Kwanza kabisa niwapongeze wana Cfc wote kwa ushindi mwembamba kabisa, hatimae kuondoka n.a. point yetu 3 kirohoo safi kabisa.
Pili, mpira ina makosa madogodogo ambayo hutokea bila player kutarajia n.a. kucost timu. Kwenye timu yetu niliona makosa yakitokea Kati kipindi cha kwanza kwani palipwaya sana n.a. kusababisha wapinzani kumiliki na kutawala mchezo kwa muda mrefu.
Tatu, wachezaji ambao hawakwepo kabisa kwenye form ni Fabrigas, Diego, Moses hawa wachezaji usiku wa Jana haikuwa pouwa kwao kabisa walipwaya kwa kiasi fulani. Moses hakipata mpira anabutua au anatoa pass kwa kipa kwa kweli nilikuwa nakereka sana n.a. hali hii. Costa kuna pasi mbili alitengenezewa n.a. Hazard angekuwa yule Costa wa mwanzo basi angepiga Hatrick n.a. kuondoka n.a. mpira wake. Fabrigas nae jana alikuwa mwepesi kama mlenda n.a. kukimbia uwanjani ovyo na kumfanya Kante afanye kazi kubwa sana. Mwisho wa yote anasababisha kosa ambayo pengine tungekuwa one one basi tungechukua point Moja tu.
Nne, Natoa pongezi kwa Hazard, Kante, Luis, Cahil, Azilipicueta kwa kazi nzuri waliyoifanya. Kweli hawa wachezaji walifanya kazi kubwa sana kuakikisha tunatoka n.a. ushindi muruaa kabisa. Big up to them.
Maoni yangu. Kama Conte ameingia uwanjani kwa kuitaji point 3 au timu inapigania ushindi basi fabrigas aanzie bench au conte acheze 3.5.2 lasivyo Fabrigas asubiri. All in all tukutane next game Stanford Bridge tukiwakaribisha Manure kwenye FA Cup.
Nawasilisha.