CHELSEA FC ilichukua kombe la UCL 2012,
Nini siri ya mafanikio? Drogba alisaidia sana, yeye pamoja na wengine:
Lakini kuna watu 3 muhimu sana pale katikati ya uwanja waliosaidia sana:
Raul Meireles #16, jamaa anajua sana kutibua mbinu za wapinzani. mfano: Nusu fainali vs Barcelona CF.
Frank Lampard "super Frankie" huyu hajui kupiga chenga kama Hazard, wala hana mbio kama Willian, ila Frank anajua kutoa pasi zenye macho na kupiga mipira mirefu, kuipandisha timu mbele. pasi yake kwenye nusu fainali Camp Nou ilimfikia Ramires, na goli la Ramires likabadili mchezo kabisa.
John Obi Mikel mchezaji bora #2 wa Afrika.
Pia mchezaji bora #2 kwenye kombe la Dunia la Vijana mwaka 2005.(namba 1 alikuwa Messi.)
Sifa ya Mikel tangu aje Chelsea ni uwezo wake wa kunyang'anya maadui mipira, ni vigumu kumnyang'anya mpira Mikel, kucheza faulo za kitaalamu, tangu Mikel aje Chelsea 2007 amefundishwa na makocha wafuatao:
Jose Mourinho, Avram Grant, Scolari, Guus Hiddink, Carlo Ancelotti, AVB, Di Matteo, Rafa Benitez, Jose Mourinho: lakini hakuna hata kocha 1 amewahi kudharau kazi ya John Obi Mikel; ingawa mashabiki wengi "hawamkubali sana" lakini jamaa amekuwa muhimu sana miaka yote hiyo. Hata gemu ya fainali vs Bayern Munich alicheza dakika zote 120.
Man Utd wanayumba kwa sababu Michael Carrick amevurugika. Tafuteni mtu anayejua kucheza Defensive Midfielder vizuri mtavuna matunda; hao kina Mata, Pogba na wenzake hawataweza kuwanusuru; pia pigeni chini kocha;
NAOMBA KUWASILISHA:
CC; Ntuzu, Mentor, Rockcity native, Siziga, Nzi, Mbu, Dully jr, etc