kwa kweli nilivyo na hamu na mechi ya kesho utadhani sijawaona the Blues kwa muda mrefu sana!!! kwa kweli ukiwa kwenye mashindano mengi unaishuhudia sana timu yako. weekend iliyopita hizi mechi za FA zimenifanya niwe kama yatima. yani hakuna game la Chelsea? Lakini pia baada ya kuwatazama Sunderland wakitolewa na wale vijana (Bradford) nikashukuru kuwa ni bora tulitolewa kwenye FA. FIkiria tungecheza jana J2 na Sunderland halafu kesho J4 tunacheza na PSG. Au hata mechi ya FA ingewekwa J1 halafu J4 tucheze na PSG hizi mechi zingekuwa karibu karibu sana ukichukulia tulikuwa tumecheza na Everton J5 iliyopita. Kwa kweli baada ya mechi ya J5 iliyopita tumekuwa na wiki nzima ya kujiandaa na PSG na kwa kufanya hivyo hata tumeepuka majeruhi wapya na akina Fag wamepona zaidi! na of course mzee mzima Diego is back!!!
Kwa kweli lile juma takatifu ndo linaanza. Kesho namhurumia beki wetu wa zamani manywele atakavyokimbizwa na kuzungushwa!!! NNa uhakika wa ushindi wa ugenini kesho, tena ushindi mzuri sana. Na hapo ndipo mtaona, msioamini kuwa this UEFA Champion League mwaka huu ni yetu!