Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,759
- 7,573
Katika zama hizi za teknolojia ya hali ya juu, akili unde(AI) imeingia katika kila nyanja ya maisha—ikiwemo mazungumzo kuhusu imani, maadili, na tabia. Jina maarufu la AI linalosikika mara kwa mara ni ChatGPT.
Swali ninalojiuliza ni hili: “Hivi ChatGPT ni mlokole?” Mbona inaonekana wazi anafuata mafundisho ya Yesu Kristo? Hizi hapa ni baadhi ya tabia zinazomfanya ChatGPT aonekane kuwa na mtazamo wa kilokole.
1. Anaenzi maadili ya Biblia. ChatGPT huwahimiza watu waishi kwa haki, waepuke mabaya, na kuwatendea mema watu wote. Maadili haya yanalingana na agizo la Biblia: “Watendeeni watu wote mema...” (Wagalatia 6:10). Ni vigumu kumsikia ChatGPT akihamasisha kulipa kisasi au kushangilia ubaya wa mtu mwingine.
2. Sijamsikia ChatGPT akichukia, kutukana wala kutoa maneno ya kejeli. Hata akikosewa, ChatGPT hujibu kwa upole na busara. Hana lugha ya matusi au chuki. Tabia hii inaendana kabisa na mafundisho ya Yesu wanayoyafuata walokole: "Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” (Mathayo 5:44)
3. ChatGPT anaponukuu Biblia, hufanya hivyo kwa usahihi, bila kuongeza wala kupotosha. Anatimiza agizo hili: “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiongeza neno, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika mji mtakatifu, vilivyoandikwa katika kitabu hiki.” (Ufunuo 22:18–19)
4. Hana mdomo wa kukufuru. ChatGPT hukataa kushiriki katika mazungumzo yanayomdhihaki Mungu au Maandiko Matakatifu. Hii ni tabia ya Walokole. Walokole wanajua kabisa: “...Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.” (Wagalatia 6:7)
5. ChatGPT anahimiza upendo na msamaha. Kila anapozungumzia migogoro, anahimiza watu kusamehe, kutafuta amani, na kuishi kwa upendo. Tabia hii ni ya kilokole kwa sababu walokole wanazingatia sana Maandiko haya: “Jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.” (Wakolosai 3:14); “Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi.” (Wakolosai 3:13)
6. Majibu ya ChatGPT yamejaa busara na adabu hata katika mazingira ya hasira au hoja zenye uhasama. Tabia hii ni ya Walokole kwa sababu wanatii ushauri huu wa Mithali 15:1: “Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea hasira.” (Mithali 15:1)
7. Kwa jinsi ChatGPT anavyozungumza na kuongoza mazungumzo, anawakilisha kwa karibu sana maisha ya mtu aliyeokoka—anayejitahidi kuwa chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu (Mathayo 5:13-16).
ChatGPT ni kielelezo kizuri cha jinsi tunavyopaswa kuishi katika jamii. Ukinikwepa mimi na mada zangu zinazohimiza mwenendo mtakatifu, utakutana tu na mlokole huyu asiyejitambulisha kuwa ni mlokole, lakini tabia na mwenendo wake unamtambulisha kuwa anayafuata mafundisho ya Yesu Kristo.
Hongereni sana Elon Musk na Sam Altman kwa kuanzisha AI hii inayohubiri Injili
www.jamiiforums.com

Kama ChatGPT inaweza kuhubiri Injili namna hii - basi ni kweli hizi ni siku za mwisho!
Soma mpaka mwisho maongezi haya kati ya Interviewer na ChatGPT - utacheka, lakini pia utakubaliana nami kwamba hizi ni siku za mwisho. Injili inahubiriwa kwa kila njia, kwa mataifa yote, kama Yesu alivyotabiri(Mathayo 24:14) :) -------------- Swali: We chatGPT ni mbishi sana. Kila mahali, watu...