Kubaya huko ngoja waje wenyewe watakwambia Disas ni sawa kucheza RB😁😁Jana Disasi alikuwa busy kurudisha mipira kwa kipa au silva, very bussy, RB mbovu kuwahi kutokea kwenye jezi ya Chelsea. Akicheza CB anakuwa afadhali kidogo. Pochettino yeye anaona hayo ni sawa kabisa, tukimtukana kuna wapenzi wake hapa wanakuja kumtetea
Jana Cole Palmer alikasirishwa mara kwa mara na Axel Disasi kwa kutopeleka mipira mbele vya kutosha na alimzomea mara nyingi kuwa katika nafasi nzuri ya kutoa nafasi kwa washambuliaji.
Watu hawataki elewa hiloHuyu mbuzi kipindi anakuja interview yake ya kwanza hakusema huu upuuzi wa process, nakumbuka alisema ukiwa Chelsea ni kwa ajili ya kuchukua makombe. Leo anatuambia habari za process, huyu kenge ameisha feli.
Nilishawahi kusema mara nyingi Pochettino anaongea vibaya kwenye media kwa kuongea maneno yasiyoleta uwajibikaji kwa wachezaji ambao hawajitumi ndani yatimu. Anawatetea sana kupita kiasi na kuwafanya wachezaji wasiojituma kuendelea kuwa hivyo.Makocha hutengeneza au kuharibu timu.
Frank Lampard alisema wachezaji wa Chelsea (kabla ya Tuchel) hawakuwa tayari kushindania makombe. Ilikuwa ni "Managerial failure".
Miezi mitano baadaye, Thomas Tuchel alisema ataijenga timu ambayo kila mpinzani hatataka kukutana nayo. Aliwajen ga kisaikolojia wachezaji wale wale aliokuwa nao Frank Lampard na kuwafanya kuwa washindi wakuu wa Ligi ya Mabingwa. Ulaya. Ilikuwa ni "managerial success".
Anachofanya Pochettino sasa ni "Managerial Failure" kwa kuwaita kila siku vijana hawako tayari kushinndana, bado ni wachanga, hawana uzoefu kwenye ligi, hawawezi kucheza mara mbili kwa wiki katika ligi iliyosongamana, mradi huyu ni mchakato unaoweza kuchukua miaka mitatu hadi mitano. Too much negativity kwenye media na press conference zake. Hizi negativity zikiwa nyingi na za mara kwa mara kama propaganda ya siasa au vita inawafanya wachezaji wafanane na hizo propaganda zilizojaa negativity na hivyo kushindwa kucheza vizuri kama ambavyo wangeweza kucheza wakiwa chini ya kocha kama Tuchel
Tukimaliza nafas za juu huyu Pochi nene hatofukuzwa tupgwe tu ili afukuzwe.Ni vile tu Hatuna Kocha, tungekuwa na kocha mzuri top 4 tungemaliza ila kwa kiwa tunahuyi msimamiz wa mazoezi tunaishia hapa hapa 9-10.
Jerem Boga
Kocha mzuri siku zote huwa anapata ubora wa wachezaji wake haijalishi ameikuta team katika wakat ganiXabi Alonso alipochukua usukani Oktoba 5, 2022, Bayer Leverkusen walikuwa wa pili mkiani mwa Bundesliga na walikuwa na mwanzo wao mbaya zaidi wa msimu tangu 1979. Lakini Xabi aligeuza mambo na kuiongoza timu hiyo kumaliza katika nafasi ya sita kwenye Bundesliga.
Katika kampeni za 2023/24, Xabi Alonso alifanya uchawi wake tena, na kuiongoza Leverkusen kwa mechi 29 ya ajabu bila kushindwa na kufanikiwa kutwaa taji la Bundesliga kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Leverkusen iliposhinda kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Mainz Siku ya Mechi ya 23 ya Bundesliga, waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 33 za kustaajabisha katika mashindano yote. Jambo hili la ajabu sasa linawainua juu ya timu ya Bayern Munich ya Hansi Flick ya 2020 na 2021 katika kumbukumbu za historia. Bila shaka, mabingwa hao wa Bundesliga wamedhihirisha ubabe wao usio na mpinzani kwa kupata mbio ndefu zaidi bila kushindwa hata moja na timu ya Ujerumani katika mashindano yote.
View attachment 2963968