Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Semeni alhamdullulah jirani zangu maana mgonjwa kapiga chafya mlango wa mortuary acha tumrudishe ICU.
 
Fabregas:

Ukimuangalia Fabregas alivyokuwa akicheza leo ni dhahiri alikuwa akicheza huku akiwa na mawazo sana kichwani.

Nikajaribu kuingia akilini mwake nikaona anachowaza. Msimu ujao bila mechi za ulaya...umri umeshamtupa bila michezo ya hivyo hata nafasi yake walau ya kuitwa timu ya taifa ni finyu sana. Amecheza akiwa na huzuni mno.
 
Mikel Obi:

Huyu ni garasa ambaye leo kutokana na kuharibu kwa Remmy na Oscar amejificha hapo kati.
Muda wote anacheza akirusha mikono sijui anamlalamikia nani. Mtazamo wangu ni kuwa umri umemtupa. Hana mbavu na wepesi tena wa kuwakinga mabeki. Matokeo yake anawagharimu kina Willian kuja chini kumsaidia. Ndipo unakuta tuna pass 500 ila asilimia kubwa zinachezewa nusu yetu.

Umri umemtupa Mikel kama vipi ahamie China...najua Hidink anamtumia kwa kuwa ndiyo waliokuwa wamebaki wenye uchungu na Chelsea ila wakati mwingine hata kukaa pembeni ni busara na bado utakuwa unaipenda timu vilevile.
 
Substitutions bench:

Leo ndo nimegundua tuna benchi dhaifu sana. Na hivi ambavyo hatutakuwepo michuano ya Ulaya ndiyo sielewi ni nani atajisikia prestigious kuja kwetu kukaa benchi la kucheza EPL.

Kuna haja ya kuwatafuta academy players the best - not Loftus Cheek - waingie kuokoa prestige ya chama.

Oscar..Remmy...hawa ni baadhi ya waliocheza leo just because i
 
courtois_getty.gif

Huyu nae anapua ndefu kama babiani. bora auzwe tu.
 
courtois_getty.gif

Huyu nae anapua ndefu kama babiani. bora auzwe tu.
Huyu wajanja wameshamjua,mikwaju ya chini haipendi kabisa, hapendi kugaragara kwenye matope
Akiona mpira wa chini anajifanya makengeza au kipofu.
 
Substitutions bench:
Leo ndo nimegundua tuna benchi dhaifu sana. Na hivi ambavyo hatutakuwepo michuano ya Ulaya ndiyo sielewi ni nani atajisikia prestigious kuja kwetu kukaa benchi la kucheza EPL.
.....
Ile penalty ilikuwa ya bahasha au mlibarikiwa?
Mna bahati, mmechomoa leo.
 
Substitutions bench:

Leo ndo nimegundua tuna benchi dhaifu sana. Na hivi ambavyo hatutakuwepo michuano ya Ulaya ndiyo sielewi ni nani atajisikia prestigious kuja kwetu kukaa benchi la kucheza EPL.

Kuna haja ya kuwatafuta academy players the best - not Loftus Cheek - waingie kuokoa prestige ya chama.

Oscar..Remmy...hawa ni baadhi ya waliocheza leo just because i
Bado tunaweza kupenya mechi za ulaya msimu ujao! Miujiza huwa inatokea kwenye soka! Mi sijakata tamaa bado mpaka hapo hesabu zitakapogoma kabisa!
 
Msimu umekwisha kwa Chelsea - Tujipange Upya 2016-2017

Karibu sana Darajani - Antonio Conte, Tumaini Jipya ChelseaFC.

Italy-v-Romania-International-Friendly

Kabla ya kufanya usajiri upya jaribu kuangalia wachezaji wote walioko mkoponi, kama wanaweza kuja kutusaidia. On Loan Players

Tuna machungu makubwa si kupoteza Ubigwa tu bali kufungwa na timu za ajabu ajabu na hata kukaribia kuvuruta mkia wa ligi kuu - hii imetushitua sana na kutuumiza mno.

Wachezaji wote waliosababisha hali hii waangaliwe kama bado wana moyo wao wa kuitumikia Chelsea Fc, kama vipi basi tuwauze maana sisi washabiki na hata Club hatujazoea kuishi kwa pressure kama wenzetu mtaa wa pili - sisi ni Mabingwa na tutaendelea kuwa Mabingwa.

Yaliyopita Yamepita - Karibu msimu mpya tupambane!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom