Ukikutana na plastic kutoka chelsea hatasita kukuambia hajawahi kutokea mchezaji hatari kama Drogba na EPL nzima hajawahi kuwepo. Sasa twende polepole;
Henry alishinda kombe la UCL 2009 alichangia magoli 8, 6 alifunga katika hatua ya mtoano. Drogba alipata UCL 2012 akachangia magoli 8, 4 tu ndiyo alifunga katika hatua ya mtoano.
Henry ana jumla ya magoli 58 ya kuamua ushindi kwenye ligi ya EPL, Drogba ana magoli 31.
Pia Henry amechagia magoli 64 dhidi ya timu za Top 4 EPL + Hatua ya mtoano kwenye UCL, wakati Drogba ana 41.
Tangu Drogba afike Chelsea mpaka anaondoka ana jumla ya magoli 20 dhidi ya top 6 wakati Henry ana magoli 24 dhidi ya Liva, Man U na Chelsea pekee. Hapo hujamhesabia waliobaki.
Henry amefunga magoli 20+ mara nne katika EPL wakati Drogba amefunga magoli 15+ mara mbili tu.
Drogba amejinyakulia kiatu cha dhahabu pale EPL mara mbili. Henry amechukua kiatu cha dhahabu mara NNE.
Henry amepata tuzo ya Player of the Season mara 2 na katika tuzo za Ballon D'Or amefika kwenye tatu bora mara mbili. Drogba hapa hana chake.
Kimataifa Henry ameshinda kombe la dunia 1998 na kua France top scorer na 2006 akatoboa mpaka fainali. Bwana Drogba hapa hana kitu pia aliishia hatua ya mtoano mara tatu zote alizonusa kombe la dunia.
Kuna plastic litakuja kuandika komedi hapa.