Ahsante mkuu. Tuko pamojaNimefurahi kukuona tena jukwaani. Karibu
Bado innocent independent tunamsubiria tangu mwezi wa 11 hajaonekana hapa.
Kwan haiwezekanKubali tu kuwa hapo umechemsha mkuu, timu ambayo ndio kwanza iko assembled ichalenge ubingwa?
Kocha wa makipa hilario inabidi aondoke na yeye ni jipu, kepa tulikuwa naye wakati wa sarri na alikuwa fresh ila kepa wa lampard alikuwa yuko poor, na mendy nae ukiangalia kiwango chake kilikuw kishaanza kushuka,Wachezaji watakaofaidika na ujio wa kocha mpya na watakaadhirika pia
Winners: Timo Werner, Kai Havertz, Toni Rudiger and KEPA
Kocha mpya anatoka ujerumani, anaongea kijerumani, tutegemee hao wajerumani wakipewa muda wa kutosha kwenye play minutes labda watuangushe wenyewe. Ktk mechi 15 Werner kafunga goli moja tu tena kwenye FA na kitimu cha mtaani, Havertz yeye kaanza vibaya hadi mechi zingine akawa anawekwa benchi. Rudiger yeye baada ya kurudi majeruhi amekuwa akila benchi na saa nyingine kukosa benchi kabisa
Mchezaji mwingine atakaefaidi ni KEPA, Kepa alifanya vizuri kwenye utawala wa Sarri, ghafla akaanza kufanya vibaya kwenye utawala wa Lampard. Wachambuzi wengi wa soka wadai ubovu wa Kepa unamizizi na ubovu wa Kante, Kovacic, Pulisic, Werner, Havertz, Jorginho
Haiwezekani 90% ya darasa ikafeli halafu tuseme ni wanafunzi vilaza. kule chuo kikuu enzi zangu, lecturer akifelisha darasa zima au kwa asilimia kubwa huwa yeye ndie anaadhibiwa ikiwa ni pamoja na kufukuzwa. Sasa Lampard kushusha viwangi vya wachezaji wote hao maana yake na KEPA yumo na hivyo Lampard na benchi lake la ufundi ndio walikuwa wabovu. Sasa Tuchel kaja tutegemee KEPA atarudi kwenye form yake iliyosababisha zaidi ya mil 70 zilipwe kwa jina lake. Kwa hiyo tutegemee KEPA naye akipewa mechi kubwa kubwa na sio zile zile za FA na Karabao cup tu
Loosers: Mount, Tammy Abraham and Giroud
Mount ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji sana kwenye kiungo na ni mchezaji anayeweza kufit takriban kila mfumo. Lampard alimuamini sana kiasi cha kufikia hatua ya kumchosha kwa kumchezesha kila mechi. Tutegemee naye kuingizwa kwenye rotation, sub na saa nyingine kupumzishwa kabisa kwenye mechi zingine. Siku zake za kufanywa mtoto wa mfalme zimefikia ukomo na sasa itabidi kisaikolojia ajiandae kuzoeza benchi na saa nyingi kulala bwenini.
Tammy alishapunguziwa mizigo na FL. Sio kwamba Tuchel atamuacha kabisa ila tutaona akimpunguzia mizigo zaidi na kijitahidi kuinua viwango vya wajerumani wenzake.
Pamoja na kufunga magoli manne kwenye mechi na Sevila, OG umri wake wa miaka 34 utamfanya Tuchell awekeze zaidi kwa vijana wadogop akina Werner na Tammy Abraham. Ningekuwa mimi Giroud ningewahi tu Juve kwa wazee wenzangu
Ushauri
Ili Tuchel afanikiwe na aweze kuwatumia vizuri akina Werner, Kai na hao wengine ni lazima atumie hizi formation mbili
4-1-4-1 au 4-2-3-1
Ila Petr Cech abaki kwa hali yeyote ileBenchi la Lampard liondolewe lote limefeli, Tuchel ashuke na benchi lake.
Daah ulivyoahadithia mkuu kama Niko kwenye kioo, niliiona hii gameBasi bwana mwaka 2009 chelsea ilikutana na Barcelona kwenye nusu fainali. First leg ilipigwa Camp Nou na kutoka bila bila hii second leg ikaenda kupigwa darajani.
Refa wa hii game alikua Ovrebo.
Game ikaanza chelsea wakapata chuma cha kwanza. Mambo yakaenda vizuri kisha hali ya hewa ikaanza kubadilika.
Alves akamkata Malouda ndani ya box. Ovrebo akasema kosa limetokea nje ya box.
Wakina Drogba wakamuwakia ila yule bwana akaweka pamba sikioni akaendelea na maisha mengine.
Replays zikaonyedha ni kweli kosa limetokea nje ya box.
Game ikaendelea.
Drogba akapata chansi ya kwenda kuscore akawa yupo mbele ya Abidal, Abidal amekazana kumtoa Drogba kwenye reli ila Drogba kakaza huko Valdes anawaza shuti litakalotoka hapo. Kufika kwenye boksi Abidal akaona isiwe kesi akamlamba rafu janja Drogba, Drogba chini.
Ovrebo akageuka zake huyooooo.
Drogba kawaka bwana Ovrebo katia pamba masikioni hata hajali.
Replay inaonyesha Drogba alianza kuchezewa rafu tangu nje ya box, body language inamuonyesha akiwa anajiandaa kupiga shuti kabla hajalazwa chini.
Kisha Chelsea ikiwa inaendelea kushambulia wapo langoni kwa Barca Anelka anapiga shuti linazuiwa na mkono wa Baba Shakira.
Anelka hata hajisumbui kumuonyesha refa kwakua ni kosa lililoonwa na kila mtu lakini Ovrebo wala hata hakujigusa akaamuru mchezo uendelee.
Kisha Abidal akagewa red kwa kumchezea rafu Anelka, marudio yanaonyesha Anelka alijikwaa mwenyewe, hata hivyo haina maana kwakua Abidal alitakiwa awe ametoka tangu muda hata hivyo.
Game ikiwa inaelekea ukingoni Iniesta akatia chuma kusawazisha.
Ikawa 1 kwa 1. Wastani kwa hapo ni Barca anasonga mbele.
Chelsea ikapata kona. Ikapigwa kona mchezaji wa chelsea akaachia shuti, Samuel Etoo akalikinga lile shuti likamgonga mkononi. Pembeni yake Etoo alikuepo Ovrebo.
Ila akawa kama hajaona kitu akajigeuza zake na kuondoka. Ballack akaona huu ni upuuzi akamkimbilia Ovrebo na kumkaripia na kuomba na kila kitu ila Ovrebo hajali, muda huo mpira unaendelea.
Game ikaisha. Chelsea ikatolewa.
Ovrebo alikua ameikatalia Chelsea penati nne za wazi.
Pale pale Drogba akamkimbilia Ovrebo, maafisa wakafika kumzuia ila mashabiki wa chelsea wakamuahidi kifo Ovrebo palepale uwanjani.
Drogba akaigeukia kamera akasema "Are you watching this? Its a disgrace. Its a fvcking disgrace"
Maafisa wakamsindikiza nje Ovrebo kwa kuhofia kuuawa usiku huo huo wakambadilishia hoteli na kumtoa nje ya Uingereza kisirisiri.
Akiwa anahojiwa na jarida la Marca, Ovrebo akasema "Chelsea imeanzishwa 2003, ni timu ndogo ilikua inapambana na timu kubwa. Hata wangepata penati 100 bado ningekataa tu"
Anyway, natania. Alisema "Makocha na wachezaji hua na siku ya hovyo na marefa pia hua na siku hatupo sawa. Siwezi kujivunia kilichotokea siku ile"
Baada ya pale Ovrebo alikatwa kwenye orodha ya marefa wa waliotakiwa kwenye tournaments. Baadaye akaja kutangaza amestaafu.
Kama umegundua vizuri jamaa kaanza na wakongwe kutokana na Aina ya game ya yenyeweMount kaanza benchi jamani.
tulia game iishe ndo ulaumuTuchel kaanza kutuzingua mapema mno
Naona anabeep ligii... anafikiri epl kuna kina caen na niceTuchel kaanza kutuzingua mapema mno
Akiwa anahojiwa na jarida la Marca, Ovrebo akasema "Chelsea imeanzishwa 2003, ni timu ndogo ilikua inapambana na timu kubwa. Hata wangepata penati 100 bado ningekataa tu"
Mount kaanza benchi jamani.
Mkuu yye ndie walimuMount amecheza mechi zote EPL, FA, CARABAO, UEFA kiwango chake kiko juu kwa sasa, labda useme uchovu ametumika sana.
Kali mnooo