Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Hapo kwa Petrovic ni ngumu mkuu, ingekuwa hivyo makocha wangekuwa wanawafundisha, ndio maana sio kila mchezaji anaendana na style flan ya uchezaji,

Petrovic na Jorgensen hawalingani

Petrovic anaweza kuwa anamzidi Sanchez kwenye shot stopping
nadhani kwa lavia nahisi ni kwa sababu ya kuwa nje mda mrefu ,
 
Hapo kuna wachezaji sidhan ht kama waliwahi kucheza na kama wamecheza bc hawajafikisha ht mechi 5.
 
Kumbe Disasi kama Enzo walicheza wakiwa na hernia msimu uliopita na sasa kafanyiwa upasuaji na anaendelea kupona

 
Nawajulisha kwamba mchezaji Filip JΓΈrgensen amesafiri jioni ya leo kuelekea Marekani ili kusaini mkataba nchini Marekani ili kujiunga na kikosi cha Enzo Maresca kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya.

Ofa ni hadi Juni 2030 pamoja na chaguo hadi 2031

@fabrizioromano

 
Kufungwa siyo shida kubwa. Shida ni kuruhusu magoli 4
 
Uchambuzi wa kuwachezesha wachezajki nje ya nafasi zao hasa James na Gusto

Your browser is not able to display this video.
 
Kufungwa siyo shida kubwa. Shida ni kuruhusu magoli 4
Na mimi sioni shida kwa sababu tatizo linajulikana, uzembe uzembe
magoli mawili mabeki wanachelewa kurudi kuweka shape ya ulinzi na Enzo kalielezea hilo hivyo mimi sioni shida
Goli la tatu ni la Badisahile, akitupwa nje ya XI hatatutosa tena
Goli la nne Madueke alipoteza posseion kizembe na pia mabeki walikawia kurudi nyuma kuweka defensive shape.
Ttaizo la kufunga magoli jana tulikuw ana bahati mbaya, kosa kosa zilikuwa nyingi, kipa kaokoa. gonga nguzo nk
 
Tulikuwa na mikwaju 23 (mikwaju 10 iliyolenga goli),
iligonga nguzo za goli mara 2 dhidi ya Celtic, na bado tukaweza kufunga penalti moja pekee.
Umaliziaji wetu ulikuwa duni na ulinzi wetu ulikuwa mbaya zaidi.
 
Sijui watu wanalalamika nini? Ukiangalia timu inavyocheza unaona kuna kitu mwalimu anakifundisha sema tu wachezaji hawajafahamu namna ya kufanyia kazi mafunzo ya mwalimu.

Uzuri mwalimu ameshaona shida ipo kubwa sana wakiwa hawana mpira. Wanaacha magape. Hata wakipress wanapitika kirahis sana.
 
Mara nyingi hili gape kubwa linatokea kama pairing sio nzuri

Kuna tatizo sehemu ya nyuma, mabeki wote tulionao hawana uzoefu wa kusoma mashambulizi na kuwa kwenye njia yenye hatari kwa wakati sahihi kama alivyokuwa akifanya Silva. Chalobah alianza kujua kusoma moves za mashambulizi na sasa anauzwa. Tuna tatizo kubwa katika ulinzi

Sioni hata moja kati ya haya; Fofana, Tosin, Disasi, Badiashile, Colwill ambao wanaweza kubeba jukumu hilo zaidi ya Chalobah. Ikiwa anauzwa, basi beki mwenye uzoefu na wasifu huo au juu ya hapo anapaswa kununuliwa, vinginevyo, Maresca atahangaika sana na mabeki hawa tulionao.

Kwenye safu ya kiungo, sina tatizo, tunajitosheleza kwa options.

Hata kwa washambuliaji, sina shida sana hata tusiposajili striker. Nadhani msimu huu utakuwa mzuri kwa Sterling na atavutia msimu huu kwa sababu namuona anaendana sana na mfumo wa Marseca.
 
Chelsea fc ni bingwa wa epl msimu huu akipatikana beki mmoja kiongozi...mengine tutasema mwisho wa msimu.
 
Tumpe muda tusijudge kwa mechi mbili za pre season, huwezi kujua akafanyia kazi makosa ya beki wake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…