Chelsea wana uamuzi mkubwa wa kufanya na kwa mujibu wa chanzo kimoja, kuna mashaka juu ya uwezo wa kiufundi wa Conor Gallagher kwa sasa.
Pochettino anataka apewe mkataba mpya lakini watoa uamuzi wanaona Gallagher akiuzwa italeta faida ghafi kubwa na pia kuondokana na uwezo wake mdogo wa kiufundi.
‘Kiwango chake cha kufanya kazi hakina shaka, uwezo wake wa kuchezea wapinzani na kurudisha mpira nyuma labda ndio nyenzo yake ya thamani zaidi,’ kilisema chanzo kimoja cha habari.
'Lakini daima kumekuwa na shaka juu ya upande wa kiufundi wa mchezo wake.'
Ambaye yuko kwenye vyanzo vingi vya habarim kwa sasa ni kiungo wa Everton Amadou Onana ambaye anaonekana ataziba pengo la Gallagher.
Chelsea tayari wameanza mazungumzo na Everton kumnunua Amadou Onana. The Blues wako tayari kulipa pesa nyingi ili kumpata kiungo huyo.
{Voetbalkrant}