Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Hakuna wachezaji wa kuwachezesha, Werner, Lukaku wakienda pale Man city watafunga sana.

Inafikirisha sana Lukaku, Werner, Kai wakienda timu za taifa wanafunga kila mechi, wakirudi BLUES ukame wa magoli.

The BLUES hatuna washambuliaji creative wanaowazunguka Lukaku & Werner. Hawa Ziyech, Mount, Barkely, Cheek, Odoi wanalazimisha kucheza vitu ambavyo havipo.

Werner angewakuta hazard, Pedro, Willan, Fabrigas angefunga sana.

Tumeenda kumsajili Lukaku, changamoto ya kutokufunga mabao ipo pale pale

Ishu ilikuwa sio kumsajili Lukaku aje kutatua changamoto ya kufunga magoli, bali ilikuwa kuziba mapengo ya hazard, willan, Pedro na fab.

Wakati CONTE anamtaka Lukaku, Hazard, fab, willan, Pedro walikuwepo, angetua wakati ule lingekuwa balaa zito.

TT pale mbele apange mifumo yote anavyojua, afundishe style zote za ushambuliaji pale mbele, hawa Werner na Lukaku watastruggle sana kufunga magoli.

Solution ni kusajili creative attacking mildfliders and wings. Magap ya Hazard, Fab, Willan na Pedro yazibwe.

Na Pulisic kula mshahara bure inatosha.
Msimu uliopita tuliongoza kwa kutengeneza nafasi zinazopotea, wachezaji ni wale wali akina Jo, Kova, Kante, Mount, Pulisic, Werner, Havertz
Ni vyema badala ya kusema hatuna wachezaji tujiulize KULIKONI ujio wa Lukaku umewafanya wachezaji kuwa wachoyo au ni nini kimetokea?
 
Mimi naona kama washambuliaji wengi wa Chelsea wana ubinafisi wanataka wafunge wao badala ya kuwapasia Lukaku na Wener.

Na hii inatokana na kutowaheshimu hao mastriker kama ambavyo Drogba alikuwa akiheshimiwa na wachezaji wenzake.

Costa naye aliheshimiwa kwa kuwa alikuwa fighter na hamuonei mtu aibu hivyo automatically wachezaji wenzie wakamheshimu na kuwa wanampatia mipira kila mara.

Wener na Lukaku wakitaka wawe goals machine pale Chelsea inabidi wafanye kitu cha ziada ili wachezaji wenzao wawaheshimu na kuwa wanawalisha mipira kila mara. Vinginevyo hawa strikers wengine wanawachukulia kawaida tu hasa ukizingatia wamewakuta tayari wakiwapo klabuni.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Advantage ya akina Costa na Drogba, hakukuwa na ubinafsi kama huu wa leo. na pia tulikuwa na caliber ya akina Fabregas, Hazard nk. Leo ni Mount tu anajitahidi na Werner pia kwenye assists.

Ukitaka kujua ubinafsi wa wachezaji wa Chelsea. Chelsea ndio inaongoza EPL kwa wachezaji wengi kufunga magoli. Hadi sasa wachezaji 14 tofauti wameshafunga angalau goli moja kwenye michuano yote tangu msimu uanze
 
Mbona CITY anayetokea benchi ana caliber/quality ya kuanza 1st eleven hapo hapo city na timu yoyote duniani?

Sio kwa sababu mchezaji anatoka benchi ndio tujaze matakataka benchi wanatupotezea muda kufikia mafaniko.

Wakati ule anatoka Malouda anaingia Ramires au Solomon Kalou, anatoka Drogba anaingia Anelka AKA Mapungo, anatoka Essen anaingia Mikel Obi. Wote quality ya hali juu.

Tuachaneni kuwapamba wachezaji matakataka, sasa hivi hatuna SUB za maana bali wastage of time
Mkuu RLC utampenda tu mpe msimu huu tu apate dakika nzuri hata kama ni za sub. Mchezaji ambaye simuamini nadhani kwa sababu ya ulevi ni Barkley, mchjezaji mzuri sana ila anaua career yake kwa sababu ya kutokuwa na nindhamu ya mpira.

Alonso alipotea wakati wa Sarri na Lampard hadi mashabiki wakawa wanamtukana kila leo. Amekuja TT jamaa kaibuka na quality ya uchezaji kila shabiki anashangaa. Hata Christensen, Rudiger alishaanza kupotea wakati wa Lampard ila TT kaja kafufua vipaji na ubora

Mifumo ya makocha saa nyingine inaua vipaji na ubora wa mchezaji
Kwa mfumo wa TT Cheek atarudi kwewnye form mpaka utampenda

Kwa issue ya Man City ni kocha ndie anawafanya hivyo, ngoja PEP aondoke, wachezaji hao hao utawaona watakapogeuka ubora wao kuwa mbovu

Kocha anayo influence kubwa kwenye kuinua viwango vya wachezaji
 
Kuna kipindi cha The Headline Makers" inaendelea sasa hivi Supersport wanamjadili TT na wanaweka recorded interview kuhusu Ugenius wa TT na Lukaku kutofunga na mambo mengineyo.

Kuhusu yeye kuitwa Super Genius TT anasema yeye anachofanya ni kutoa solution ya ushindi kwa wachezaji wenyewe
Mbinu zake zinabadilika nchi kwa nchi, ligi kwa ligi, timu kwa timu na pia mwaka kwa mwaka kwa sababu wachezaji wanaondoka na wanakuja wapya.

Kuhusu Lukaku kutofunga anasema wachezaji bado wanafahamiana, saa nyingine inachukua muda na pia kasema Lukaku sio mbinafsi na hiyo imejionyesha kwenye ushirikiano anaoutoa kwa washambuliaji wenzake na pia kwenye dressing room.

Anasema Lukaku kupewa huduma ya mipira ni suala la connections
Kuna wachezaji wameshamtambua Lukaku na wengine bado wanajifunza ni suala la muda tu

Pundits wanaoendesha mjadala wakatoa comment ambayo nimeipenda

TT ni supper genius, kaja EPL ligi ngumu akaleta mabadiliko ya haraka kuliko ilivyotegemewa na wengi na hasa kubeba UCL
Pia wakasema angalia Chelsea haichezi kwenye kiwango chake na iko top of the League wakati imeshacheza mechi ngumu zaidi ya contenders wenzake.

Je form ya Chelsea ikirudi mahali pake itakuwaje?

Mambo mazuri yanakuja The Blues msivunjike moyo
 
Amanda wa Newcastle kaanza, anamtaka Werner kwa paundi mil50
 
Werner hatari anarudi blues wote tukae mikao ya juicy na popcorn ,huyu kiumbe hatari yake inarudi,nikikumbuka TT alipoulizwa kwanini Werner afungi alijibu kijana ameanza kufunga akiwa mdogo ,ameishi katika ufungaji ,muda huo utarudi tu ,kila ishara inaonyesha mjuba anarudia hatari yake .
 
Sasa Lukaku itakuwaje?

Werner akifunga magoli mengi Lukaku atajeuka kuwa mpikaji wake.

Kwa sababu the BLUES hatuna mchezaji mwenye uwezo wa kuwapikia magoli wote wawili Werner na Lukaku.

Lazima mmoja kati ya Werner au Lukaku atamtegemea mwenzake kumpikia magoli

Na juzi Lukaku amekataa hiyo role, yeye anataka kucheza ndani ya box alitazame goal mbele atoe pass arudishiwe pass afunge goal.

Na akianza Striker mmoja mfano WERNER kufunga ni shughuli wanaomzunguka kushoto, kulia na nyuma hawana msaada kwake.

Akianza Lukaku wanaomzunguka kushoto, kulia hawana msaada kwake labda asubirie mipira kutoka kwa James, Azipi na Kovacic.

Kwa hali ilivyo sasa hivi pale mbele lazima wacheze wote kwa pamoja Werner + Lukaku.
I trust in Mason Mount
 
Habari Mchanganyiko
  • Timu ya Wanawake wa Tanzania yatwaa COSAFA Women Cup. Nimeangalia mechi aisee hao wadada wanakiputa ile mbaya na yule mfungaji wa goli Lunyamila ni hatari. Hii timu inaweza hata kuchukua kombe la Afrika
  • Timu ya wanawake wa Chelsea yaifunga Juventus 2-1 kwenye mashindano ya UEFA ya wanawake hapo jana. Nimeangalia mechi nzima, wamecheza vizuri sana. Surely they can win UEFA this round
 
Denmark mpaka sasa hawajafungwa goli kwenye mashindani ya European Qualifier kwa maneno mengine wana clean sheet 5 na wameshinda zote. Je Christansen ana mkono hapo.

Bosi wa Brentford amekiri tayari kuwa Christensen ni Complete Package

Brentford manager Thomas Frank believes Chelsea defender Andreas Christensen is ‘almost the complete package’ and ‘one of the best defenders in the world’.
 
Drogba alikuwa akiifanyia ugaidi Arsenal wakati wa kipindi chake
Katika mechi 16 alizocheza dhidi ya The Gunner kawafunga goli 11

Matches = 16
Goals = 11
GettyImages-96480460.jpg
 
Mkataba wa PAUL POGBA unakaribia kuisha kule kwa manyumbu.

Nadhani January tufanye juhudi za kumsajili. Why not?

Tunahitaji mchezaji aina ya Pogba, atupe ufundi wake pale mbele

------------ WERNER ------- LUKAKU ----------------

------------------------ POGBA ------------------------------

ALONSO --- JOGINHO --- KANTE --- JAMES

------RUDGER ---- CHRISTENSEN -- AZIPI ----View attachment 1973911
Hii takataka ya nini, yata benchi la chelsea hapati namba.
 
Mkataba wa PAUL POGBA unakaribia kuisha kule kwa manyumbu.

Nadhani January tufanye juhudi za kumsajili. Why not?

Tunahitaji mchezaji aina ya Pogba, atupe ufundi wake pale mbele

------------ WERNER ------- LUKAKU ----------------

------------------------ POGBA ------------------------------

ALONSO --- JOGINHO --- KANTE --- JAMES

------RUDGER ---- CHRISTENSEN -- AZIPI ----View attachment 1973911
Hii type ya wachezaji itasumbua kwenye dressing room
 
Mkataba wa PAUL POGBA unakaribia kuisha kule kwa manyumbu.

Nadhani January tufanye juhudi za kumsajili. Why not?

Tunahitaji mchezaji aina ya Pogba, atupe ufundi wake pale mbele

------------ WERNER ------- LUKAKU ----------------

------------------------ POGBA ------------------------------

ALONSO --- JOGINHO --- KANTE --- JAMES

------RUDGER ---- CHRISTENSEN -- AZIPI ----View attachment 1973911
Pogba mzuri, tatizo lake hawezi kuendana na baadhi ya makocha, kwenye assist na kufunga ni mzuri
 
Line up ya Chelsea against Brentford

3-4-2-1

Werner ------- Havertz ---------Mount

Chilwell ------ Kovacic -----Jorginho ---- Azpilicueta

Malang Sarr------ Christensen ------Chalobah

Mendy
 
Line up ya Chelsea against Brentford

3-4-2-1

Werner ------- Havertz ---------Mount

Chilwell ------ Kovacic -----Jorginho ---- Azpilicueta

Malang Sarr------ Christensen ------Chalobah

Mendy
Lukaku karudi ameonekana leo mazoezi
 
Matukio ya Antony Taylor dhidi ya Chelsea na ni kwanini hafai kuchezesha mechi za Chelsea

  1. 2014 alimpa Fabregas kadi ya njano kwa kudive eneo la penalti wakati ni kweli Fab alifanyiwa rafu na kuinyima Chelsea penalti ya wazi- Baadaye aliomba msamaha ila haikuwa na msaada kwa Chelsea
  2. December 2019, kipa wa Spurs Gazzaniga alimfanyia uninja Alonso lakini Taylor alipotezea hiyo rafu ilitakiwa iwe penalti
  3. May 2017 Sanchez aliunawa mpira kabla ya kufunga na Taylor akaminya na Arsenal wakabeba FA
  4. February 2020 Maguire alimpiga mapumbu Batsuayi, Taylor akapotezea
  5. August 2020, Kovacic alifanyiwa rafu na Xhaka lakini Taylor alimpa kadi ya njano ya pili Kovacic na kumtoa nje kwa red card
  6. 28 Aug 2021, Taylor alimpa Reece James kadi nyekundu kwa kushika mpira
  7. Tarehe 16 October 2021 sijui Taylor atatulimia wapi???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom