Baada ya uchovu wa majukumu ya leo ngoja niwape stori flani kuelekea mechi yetu na Bayern.
Mwaka 2010 nikiwa arusha maeneo ya mnara wa mwenge, maduka flani upande wa chini yanayotazamana na makaburi, njia ya kuelekea polisi.
Siku hiyo ilikuwa jumamosi mida ya saa 1 asubuhi. Mimi na baba yangu mdogo tulikuwa tumesimama nje ya duka lake tunapiga stori.
Kwa kipindi hicho ilikuwa kila siku ya jumamosi wamiliki wa mbwa majumbani walikuwa wanapeleka mbwa wao kule polisi kuoshwa na huduma nyingine.
Kwahiyo mida hiyo mbwa wengi walikuwa wanapitishwa na vijana kwenda huko polisi, tukasikia sauti kwa mbali jamaa anasema "FUKUZENI HUYO MBWA KOKO HAPO TUPITE, TUSIJE TUKAMUUA BURE", jamaa walikuwa ameshika minyororo ya mbwa wawili wakubwa sana kama ndama wanatisha, yanataka kukata mnyororo kwa hasira.
Kweli pembeni yetu alikuwa amelala mbwa wa pale mtaani hana makazi ya kudumu huwa anazungukaga tuu maeneo hayo tulishamzoea, mara alale chini ya magari parking, vibarazani.
Baba mdogo akamjibu wale jamaa "AMUENI MTAKALOFANYA HUYU MBWA ATAJAZA MWENYEWE"
Yule jamaa akajibu sawa ngoja mzee tumuonyeshe rangi zote, bwana akaachia mnyororo wa limbwa limoja likawa linakuja kwa kasi kumfuata huyu mbwa wetu. Ikabidi tukimbie pembeni tuone movie.
Yule mbwa wa mtaani alivyoona lile limbwa linakuja kwa kasi akasimama akamcheki, akanguruma kwa hasira, aisee huyu mbwa wa mtaani alimpokea kwa kumrukia shingoni, wakaamguka chini, alimvuruga kwenye mavumbi tukasikia mlio wa maumivu.
Lile limbwa la jamaa likatoka baruti likarudi kwa wale jamaa. Nikasikia wale jamaa wanasema eeh eeh eeh hatareee huyo mbwa ni noma, jamaa wakavuka upande wa pili wanaenda huku wanajeuka nyuma hawaamini kilichotokea.
Kilichofuata ni pongezi kwa yule mbwa wetu wa mtaani, tunamdharau kumbe vita anaviweza. Nakumbuka kuna mzee alipita akasema leo naenda moshi naombeni mnikamatie huyu mbwa nimpeleke moshi nikamfuge hakiamungu mwizi hatakanyaga kwangu. Hahahaha
Mwache BAYERN aje kibabe tutakachomuonyesha rangi zote stanford, tutamchanachana vipande atatoka na kilio cha uchungu.