Habari yako Mkuu
EMT, kitambo sana sijasoma nondo zako hata kwenye WC sikuoni, turudi kwenye hoja
Nakumbuka wakati wa Di Matteo, David Luiz alimaliza ule msimu vizurj sana na pamoja na mapungufu yake kwenye nafasi yake, washabiki wengi wa Chelsea walikua wanapenda jamaa arithi mikoba ya JT, nadhani na mimi nililileta hapa nikiwakilisha tu hayo maoni.
Kuna baadhi ya leadership skills ambazo Luiz anazo, wanasema jamaa ni very vocal kwenye dressing room na huwa anapresent a brother figure kwa mayoso na hata watu wa age yake na ukaribu wake na washabiki
Lakini akiwa uwanjani kwa kweli hawezi kulead by example, hawezi kupanga wenzake kwa sababu yeye mwenyewe hawezi kujipanga na sometimes yuko too emotional.
Naomba kukiri hapa kwamba nilikosea sana kudhani huyu bwana anaweza kuwa Captain wa team kama ya Chelsea