Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Niliumia kwa mengi;

1. Tangu nilipoona kikosi nilijua hatushindi mechi

2. Nilienda kuangalia mechi na shemeji yako.

3. Ili kunisapoti (ingawa yeye ni Arsenal) alivaa jezi yangu ya Chelsea

4. Mbaya zaidi kwa kuwa ilikuwa J'mosi jioni nguo zangu nyingine (zikiweno jezi nyingine za Chelsea) nilikuwa nimezifua hivyo mimi nilivaa kawaida tu

5. Ushawahi kuaibishwa mbele ya demu wako wewe???

Acha bana Nonda acha bana...inauma we acha tu...for the first time nilitoka kama naenda chooni kumbe naenda kujifuta machozi. Watu wote wanamcheka yeye yani...dah! acha tu... RRONDO herrera Belo everlenk cute b acheni kututania bana...ya juzi mi iliniuma! Mbona ya Man city sikuwaomba mnyamaze..hii tu potezeeni iishe!

6. Tulikuwa tumekubaliana weekend ijayo mimi nivae jezi yake ya Arsenal yeye avae yangu. Baada ya game ya juzi eti akakataa...eti hataki kuaibika tena....do you understand what am saying guys!???? tuacheni kwa hili..yani sina raha kabisa yani...!

Halafu unauliza kwa nini niliumia Nonda???!

Polee mkuu wangu.
Inaumaga kweli.. hata mimi nilishawahi kulia kwa ajili ya timu yangu kufungwa.
Sitanii tena Mentor
 
Last edited by a moderator:
Despite kinachoendelea ambacho kinawafanya wengi wamuone Mou kama kocha mbaya...mimi bado naamini tukiwa na Mou tunakuwa timu inayotisha zaidi ya tukiwa na kocha mwingine yeyote yule.

Nahisi kutaka trasition from defence-based team to attack-minded team kwa haraka ndo kunapelekea hizi results. Turudi kwanza kwenye defence huku akisuka kikosi (kununua) kwa kuanzia nyuma. Am sure bado tunayo nafasi ya kutetea kikombe chetu.
.......
Hiyo -ekundu... Mentor una uhuru wa kuota ndoto yoyote ile. Ingawaje ni mapema lakini Chelsea inahitaji miujiza kuweza kutetea kikombe "chenu". Kuna uwezekano wa Chelsea kumaliza msimu nje ya top-four.

Hilo la kuwa Chelsea inataka kuacha ku-park bus...nilishamiambieni msijaribu, mmezoea mieleka na rugby na ndio mtindo wa uchezaji anaopendelea Mou. Anataka kuiga mbinu za Man City, Arsenal, Man United ya kucheza kabumbu ategemee maumivu tu.

Mou hajali utamu wa kandanda , anajali kushinda vikombe tu. Lakini ile kubezwa "Chelsea boring, boring" imemfanya aingie mkenge.
 
Duuu wanavyotia huruma daah.
Ila washazoea maumivu so hata wakifungwa kesho kutwa hawataumia.
Na mimi nasema wapigwe tuu.
Nataka nione ENZO akilia
Ukiona hii Kijana Enzo iambie irudi hapa jukwaani. Hii kijana italia tu msimu huu, kama wakongwe, Ntuzu, Mentor wameonesha njia, kulia inaruhusiwa.
 
uploadfromtaptalk1442233923258.png
 
naona mnaongea! matatizo ya blues tunayajua sisi fans wake bhana soon special one atarekebisha mambo!
 
Ukiona hii Kijana Enzo iambie irudi hapa jukwaani. Hii kijana italia tu msimu huu, kama wakongwe, Ntuzu, Mentor wameonesha njia, kulia inaruhusiwa.

Huyu kijana lazma ajifiche maana alitunyanyasa sana man u kusema tumesajili wababu
 
naona mnaongea! matatizo ya blues tunayajua sisi fans wake bhana soon special one atarekebisha mambo!
Unaweza kutunong'oneza na sisi hayo matatizo unayoyajua wewe fan wa ze bluuzz?

Mentor na Ntuzu walishaorodhesha machache.

Kwani Ze bluuzz ina matatizo? Yepi?

Kufungwa na kupoteza mechi chache ni matatizo?

The special one akiweza kurekebisha domokaya lake, ataweza pia kurekebisha "mambo".
 
Huyu kijana lazma ajifiche maana alitunyanyasa sana man u kusema tumesajili wababu
Everton wameleta amani jukwaa la Ze bluuzzz.

Enzo ameenda shule na mwalimu alibaini Enzo ana macho mekundu, anatumikia adhabu ya kuvuta "sigara na bange".

Mwalimu alipojua kuwa Enzo ni shabiki wa Ze bluuzz amemfutia adhabu ya viboko.
 
Naona ktk thread ya timu bora the blues watu hawaishi kupita........nafurahi sn kuona watu wako pamoja na sisi..

Binafsi sishangai sn kwa Timu kupata matokeo km hayo kwao Everton.....

Tangu Mourinho arudi darajani kwa Mara ya pili ameshinda Mara moja tu ktk hicho kiwanja.

Ktk vitu ambavyo havinisumbua kua kuna baadhi ya viwanja wakiiona Chelsea imetua kwao basi wako radhi kucheza na kufia uwanjani kikiwepo na kiwanja cha hawa Everton. Kwahiyo ukiwa unayajua haya wala hayakusumbui.

Ninachofurahi tumepoteza ikiwa ni September... Lkn km tungepoteza ikiwa mwezi wa 4 basi nisingekua na amani....

Msimu uliopita tulikua mabingwa huku tukiwa tumepoteza game 3 hivi km sikosei....na kupata sare nyingi tu na bado tuka mabingwa. Naamini kwamba timu zingine zitapoteza Zaidi ya game 3 na kupata sare nyingi na hii litaanza kwa Arsenal tarehe 19 atapoteza mchezo wake wa pili....

Bado tuna uwezo wa kua mabingwa wa epl na huwezi kuitoa Chelsea ktk mbio za kuwania ubingwa.... Huko kutakua ni kuota mchana kweupe.
 
Unaweza kutunong'oneza na sisi hayo matatizo unayoyajua wewe fan wa ze bluuzz?

Mentor na Ntuzu walishaorodhesha machache.

Kwani Ze bluuzz ina matatizo? Yepi?

Kufungwa na kupoteza mechi chache ni matatizo?

The special one akiweza kurekebisha domokaya lake, ataweza pia kurekebisha "mambo".

Mbinu za mpira ni nyingi ata km ukiweza kuutumia mdomo wako vzr hiyo ni moja ya mbinu nzuri pia.... Sasa unataka Mou arekebishe mdomo wake akae kimya au vipi? Najua timu zote na mashabiki wote mnafurahi kuona Chelsea ikipambana kweli kweli kua bingwa.... Tumeshasahau matokeo ya Everton sasa tunafikiria Uefa kwanza then tuje kwa gunners.
 
Hiyo -ekundu... Mentor una uhuru wa kuota ndoto yoyote ile. Ingawaje ni mapema lakini Chelsea inahitaji miujiza kuweza kutetea kikombe "chenu". Kuna uwezekano wa Chelsea kumaliza msimu nje ya top-four.

Hilo la kuwa Chelsea inataka kuacha ku-park bus...nilishamiambieni msijaribu, mmezoea mieleka na rugby na ndio mtindo wa uchezaji anaopendelea Mou. Anataka kuiga mbinu za Man City, Arsenal, Man United ya kucheza kabumbu ategemee maumivu tu.

Mou hajali utamu wa kandanda , anajali kushinda vikombe tu. Lakini ile kubezwa "Chelsea boring, boring" imemfanya aingie mkenge.

Tutamaliza ligi tukiwa mabingwa na wala haiitaji miujiza. Unaweza ukawa bingwa ata km umefungwa michezo 7
 
Mbinu za mpira ni nyingi ata km ukiweza kuutumia mdomo wako vzr hiyo ni moja ya mbinu nzuri pia.... Sasa unataka Mou arekebishe mdomo wake akae kimya au vipi? Najua timu zote na mashabiki wote mnafurahi kuona Chelsea ikipambana kweli kweli kua bingwa.... Tumeshasahau matokeo ya Everton sasa tunafikiria Uefa kwanza then tuje kwa gunners.
Kuifunga Gunners ndio itawapatia ubingwa?

Umeziacha timu za Man. city na Man united katika orodha yako kwa timu mtakazozishughulikia kwa bahati mbaya au ndio kukiri kimya kimya kuwa msimu huu Ze bluuzz inaugua kwashiorkor?

Tuna-miss mieleka na rugby ya Chelsea.

Yokohama choma mafuta, ongeza speed. wiki end hii naiona Ze bluuzz ikiwa nafasi ya 18.
 
Niliumia kwa mengi;

1. Tangu nilipoona kikosi nilijua hatushindi mechi

2. Nilienda kuangalia mechi na shemeji yako.

3. Ili kunisapoti (ingawa yeye ni Arsenal) alivaa jezi yangu ya Chelsea

4. Mbaya zaidi kwa kuwa ilikuwa J'mosi jioni nguo zangu nyingine (zikiweno jezi nyingine za Chelsea) nilikuwa nimezifua hivyo mimi nilivaa kawaida tu

5. Ushawahi kuaibishwa mbele ya demu wako wewe???

Acha bana Nonda acha bana...inauma we acha tu...for the first time nilitoka kama naenda chooni kumbe naenda kujifuta machozi. Watu wote wanamcheka yeye yani...dah! acha tu... RRONDO herrera Belo everlenk cute b acheni kututania bana...ya juzi mi iliniuma! Mbona ya Man city sikuwaomba mnyamaze..hii tu potezeeni iishe!

6. Tulikuwa tumekubaliana weekend ijayo mimi nivae jezi yake ya Arsenal yeye avae yangu. Baada ya game ya juzi eti akakataa...eti hataki kuaibika tena....do you understand what am saying guys!???? tuacheni kwa hili..yani sina raha kabisa yani...!

Halafu unauliza kwa nini niliumia Nonda???!

Pole sana mkuu kulia ni jambo la kawaida ila usirudie kwenda na shemeji
 
Last edited by a moderator:
Tutamaliza ligi tukiwa mabingwa na wala haiitaji miujiza. Unaweza ukawa bingwa ata km umefungwa michezo 7
Kwa hiyo mtafungwa michezo saba tu?

Na Man City itafungwa michezo nane?

Ndoto ni dunia ingine kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom