Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Nawaambiaga siku zote kuwa Sariball inatukosti sana Chelsea, haya ss dkk 120 hizo cjui kwanini Ollachuga anajifanyaga ana makengeza kuhusu hili
Shida sio sarri ball, shida ni mabeki wa kati na washambuliaji, hili ni tatizo kubwa Chelsea tulilonalo kwa sasa
 
Hyo fainali hata sito angalia labda zola apa ge kikosi...auba na lacca mmmmmh
We ni Chelsea na hujui shida ya Chelsea mkuu?

Chelsea shida sio kocha wala kupanga team Bali hatuna mabeki wa kati viongozi na wala hatuna striker wa maana kwa sasa

Suluhisho kwa kuwa tumefungiwa basi warejee Zouma, tamy Abraham, na michy batshuay.

Kumbuka pia tuliwakosa watu muhimu Rudiger na Ngolo
 
Zapakosta atamuweka nani bench sasa mkuu cha msingi apambane kiwango chake kimeshuka mno tofauti na siku za nyuma
 
Kiufupi sarri amefanya kazi yake sawasawa, katutoa tulipokuwa msimu ukiopita katuleta tunapostahili kuwa, Chelsea sio team ya kukosa champions league hata Mara moja
 
Hapa pana Kamsiba unatarajiwa kutokea

Hivi Auba na Laka mumeshawahi kuwasikia?
Sijui mutawazuia kwa njia gani!
Itategemea siku hiyo wameamkaje na wamelalia upande gani,

Chelsea hata kama ni mbovu kuanzia beki na washambuliaji, siku wakiamka poa unaweza usiamini kama ndio wachezaji walewale uliowaona wakicheza Jana
 
Tusikate tamaa added advantage tuliyonayo Hazard, Luiz, azpi, willian,Ng'olo wamezoea kuchukua vikombe vizito tofauti na wenzetu hivyo wanajua uzito wa kombe kubwa na fainali zinachezwaje, wenzetu walichotuzidi ni kocha tu
 
Japo Luiz alifanya kosa kwenye goli la kusawazisha lakini baadaye alikuja kujirekebisha na tactical move nyingi alizitibua yeye kabla ya kuzuia goli la wazi dk ya 100. Generally Luiz ni mzito na mipira ya counter attack haziwezi
 
Nimefurahi japo kishingo upande, fainali sitahitaji tena kuwa na presha kama hii, utanipatia matokeo tukijaliwa uzima[emoji16]
 
Tatizo dogo la Zapacosta sio clinical kwenye crosses kama Emerson. Ndio tofauti ya Emerson na Alonso, Luiz pia kacheza vizuri sana ukiondoa ile blunder iliyozaa goli la kusawazisha. Katibua kama chances nne hivi za hao madogo bila kusahau lile goli la wazi dk ya 100
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…