Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

46F8353700000578-5143381-image-a-42_1512388487559.jpg


Defence ndo sijui itakuwaje...ingawa Luiz hatocheza..so hapo wanabaki hao wawili Christensen na Rudiger
 
Ratiba ya raundi ya tatu ya michuano ya kombe la Fa, imetangazwa usiku huu na michezo hiyo itachezwa wikiendi ya januari 6 na 7 mwaka 2018
Majogoo Liverpool wataanza michuano hiyo kwa kuchuana na wapinzani wao wa jadi Everton,huku bingwa mtetezi Arsenal akianzia ugenini kwa kucheza na Nottingham Forest.

Matajiri wa Manchester City wataanzia nyumbani katika dimba la Etihad,kwa kucheza na Burnley nao Manchester United wakiwalika Derby County.

Vijana wa Antonio Conte, Chelsea wataanzia ugenini kwa kucheza na Norwich, Tottenham Hotspur watakua wenyeji wa AFC Wimbledon
 
Ratiba ya michezo mingine ya raundi ya tatu ya kombe la Fa.

Birmingham City v Burton Albion

Brighton & Hove Albion v Crystal Palace

Coventry City v Stoke City

Bolton Wanderers v Huddersfield Town

Queens Park Rangers v MK Dons

Middlesbrough v Sunderland

Fleetwood or Hereford v Leicester City

Blackburn Rovers or Crewe Alexandra v Hull City

Cardiff City v Mansfield Town

Shrewsbury Town v West Ham United

Wolverhampton Wanderers v Swansea City

Newcastle United v Luton Town

Fulham v Southampton
 
Chelsea wanaweza kushika usukani wa Kundi C ikiwa watashinda nyumbani dhidi ya Atletico mechi ya Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku
Kikosi cha Antonio Conte kimeshajihakikishia nafasi 16 bora katika michuano hii, lakini Roma inaweza kushika usukani wa Kundi C ikiwa watakubali sare au kipigo dhidi ya Atletico mechi ya mwisho hatua ya makundi.
Chelsea wameitangulia Roma kwa alama mbili, lakini wana rekodi mbovu dhidi ya miamba hao wa Italia ambao wataikaribisha Qarabag katika mechi yao ya mwisho hatua ya makundi.

Atletico Madrid kwa sasa wanashika nafasi ya tatu na ni lazima waifunge Chelsea kupata nafasi yoyote kutinga hatua ya 16-Bora.
Kikosi cha Diego Simeone kitaitegemea Roma kupoteza pointi dhidi ya Qarabag vinginevyo wataangukia Ligi ya Europa 2018.
 
Habari za Timu


David Luiz hatakuwepo mchezoni kwa mara nyingine Chelsea watakapoikabili Atletico Madrid Ligi ya Mabingwa.
Luiz - kama ilivyo kwa Charly Musonda - anasumbuliwa na majeraha ya goti wakati bosi wa Blues akinuia kufanya uwiano mzuri kukaa kileleni mwa Kundi C lakini pia kushinda Jumamosi dhidi ya West Ham.
Mshambuliaji Michy Batshuayi alikuwa benchi lakini hakutumika katika mechi dhidi ya Newcastle, kwa hivyo anaweza kucheza.
Roma wanakwenda kuifunga Qarabag kwa hiyo wanachotakiwa Atletico ni kumaliza njaa yao ya kulipa kisasi dhidi ya Chelsea. Wameamka na wamefanikiwa kupunguza pengo dhidi ya Barcelona kwenye ligi ya nyumbani.
 
Meneja wa Chelsea Antonio Conte ameeleza ni kwa nini Cesc Fabregas anacheza mechi nyingi msimu huu
Kabla ya mechi tano za mwanzo msimu uliopita, kiungo huyo alikuwa ameanza mechi nne tu chini ya bosi huyo wa Kiitaliano.
Mwisho wa yote, Muhispania huyo alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Blues wakishinda taji na kwenye kampeni za 2017-18, Fabregas amecheza mechi 21 katika michuano yote, ikiwa ni pamoja na kuanza mechi 12.
"Nadhani Cesc mwanzoni hakucheza sana, lakini nilikuwa na furaha kwa sababu kupitia kazi anayofanya amejaribu kubadili akili yangu na imekuwa," Conte aliwaambia waandishi.
"Kama utakumbuka ngwe ya pili ya msimu uliopita alianza kucheza mara kwa mara. Sehemu ya kwanza ya msimu niliamua kucheza karibia kila mechi na [N'Golo] Kante na [Nemanja] Matic lakini sehemu ya pili ya msimu nadhani Cesc alicheza mechi nyingi.
"Nadhani alikuwa muhimu sana kwetu kutwaa taji msimu uliopita. Msimu huu ameendelea na kazi nzuri na kujituma na ameonyesha uwezo mkubwa na tabia njema."
Fabregas ametengeneza mabao manne na kufunga mawili katika kampeni za msimu huu.
 
Mtambue mdogo wake Hazard; Kylian Hazard.

Kylian Hazard (22), Eden’s younger brother who trained with the first team this morning, is one of a number of younger players to have done so this season.

Chungulia mechi ya leo, si ajabu unaweza kumwona among subs kwa mara ya kwanza.




kylianhazard1.jpg
 
Mtambue mdogo wake Hazard; Kylian Hazard.

Kylian Hazard (22), Eden’s younger brother who trained with the first team this morning, is one of a number of younger players to have done so this season.

Chungulia mechi ya leo, si ajabu unaweza kumwona among subs kwa mara ya kwanza.




kylianhazard1.jpg
Explosive midfielder huyooooo
 
Wakuu kwa wale wa mobodro ni channel gani wanaonyesha match yetu na Atm
 
Hivi ni kigezo kipi kilichoiweka Chelsea ya pili wakati wao wana GD ya 8 na Roma ni chin ya hapo
50f5e106e22a9df808bb54025770aafe.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom