Kyatile
JF-Expert Member
- Feb 5, 2017
- 1,736
- 1,582
Conte ni mtu sahihi kwa Chelsea yetu. Tatizo tu kuna msuguano kati yake na bodi. Wachezaji anaowataka Conte siyo anaoletewa.Hivi kweli Sarri ni bora zaidi ya Conte? Mimi nadhani kama hakuna option bora zaidi ya Sarri basi abaki tu Conte. He is a serial winner View attachment 786936
Ni mtu ambaye anaweza kuimprove timu na wachezaji. Naweza kusema Chelsea ya kwetu angekaa nayo muda wa miaka mingine miwili tungekuja kupata timu nzuri sana.
Msimu huu ukweli ni kwamba hatukuwa na wachezaji ambao Conte anawahitaji hasa katika baadhi ya maeneo kama Striker na midfield. Lakini pia hatukuweza kupata beki wa kati mzoefu.
Sari ni kocha anayependa mpira wa pass(tick-tack) na kushambulia. Ni mpira mzuri ila ukichezwa bila malengo na mikakati madhubuti hauna maana. Mfano ni Tottenham ambao wamecheza mpira mzuri wa kuchambulia lakini mpaka sasa hawana cha maana walichochukua.
Isitoshe Chelsea haina aina ya wachezaji wa kucheza tick-tack. Kante, Fabrigas, Hazard, Christensen na Azpillicueta kidogo ndo wangeweza kufit. Sasa hapo ujue inakuwa vigumu kuchukua EPL kwa mazingira haya.
Sari atahitaji muda wa kutengeza timu inayofit style yake. Swali linakuwa ni je Chelsea itamvumilia kwa misimu miwili au mitatu?
Je klub itakubali kutumia pesa kama Man city wanavyofanya ili kununua wachezaji wa kufit style ya Sari?
Au yatakuwa kama ya Andre Boaz? Maana sababu ya kumleta Boaz ni sababu anapenda mpira wa pass ni offensive football. Lakini tunajua kilichompata. Sari is not an exception.
Tatizo jingine la Chelsea wachezaji fulani wanakuwa na power(indirectly) kuliko makocha. Kipindi kile walikuwepo Terry, Lampard, Drogba na Peter Cheki, Yaani hawa ilikuwa wakimchukia kocha basi hakuna namna lazima aondoke. Haka katabia naona kuna watu wamekarithi.
Alafu falsafa ya Conte ni work, work, work. Hii ni kama haieleweki kwa wachezaji wengi wa Chelsea, mfano mtu kama Willian mgogoro wake ni kwa sababu hapendi kunituma sana mpaka aamue.
So Sari peke yake hatamaliza matatizo ya Chelsea.
[HASHTAG]#Conte[/HASHTAG] abaki apewe World class sticker, full back mmoja mzoefu na kiungo mmoja pamoja na RWB. Atatusaidia sana.