Mkuu mimi sina tatizo na goal scoring record ya Higuain, Ukiangalia Performance yake wakati yuko AC Milan kwa mkopo utaona hajawa na msimu mzuri kivile, amefunga magoli 6 na assist 1 na amecheza dakika 1280. Anaumri mkubwa (32) sidhani kama ataendana na mpira wa kasi uliopo Chelsea sasahivi. Utaendelea kushuhudia magoli ya Chelsea yanafungwa na Hazard pamoja na Willian.
Na hata kama idadi ya magoli ya Juve imepungua sidhani kama Higuain angeperform vizuri kuliko Ronaldo kwa wakati huu, angalia record zao utaona, Ronaldo anagoli 15 na assist 5 ni wa pili kwa magoli pale Serie A anazidiwa goli moja na yule jamaa wa Sampdoria.