Point, pamoja na kumchukua miaka minne Klopp alikuja akiwa na miaka mingi ya uzoefu kama kocha wakati Lampard ndio mwaka wake wa pili kwenye football na wa kwanza kwenye big league. Waliokuwa wanamsodoa Klopp akiwemo King Ngwaba leo hii wamekuwa wapole kama njiwa
Mimi sikumkosoa Klopp kwasababu ya uwezo wake kwani alishaprove uwezo wake since yupo Dortmund.
Mimi na wengine kama mimi tulimkosoa Klopp kwasababu ya Falsafa zake za usajili pale alipokuja na kusema "Anashangaa kuona Manchester anasajili wachezaji wa bei ghali" yeye akasema hatosajili wachezaji wa bei ghali bali ataboresha alionao na wale atakaonunua kwa bei ndogo.
Hapo ndiyo Vitaa vikaanza kwani kwa Magarasa aliyokuwa nayo hakukuwa na mbinu ya kuboreka.
Alipoanza kushusha Kina VVD, SALAH, OX tu tulinyamaza kwasababu ametupa tunachotaka, kwahiyo kumkosoa haukua ujinga na kunyamaza sasahivi si ujinga.
Ujinga ni kukosoa pale ambapo hapana cha kukosoa.
Na sidhani kuwa sasahivi simkosoi Klopp kama unavyowaaminisha Watu! Labda uwe huji kwenye Uzi wetu.
Issue inakuja kwa Lampard!
- Kisingizio cha kuwa hana Wachezaji bora hakipo tena.
- Kisingizio cha kuwa Wachezaji wake hawana experience hakipo tena.
- Kisingizio cha kuwa kufungiwa kusajili hakipo tena.
Kwahiyo kwasasahivi wakati Timu inafanya vizuri kumlalamikia ni Ujinga! Ila kumaliza Msimu bila ya Kombe (EPL au UCL) na sio mickey mouse cup basi washabiki wanayo haki ya kumlalamikia na kukosoa uwezo wake.
• Klopp hakupata bahati kama Lampard kwani Matajiri wa Liverpool hawakumpa pesa ya kusajili wachezaji wengi kwa pamoja bali alipewa kidogokidogo ndiyomana inamchukua miaka 4 kupata mafanikio.
Ukiangalia kina MANE, SALAH, VVD, ALISSON wote hao wamekuja kwa madirisha tofauti.
But Lampard kupata bahati ya kupewa CHILWELL, MENDY, KAI, ZIYECK, WERNER, SILVA ndani ya Msimu mmoja ambao wote hao ni Wazoefu wa Bara Ulaya unataka nayeye asubiriwe atimize miaka MINNE kama Klopp?
Kaka Lampard ni lazima kudiliver msimu huu vinginevyo Washabiki hawatomuelewa.