPA' ACHENI TUANZE UCHAMBUZI WETU KUELEKEA MECHI YETU YA JUMAMOSI.

CHELSEA FC vs EVERTON...
SEHEMU YA KWANZA - UIMARA WA EVERTON FC.

Katika idadi ya mechi za chelsea vs everton...chelsea fc imeshinda mara nyingi zaidi.
hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni vijana hawa wa mjini Liverpool; na ambao ndo walioizaa Liverpool fc wamekuwa wagumu sana kufungika. Kama mjuavyo tumekuwa tukishinda kwa tofauti ndogo sana ya magoli kwenye mechi zetu vs Everton fc.

mfano: msimu ulopita walitunga kwao na sisi tukawafunga kwetu. Ikumbukwe kwamba katika msimu ulopita CHELSEA FC haikufungwa na timu yoyote ya top 5 isipokuwa Everton.

Everton hii ya Roberto Martinez ni tofauti sana na Everton ya d.Moyes..
Huyu kocha Martinez ni kocha mjanja, anajua jinsi ya kudhibiti timu kubwa tofauti sana na Moyes.

Mfano 2. r.Martinez alipokuwa kocha wa Wigan Athletic alichukua ubingwa wa kombe la FA. timu yake ilishuka daraja na kombe lao la FA.

Everton fC, inacheza mpira mzuri wa haraka na wanatumia sana mashambulizi ya pembeni. Kinachowasaidia sana ni wepesi wa wachezaji wao wa mbele hasa Kevin Mirallas na Steven Naismith..bila kusahau 'mwili nyumba' Romelu Lukaku, jamaa ana zaidi ya kilo 100. 'the big # 9.'

Everton Fc, wanacheza mfumo wa 4-3-3..kule mbele wanakuwa Lukaku,Naismith na Mirallas..
Katikati wanasimamaa; Gareth Barry, James Mc Cathy, na Steven Pienaar..

mabeki: Baines{kushoto}, Coleman{kulia}, kati Jagielka na Distin...
kipa wao uwezo wake unajulikana..Tim Howard..

Mechi ya jumamosi itakuwa na ushindani wa kutosha...

mkuu wangu kabla sijaendelea,je everton na liverpool ni watu wa jiji moja?
 
USUMBUFU WA BAINES # 3.{WA EVERTON}

beki huyu wa kushoto wa Everton ni miongoni mwa mabeki bora wa kushoto nchini Uingereza..

uzuri wake pia anaweza sana kupiga mipira ya adhabu na hata penati..{tusiwape nafasi katika hilo}

BAINES pia wanamtegemea sana kupandisha masahambulizi ya timu yao..krosi nyingi zinatoka kwa huyu bwana BAINES pia yule wa upande wa kulia anaitwa Coleman..

CHELSEA FC IFANYE NINI?..
tutahitaji kuwazuia hawa mabeki wa pembeni wasipande sana na kupiga krosi kwenye goli letu. Wakati huo huo tunahitaji kuendelea kuwashambulia. Sasa tutafanyeje majukumu yote hayo mawili kwa wakati mmoja?

Tutahitaji kuwapanga 'wazee wa kazi'..yaani, Blanislav `Ivanovic na Cesar Azpilicueta kwenye mabeki wa pembani..

Faida ya Ivanovic ni kwamba anapandisha timu ...pia jamaa hapendwi kufungwa, mzuri sana kwenye kona; anafunga sana..

'udhaifu' wake ni kwamba kukaba huwa anazidiwa ujanja; kwa sababu yeye 'namba yake asilia' ni beki wa kati 4 au 5. Na kwa Chelsea ni Cahill na Terry{watacheza hawa hawa hadi waumwe}

sasa kama IVANOVIC atazidiwa ujanja; itabidi Cesar Azpilicueta acheze kulia na Filipe Luis aingie acheze kushoto..nasema tena kama IVANOVIC atazidiwa..ingawa sidhani atazidiwa..
 
Ndiyo mkuu Viol;

Everton fc na Liverpool fc ni timu zinazotoka katika jiji la LIVERPOOL {kaskazini mwa Uingereza} hizi ni timu za mtaa mmoja ..
Kwa hapa Tanzania tungesema kama vile kule Tanga; kuna African Sports na Coastal Union..timu moja barabara ya 11 nyingine iko barabara ya 12.

Everton Fc ilikuwa timu ya kwanza kabisa kuanzishwa...baadaye ikaanzishwa Liverpool Fc..

mkuu wangu kabla sijaendelea,je everton na liverpool ni watu wa jiji moja?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom