Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

OllaChuga Oc lembu huwa mna kelele sana kwenye jukwaa letu kumbe team yenu ndio hii?Chelsea mnayoitambia?matak* yenu tumewanyanyasa kinyuma na mbele I think itakuwa mwisho wa kuja kupiga kelele kwenye jukwaa na Arsenal
Mmepiga maiti wala hamna haya kushangilia. Timu ina injuries 8 tena wa first team. Mmecheza na development team na bado mmeshindwa kufunga magoli mengi huku mkishangilia. April Mungu akijalia tutakuwa wote hapo Emirate
 
acha tupigweee tuuu maana huyu kocha ni *****, hivi kati ya makocha wote duniani huyu ndio tuliona ni kocha????
Hlo swali ndo la msingi , tafuta kocha mwenye CV , sio kocha et amepandisha timu daraja na anagombea top 4 unampa kisima 😁
 
Ninyi ninyi mliisifia timu hii hii ilipocheza na goigoi RB Salzburg. Tukawaambia timu hii bado. Middle zaidi ndio imepotea. Cheek hafai kabisa, hata kule mbele kushindwa kufunga ni kwa sababu ya hawa middle wetu.
 
Man city anatutoa carabao na Newcastle wanatufunga. Tushukuru tu kombe la Dunia tupumzike na baadhi ya wachezaji wapone. Team hatuna kiungo mkabaji wa maana, hatuna kiungo mshambuliaji, hatuna mshambuliaji wa kumaliza msimu hata na goli15.
Tatizo la msingi liko middle. Time will tell
 
Aterta kaleta nn arsenal , ? Hata msimu huu ataishia kuwa forerunner... Kama ndio mipango yenu endeleeni kumwamini kocha,
 
Tena cheek ndio hovyo
 
Kinacho tuuma ni kufungwa na Arsenal mbovu kwasabb ya majeruhi wengi akiwemo na kocha huyu chakinorisi wenu hatupeleki popote ana bahatisha mbinu.
Arsenal sio mbovu hata tungekuwa na wachezaji wetu wote na tukamfunga Arsenal, tuweke ushabiki pembeni bado Arsenal ya mwaka huu ni imara na yenye chemistry nzuri kuliko sisi, Wana ball control nzuri na utawaona kwenye pasi zile za haraka haraka wanavyothibiti mpira usiwatoke. Tushukuru Mungu tu WC inakuja kutuokoa ili tukirudi Desemba mwishoni tutakuwa na baadhi ya majeruhi kama akina Fofana, James na Kepa
 
Tena cheek ndio hovyo
Cheek akipata mpira lazima aweke miguuni halafu ajifanye mjanja wa mjini, yaani yeye kupata mpira na kutoa haraka hana hiyo tabia. Mpira wa siku hizi wa kasi ukizubaa na mpira watakunyang'anya tu
 
Kosa kubwa kumuondoa Tuchel yule bonge la kocha alitakiwa apewe muda aweke mambo sawa. Rahem kama hawezi kucheza mbele akae bench sio kumpa wing back. katika lazima wacheza watatu hii 4222 haifai
Kocha alishakiri kosa na tangu hapo Sterling amekuwa akicheza nafasi yake. Jana kocha aliweka 4-2-3-1 na tatizo kubwa waliotuangusha jana ni midle Jo na Cheek hawakuweza kuthibiti mpira pale katikati. Hawako cretive pia kushirikiana na CAM kutengeneza nafasi kwa washambuliaji. Tusiwachukulie wachezaji wote ni wabovu. Auba ni mzuri sana wa kutupa angalau goli 15-20 kwa msimu ila asipohudumiwa atawezaje?
 
Hakuna mtu aliyesema TT ni mbovu, zama zake zimeisha sasa tupo zama za GP. Timu bado inajengwa tusisahau hili. Hao wachezaji wasiofaa wataondolewa ila sio kwa mkupuo mmoja na pia hao wachezaji wanaofaa watasajiliwa ila sio kwa mkupuo mmoja. Tukumbuke pia usajili hata uwe makini sana ni gambling mwisho wa siku. Tulimchukua Silva kwa matarajio ya kumjaribu msimu mmoja tu lakiniu sasa ni msimu wake wa 3 nafikiri. Tulimsajili Havertz kwa mbwembwe nyingi na nyoyo za mashabiki wakaridhika kabisa. Yuko wapi hadi sasa anapeta uwanjani tu bila impact ya maana. Timu imara inajwngwa kwa mikakati mizuri. Boehly ameonyesha anayo mikakati
 
Boehly hapo alizingua sana
Ilitakiwa Boehly angefanya mambo mawili
  1. Angemfukuza TT kabla ya usajili ili kocha mpya apendekeza wachezaji wake AU
  2. Angemuacha TT ili ajenge timu kwa wachezaji aliowataka wanaoendana na falsafa yake kama Arsenal walivyofanya kwa MA hata alipoboronga walimuacha akamtoa kafara AUBA aliyekuwa anaharibu Dressing room. Naye TT angeachwa angemtoa Jorginho kafara aliyekuwa anamharibia TT
 
Huu usajili haukuwa wa mapepe, ulikuwa ni usajili wa TT. Kosa la Boehly ni kumfukuza TT huku wachezaji waliosajiliwa ni wa kwake
 
Mmepiga maiti wala hamna haya kushangilia. Timu ina injuries 8 tena wa first team. Mmecheza na development team na bado mmeshindwa kufunga magoli mengi huku mkishangilia. April Mungu akijalia tutakuwa wote hapo Emirate
Na zile nne za mwaka jana msimu uliopita injury walikuwa wangapi?
 
Wakuu, hivi huyu kocha nyie wenzangu umnakwelewa kweli? kuna timu mule ya walau kuwa top four mwisho wa msimu ?

Au na sisi tunaanza kujenga timu upya, maana sikuona lolote jana na tulitakiwa tupate adhabu zaidi ya hiyo.
 
Pierre-Emerick Aubameyang had just four touches in the first half against Arsenal, at least 15 fewer than any other outfield player.

He also received more yellow cards (1) than he had shots (0). [emoji102]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…