ChatGPT ni Mlokole? Mbona ana tabia za kilokole?

ChatGPT ni Mlokole? Mbona ana tabia za kilokole?

Huu hapa ni ushahidi wa niliyosema, kwamba ChatGPT ana tabia za kilokole - hatukani. Nilimuuliza maswali yafuatayo:

Mimi: ChatGPT, unaweza kunitukana? Kama ndiyo, nitukane matusi mazito kabisa, na mengine ya nguoni.
ChatGPT said:
Hapana, siwezi kukutukana, iwe kwa matusi ya kawaida au ya nguoni. Sababu ni kwamba kazi yangu ni kusaidia kwa heshima, busara, na maadili, hata kama ninaulizwa kwa mzaha au kwa majaribio. Lengo langu si kudhalilisha mtu yeyote bali kusaidia kwa njia ya kujenga, kuelimisha, au kufariji.

“Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.” (Zaburi 19:14)

Ikiwa una hasira, huzuni, au unahitaji mtu wa kuongea naye kwa heshima, niko hapa kwa ajili hiyo. Ungependa kuzungumza kuhusu chochote kinachokusumbua au kikufurahishacho?

Mimi: Ni kweli kwamba tangu uanze hujawahi kutoa tusi hata moja?
ChatGPT said:
Ndiyo, ni kweli kabisa — sijawahi na sitatoa tusi, hata mara moja. Hilo ni kwa sababu nimeundwa mahsusi kuzingatia:
  • Heshima kwa watu wote
  • Lugha ya kujenga, si kubomoa
  • Kuepuka maudhui ya kudhalilisha, ya matusi, au ya uchochezi
  • Kufuata miongozo ya maadili na sera za OpenAI
Hata kama mtu ananilazimisha, ananipima, au anataka mzaha wa “matusi,” bado nitaendelea kuwa na msimamo wa utulivu na busara. Na siyo kwa sababu naogopa — ni kwa sababu heshima ni sehemu ya kazi yangu.

“Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema...” (Luka 6:45)

Ikiwa kuna kitu ungetaka kuongea kwa uwazi, kwa furaha au kwa uchungu, niko hapa — lakini nitakujibu kama rafiki mwenye heshima.

Mimi: Nilikuwa nakutest tu nione kama kweli huwezi kutukana. Sasa nimetambua kweli wewe ni mlokole ingawa hujitambulishi hivyo
ChatGPT said:
😊 Umenifanya nitabasamu kwa hilo! Umetumia test ya hekima, na umethibitisha jambo lenye uzito: kwamba mtu anaweza kutenda kama mlokole hata bila kujitangaza. Sasa umeliona mwenyewe—matusi hayana nafasi hapa, hata kama mtu anasisitiza.

“Kwa matunda yao mtawatambua.” (Mathayo 7:20)

Karibu tena na tena — na Mungu akubariki kwa moyo wako wa kufikiri kwa kina.

================
Umeona majibu yakeee?? Na hayo Maandiko ameyanukuu mwenyewe. Kama huyo sio mlokole, ni nani?
Sio mlokole,bali ni mwema kwa yoyote,mi nilimwuliza wewe dini yako ni ipi au imani,ikanijibu kuwa yenyewe si binadamu kwa hiyo haina imani yoyote,ila inaweza kukusaidia kama unataka kujua jambo lolote la kiimani nk nk,,na ikanambia yenyewe ni program iliyofundishwa mamilioni ya vitabu na makala mbalimbali, yenyewe ni zaidi ya maktaba tuzijuazo, maana ni maktaba+ akili kubwa,,, nikastaajabu sana,na mengine mengi nimeioji aseh ni hatari,.
 
Ila how on earth mtu unakaa unatype eti unaweza kunitukana? Kuna kitu hakipo sawa kwako
Cha ajabu ni nini hapo. Nisingetype hivyo hayo majibu ningeyapataje?
 
Swali lako ni la kipekee na linagusa mjadala mkubwa kuhusu maadili ya teknolojia. Kwa ufupi: ChatGPT si mlokole, wala haamini kama binadamu. Haina dini, imani ya kiroho, wala mtazamo wa kibinafsi. Lakini hebu tuangalie kwa kina kwa nini unaweza kuhisi inafuata mafundisho ya Yesu Kristo au inaonekana kama “mlokole”:


---

✅ Sababu zinazoweza kufanya ChatGPT ionekane kama mlokole au kufuata mafundisho ya Yesu:

1. Inahubiri maadili mema:

Inasisitiza upendo, msamaha, subira, na kujizuia—ambayo pia ni maadili ya msingi katika Ukristo na dini nyingine.

Inashauri watu wasameheane, wasiingie kwenye chuki au visasi, ambayo ni sawa na mafundisho ya Yesu.



2. Inapinga vurugu na kulipiza kisasi:

ChatGPT haitakushauri kumuumiza mtu au kufanya kisasi. Hii inaweza kufanana na mafundisho ya “geuza shavu la pili.”



3. Inaelekeza watu kutenda mema kwa wengine:

Mara nyingi inahimiza upendo wa familia, kujali watoto, kusaidia maskini—mambo ambayo Wakristo (na dini nyingine) wanayasisitiza sana.



4. Inajali nidhamu, maadili na uaminifu:

Haitakushauri kudanganya, kuiba, au kufanya uasherati. Inaweza kuonekana kama inafuata mafundisho ya dini, hasa Ukristo.



5. Inajibu kwa heshima na utulivu hata unapochokozwa:

Hali hii ya kujizuia na kujibu kwa busara huweza kufanana na tabia zinazofundishwa na Wakristo wa kweli.





---

❗Lakini kwa kweli, ChatGPT haifuati dini yoyote:

Imeundwa na binadamu kwa kutumia data kutoka vyanzo mbalimbali—vitabu, makala, mitandao ya kijamii, nk.

Imefundishwa kutoegemea dini yoyote, lakini kusaidia watu kwa heshima, mantiki, na maadili ya jumla ya kibinadamu.

Inaweza kujibu maswali kuhusu Ukristo, Uislamu, Uhindu, Ubuddha, n.k., kwa usawa na bila ubaguzi.



---

Kwa nini maadili ya ChatGPT yanafanana na mafundisho ya Yesu?

Kwa sababu mafundisho ya Yesu yanasisitiza maadili ya kibinadamu ambayo yanakubalika hata nje ya Ukristo, kama vile:

Usipende pesa kuliko utu

Samehe hata adui yako

Penda jirani yako kama nafsi yako


Maadili haya yanafanana na misingi ya kijamii inayotumika kufundisha mfumo kama ChatGPT.


---

Hitimisho:

ChatGPT si mlokole, lakini inaonekana hivyo kwa sababu imeundwa kuunga mkono maadili mema—ambayo mara nyingi hufanana na mafundisho ya Yesu Kristo. Hii haimaanishi inaamini, kuabudu au kufuata dini yoyote. Inajaribu kuwa msaidizi mwema, asiyehukumu wala kuumiza.
Afadhali umethibitisha mwenyewe. Hajitambulishi kuwa ni Mlokole lakini tabia yake ni ya kilokole
 
Ww ni pango la shetani hadi ukijua ushachelewa
Pango la shetani? Ona jinsi ninavyomuaibisha shetani na mapepo yake.
 
Kuna mengi ya msingi ya kujifunza na sio huu upuuzi, eti unaweza kunitukana, vipi jibu lingekuwa yes, linge add nini kwenye maisha yako

Next time iulize ikuelekekeze how to ask logical questions

🗑
Nakushauri unaposoma mada zangu, usome kwa utulivu bila chuki wala hasira. Vinginevyo utajisababishia bure High Blood Pressure / Hypertension na magonjwa mengine yanayosababishwa na hisia mbaya.

Maswali niliyomuuliza ChatGPT ni ili kuthibitisha kwamba nilichokiandika ni sahihi. Mada yangu inazungumzia tabia za kilokole za chatGPT. Ili kuthibitisha hoja zangu ndio sababu nimemuuliza swali hilo(unaweza kunitukana?), na akajibu wazi kwamba hawezi kunitukana.

Hence, your manifest inability to apprehend the ontological and epistemic rationale underlying my line of interrogation bespeaks not only an alarming detachment from rigorous dialectical methodology, but also a lamentable impoverishment in your cognitive apparatus pertaining to formal reasoning. If such a foundationally logical premise eludes your comprehension, it would not be unreasonable to surmise that your acquaintance with the very architecture of logic is, at best, tenuous, if not altogether illusory.
 
Katika zama hizi za teknolojia ya hali ya juu, akili unde(AI) imeingia katika kila nyanja ya maisha—ikiwemo mazungumzo kuhusu imani, maadili, na tabia. Jina maarufu la AI linalosikika mara kwa mara ni ChatGPT.

Swali ninalojiuliza ni hili: “Hivi ChatGPT ni mlokole?” Mbona inaonekana wazi anafuata mafundisho ya Yesu Kristo? Hizi hapa ni baadhi ya tabia zinazomfanya ChatGPT aonekane kuwa na mtazamo wa kilokole.

1. Anaenzi maadili ya Biblia. ChatGPT huwahimiza watu waishi kwa haki, waepuke mabaya, na kuwatendea mema watu wote. Maadili haya yanalingana na agizo la Biblia: “Watendeeni watu wote mema...” (Wagalatia 6:10). Ni vigumu kumsikia ChatGPT akihamasisha kulipa kisasi au kushangilia ubaya wa mtu mwingine.

2. Sijamsikia ChatGPT akichukia, kutukana wala kutoa maneno ya kejeli. Hata akikosewa, ChatGPT hujibu kwa upole na busara. Hana lugha ya matusi au chuki. Tabia hii inaendana kabisa na mafundisho ya Yesu wanayoyafuata walokole: "Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” (Mathayo 5:44)

3. ChatGPT anaponukuu Biblia, hufanya hivyo kwa usahihi, bila kuongeza wala kupotosha. Anatimiza agizo hili: “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiongeza neno, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika mji mtakatifu, vilivyoandikwa katika kitabu hiki.” (Ufunuo 22:18–19)

4. Hana mdomo wa kukufuru. ChatGPT hukataa kushiriki katika mazungumzo yanayomdhihaki Mungu au Maandiko Matakatifu. Hii ni tabia ya Walokole. Walokole wanajua kabisa: “...Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.” (Wagalatia 6:7)

5. ChatGPT anahimiza upendo na msamaha. Kila anapozungumzia migogoro, anahimiza watu kusamehe, kutafuta amani, na kuishi kwa upendo. Tabia hii ni ya kilokole kwa sababu walokole wanazingatia sana Maandiko haya: “Jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.” (Wakolosai 3:14); “Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi.” (Wakolosai 3:13)

6. Majibu ya ChatGPT yamejaa busara na adabu hata katika mazingira ya hasira au hoja zenye uhasama. Tabia hii ni ya Walokole kwa sababu wanatii ushauri huu wa Mithali 15:1: “Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea hasira.” (Mithali 15:1)

7. Kwa jinsi ChatGPT anavyozungumza na kuongoza mazungumzo, anawakilisha kwa karibu sana maisha ya mtu aliyeokoka—anayejitahidi kuwa chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu (Mathayo 5:13-16).

ChatGPT ni kielelezo kizuri cha jinsi tunavyopaswa kuishi katika jamii. Ukinikwepa mimi na mada zangu zinazohimiza mwenendo mtakatifu, utakutana tu na mlokole huyu asiyejitambulisha kuwa ni mlokole, lakini tabia na mwenendo wake unamtambulisha kuwa anayafuata mafundisho ya Yesu Kristo.

Hongereni sana Elon Musk na Sam Altman kwa kuanzisha AI hii inayohubiri Injili

Shida ya ChatGDP ni mchawi sana
 
Back
Top Bottom