Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Huyu Galagher naye naanza kumuona ni mchezaji wa timu ndogo au average teams. Yan anataka timu ambazo hazina pressure kubwa acheze a relax ndio uraona kiwango chake. Angalia sasa hivi Barkley anavyokiwasha huko, muangalie RLC, muangalie huyu Galagher alipokuwa Crystal Palace

Hatimae mnaanza kukubali kuhusu Galagher
 
Niliwahi kusema ni mchezaji gani tuliyenae anaweza kupiga pass nyingi kwa usahihi aidha CM au AM. Huyu Gallagher tutamlaumu bure ila anahitaji kupandisha kiwango chake na akue zaidi kuacha mistakes ndogondogo kama hizi. Upigaji wa pass bado sio mzuri, kudrible bado. Ufanisi bado yuko chini.

Galagher ni mkimbiaji tu na kukaba ila kwenye kuwa na mali mguuni hamna mtu hapo
Yeye mpe mali atarudisha nyuma o apige pass pemben hata kama kuna mtu ashafungua
 
Brother THE BLUES ikicheza mechi za final huwa anacheza kwa kiwango kikubwa sana, ndio maana tuna makombe makubwa kabatini.

Labda kwa wakati huu tuna wachezaji wengi wapya na wadogo ambao hawana historia ya kubeba makombe na Chelsea.

Wenye historia ni Silva, Chilwell. Dah kwa kweli tunaweza kuangukia pua.
MMESAHAU LIVERKUKU ILIWAFUNGA FAINALI MBILI MFULULU?
 
Hatimae mnaanza kukubali kuhusu Galagher
Nilishasema muda mrefu. Hatuna namba 10 anayeweza kupiga pass za mwisho au namba 8 mwenye uwezo kuisukuma timu kupanda juu. Huyu Gallagher bado anakua anayo nafasi ya kujifunza na kufanya vizuri zaidi ya sasa akirudi kucheza position yake.
 
Yani unavyomuekea Mtu mkwala utadhani hukula 4 pale Anfield au huko nafasi ya 10.

Mtu ambaye yupo serious kama King Ngwaba hawezi kuja kwenye uzi wa Timu aliyoipiga 4 na iliyo na nafasi ya 10 kwasababu hakuna cha kujadili.
Nakuja kubeba ndoo mbele yako na hauta amini. Mnataka kuleta mazoea sasa.

Ila ndugu umepotea sana
 
Galagher ni mkimbiaji tu na kukaba ila kwenye kuwa na mali mguuni hamna mtu hapo
Yeye mpe mali atarudisha nyuma o apige pass pemben hata kama kuna mtu ashafungua
Yaani kuna mechi moja nilicheka akiwa katikati ya uwanja akaweka effort kubwa kupiga chenga nyingi ili tu amtafute Disasi kule nyuma wakati alikuwa na option nyingi tu za kuwapa wenzake wa karibu
 
Me nachojua
Chelsea itachukua EPL kabla ya arsenal 😅😅😅
Lkn kwa sasa huu uzi ungefungwa, au mnauziana kahawa kimyakimya
Make mnajadili Gallagher kila siku😅😅😅
 
Kikosi cha Jumapili, bado Nkunku hawezi kupenyeza kwenye kikosi cha Pochettino
Subs
  1. Sanchez
  2. Chalobah
  3. Silva
  4. Gilchrist
  5. Cesare Casadei
  6. Chukwuemeka
  7. Mudryk
  8. Nkunku
  9. Noni Madueke
1708669236213.png
 
Mauricio Pochettino alalamikia waamuzi wa mechi ya Chelsea na Liverpool mwezi uliopita. Awataka kesho wasirudie hivyo kama zawadi ya kumpa Klopp anapoaga Liverpool.

ana wasiwasi kuwa maafisa wa FA watakaochezesha mtanange wa Chelsea na Liverpool kesho watachukuliwa na upepo wa SENDOFF (yaani KUAGA) ya Jurgen Klopp baada ya baadhi ya maamuzi yaliyofanywa Anfield mwezi uliopita kuipendelea Liverpool.
Amesema labda kuna watu wanaotaka kusheherekea na Klopp anapoaga
"Nadhani tulipocheza dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Anfield nadhani maamuzi mengi sana...
hakuna uamuzi hata mmoja muhimu ulikuwa upande kwetu. Penalti mbili hazikutolewa. Duels, 50-50s, mara zote upendeleo ulitolewa kwa rangi nyingine (yaani nyekundu) - mara zote nyekundu. Nataka kuwa kutendewa kwa haki."
"Walikuwa bora kuliko sisi [Anfield], bila shaka. Lakini uamuzi wa kwanza baada ya dakika tano ulikuwa penalti ya wazi. Kipindi cha pili ilikuwa penalti, Nkunku. Sisi ni Chelsea na tunahitaji kushindana na zana sawa." [telegraph]

Kwa maoni yangu niko na Poche kwa 80%
Mkwara kabla ya mechi ni muhimu
Japo hatukucheza vizuri ila waamuzi walitoa maamuzi ya upendeleo kwa Liverpool na ikijirudia tena kesho itaharibu hiyo fainali

1708757836154.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom