Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Sasa hivi timu yangu chelsea inanipa matumaini ila bado mapema tuwe na subira paka angalau january ndotutakua nawakika kama Chelsea imekua salama na lampard
 

Kabisa kaka. Naamini Kante alipo najisikia raha japo majeruhi. Na inawapa motishs majeruhi wote wanakuwa na furaha wanapoona timu inaperform vizuri. #CheekRudgerKante# soon they will be back on the field[emoji1545]
 

Anacheka kila anapoona hawa vijana wanachofanya uwanjani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Pia Lampand afanye rotation ili kila mchezaji ajione mwenye thamani kuichezea chelsea. Nimependa anavyofanya kwa sasa. Ili afanikiwe hasiwakumbatie waingereza kwenye stsrting XI. Hongera chama langu kwa ushindi next Barnley.
 
Mkuu sokoni lazima tuingie hasa beki mmoja, kiungo mmoja pamoja na kwenye attacking lazima tufanyie kazi hizi nafasi.
 
Pia Lampand afanye rotation ili kila mchezaji ajione mwenye thamani kuichezea chelsea. Nimependa anavyofanya kwa sasa. Ili afanikiwe hasiwakumbatie waingereza kwenye stsrting XI. Hongera chama langu kwa ushindi next Barnley.
Yeah rotation ni muhimu kuongeza competence kwa kila mchezaji na pia itasaidia kupunguza specialization. Leo hii Jorginho asipikuwepo tutaanza kuwaza nafasi yake atachukua nani
 
Kwa ufupi tunacheza na team B, Team A iko majeruhi
 
Mimi mtu wa Liver ila nimepitia tu huku kusalimia. Unajuwa Ajax ni wazuri sana tu ila jana nawapa sifa zote Chelsea waliifanya Ajax kuonekana team ya kawaida sana tu. Chelsea walienda kama wababe na team kubwa walicheza kwa kujiamini sana na 3 5 2 ni mfumo unawafit sana Chelsea inawachezaji wanaondana na mfumo huo. Jana Chelsea walikuwa vizuri sana tu nadhani Lampard ana future nzuri kama kocha hakuna uwoga katika uchezaji wao.
 
Huu utani wa jorginho huu, kwa tulioangalia game Jana tuliona hili tukio, #Cfc #Blues
 
Timu yetu ni nzuri na kila mwaka tunakua na kikosi kizuri shida inakuja makocha. Wakati Antonio Conte anachukua PL na kikosi mimi kwa upande wangu nilichukia sana, ushindi kilikua kinapatikana kwa ubabe sana bila kuonesha mpira mzuri wa kuvutia. Niliwaambia watu kua msimu unaofuata tutashuka chini sana, sababu ushindi ulikua unalazimishwa sana mpaka ikasababisha wachezaji kuchoka na pia timu pinzani wakawa wanacheza mpira bila kulazimisha ushindi bali kwa plan nzuri.

Alipokuja Sarri, wachezaji walikua na uwezo mzuri wa kucheza na kwa kiwango kizuri shida ikaja mbinu ya kocha. Kila wakati mpira ulikua unarudishwa nyuma mara nyingi zaidi na hicho kilikua kinawapa wapinzani nafasi ya kujipanga, mbinu ya Sarri ya kutokufanya wachezaji kua na uchu wa kufunga magoli ilisababisha tunatoka uwanja kwa kucheza mpira vizuri ila tumefungwa. Kocha alikuja kustuka kwenye mechi tano za mwishoni baada ya kuona wapinzani wako TOH na MAN U.

Mechi ya kwanza kwa upande wa Lampard, Chelsea v Man U; niliona wachezaji walivyokua na plan nzuri ya uchezaji ila wakawa wanachelewa na kutegeana kwenye kukaba na mwishowe tukafungwa magoli manne. Ile shida ya kukaba kwa kutegeana kilifanyiwa kazi kwa kiasi ndiyo sababu Liverpool walitufungwa kwa shida kiasi.

Kikosi kinashida ya wachezaji kuchoka kipindi cha pili kwa baadhi ya mechi na pia majerui wanaongezeka kila kukicha, kocha wa makipa hajatimiza wajibu vizuri kwani anatambua kabisa kua Keppa si mrefu sana ki maumbile na hajamweka vizuri ili ajue jinsi ya kuendea mpira ya juu za kwenye angle.

Kwa uchache haya ndiyo maoni yangu....Blues is my colour
 
Batshuayi kafunga goli la ushindi.. Halafu leo unasema tushukuru VAR ile game yetu na Liver uliwaambia waseme ahsante kwa VAR? Mahaba yenu ni motomoto

Kwahiyo ule mnazi alioupiga haujauona [emoji23][emoji23]alipobaki yeye na goli 🤣🤣au kwa kuwa Pepe ni mchezaji mkubwa kutoka timu kubwa ndio sababu mlikija kutoa povu kwa ile mis.....🤣🤣🤣🤣🤣


ThanKS VAR
 
Kazi kubwa ilifanywa na kovasic na jogihno
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…