Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Yote hayo hayana maana yoyote bila katiba bora inayo akisi maoni ya Wananchi.
Mpaka sasa suluhisho mojawapo ni katiba,katiba ya sasa,kwa mujibu wa nyerere,angeweza kuwa dikteta,nyerere alijizuia,hawa waliomfuata je? Nyerere ndio mzizi wa matatizo ya nchi kiuchumi,kisiasa,kijamii,kielimu na mila kitu,katuachia katiba mbovu,kaiacha Ccm imekaa kinafikinafiki,nchi aliiacha haina taasisi imara japo aliitawala kwa miaka 27,kwa muda wote huo alikuwa kama anatawala Shamba tu....madhara yake ndio haya,hatuwezi kumlaumu kiongozi yeyote bila kupata mzizi wa tatizo....mzizi ni nyerere,huyu aliwafanya wazee wetu wafe maskini,kwa kuua uchumi wa mtu mmoja mmoja,kafanya watanzania wawe wavivu,kaua vyama vya ushirika,ni mtu wa kwanza kuua viwanda vya sekta binafsi,kaua sekta ya Nyumba.....mengine ongezea
 
Wanabodi,

Hapa simzungumzii mtu yoyote bali nazungumzia hulka za watu wenye tabia za udikiteta katili, kitu kinachoitwa "character assassinations" ndio "modus oparandi" ya madikiteta wote duniani, na huanza kwa kuwa populist kwa kuonyesha heroick actions hivyo kushangiliwa sana kama mashujaa na kupendwa sana na watu!.

Hulka hizo za udikiteta zinatokana na kitu kinachoitwa "deep rooted neurosis" kwa madikiteta hawa kuwa waliteswa sana utotoni!, baadhi yao walikataliwa ndani ya familia, na hii hutokea baba kuhisi mtoto huyo sii wa kwake kwa kumhisi mke alichepuka, mama kamwe hawezi kukiri kuchepuka hata kama ni kweli alichepuka, hivyo baba anakuwa anamtesa sana mtoto, na mama hawezi kuingilia!, mtoto wa aina hiyo anakuwa amekulia katika usongo mkubwa wa mawazo, unaomtia hasira kusoma kwa bidii na huku ana visasi ili kuonyesha mateso hayo ni jambo la kupita tuu, na kweli wengi hufanikiwa, na wakiishafika at the top!, ndipo ile "deep rooted neurosis" ya kumbukumbu ya mateso iliyohifadgiwa kwenye "sub conscious mind" inaibuka na kupelekea kumfanya mtu huyo kuwa katili!, kwa ku inflict pain kwa njia za character assassinations, anaumiza ukiumia yeye ndio anapata furaha!.

Madikiteta wa Roma ya kale, waliandaa michezo ya kupigana ya ma gladiators mnapigana hadi mmoja afe!. yule gladiators mwenye nguvu kuliko wote, anakuja kuletwa pale kwenye Colosium (stadium) na kusakiziwa simba watatu wenye njaa ya siku 7, huku watu wamejaa kushuhudia jinsi binadamu anavyoraruwa na simba huku watu wanashangilia!.

Adolf Hitler yeye alikuwa akinyoosha mistari ya jeshi lake kwa risasi za moto, anayepindisha tuu, anakula hapo hapo!. Idi Amini Dada yeye alikuwa anatumia kikosi kinachoitwa "firing squad", lengo ni kuogofya!.

Hivyo wandugu, tusije wote tukawa washangiliaji wa hiki kinachoendelea tukitaraji tutafika mwisho na wote watanyooka, kumbe huu ukawa ndio kwanza ni mwanzo tuu wa makubwa yajayo!.

Naomba kumalizia kwa msisitizo, kuna aina mbili za madikiteta!. Kuna Madikiteta Katili na Masikiteta wazuri!. Mada hii inawazungumzia madikiteta katili!, hivyo nawaomba wachangiaji msije kuchanganya madawa mkaanza kuwadhania watu humu!.

Namalizia kwa swali, jee wote tunaoshagilia hizi character assassination za sasa, ambazo we take them as "the sweet", jee tuko tayari to "swallow the bitter with the sweet" wakati wa vidonge vichungu ukifika, au tutaendelea tuu kuchagua vidoge vitamu ndio tumeze, lakini vichungu tuteme?!.

Nawatakia Jumatatu Njema.

Pasco

Hilo la Adolf Hitler kunyoosha mstari kwenye gwaride kwa risasi za moto ni tetesi tu wala halina ushahidi wa kitaalamu. Ni propaganda zilizotengenezwa na Wayahudi kumchafua kama ambavyo mambo mengi yametengenezwa kuonyesha kuwa Manazi walikuwa ni watu makatili sana kuwahi kutokea duniani.
 
Ila jamani acheni utani kwa nchi yetu tulikokuwa tumefikia......inatakiwa awepo dikteta mzuri na nadhani huyu jamaa kama anareflect hivyo kwenye huo udikteta ila natakiwa aandae mfumo bora asiwe totally dikteta anatakiwa awaandae na wenzie wamuige au wafanye kama anavyofanya.......namuona Majaliwa kama ameshakamata kasi yake sasa wanaenda sambamba
Ngoja twende hivi hivi tutafika!!!
 
Ila jamani acheni utani kwa nchi yetu tulikokuwa tumefikia......inatakiwa awepo dikteta mzuri na nadhani huyu jamaa kama anareflect hivyo kwenye huo udikteta ila natakiwa aandae mfumo bora asiwe totally dikteta anatakiwa awaandae na wenzie wamuige au wafanye kama anavyofanya.......namuona Majaliwa kama ameshakamata kasi yake sasa wanaenda sambamba
Ngoja twende hivi hivi tutafika!!!
Magufuli hana udikteta wowote. Hata mimi huwa natamani sana siku moja kuwa na dikteta lakini siyo kwa demokrasia hii. CCM bado ipo intact kwahiyo Magufuli ataendeleza sera za chama na si vinginevyo. Hizi ngonjera za kufukuza mawaziri ndiyo mnaziita udikteta? Hivi mbona vitu vya kawaida tu.
 
Yote hayo hayana maana yoyote bila katiba bora inayo akisi maoni ya Wananchi.
Katiba bora bila rasilimali watu, bila kupata mtu mwenye uthubutu wa kuisimamia hiyo katiba ni kazi bure.

Tengeneza kwanza watu wenye uwezo, wazalendo, waadilifu ili waisiamie katiba. Nchi hii imekosa waadilifu, waaminifu na wachapa kazi. Endelea tu kuimba "katiba yenye maoni ya wananchi"
 
Magufuli, keep on keeping on. Tulihitaji dikteta, tumepata msimamizi mzuri, hata kama zipo setbacks huo ni ubiadamu tu.
 
Mkuu Pasco bandiko lako si rahisi mtu kulielewa ikiwa atakimbilia itikadi.Jana nilikuwa nimealikwa mahali,kikao kilikuwa na watu kama 50 hivi lakini nilishangaa kila mtu alikuwa akiijadili serekali ya Dr yaweza kutupeleka ambako ndiko siko kabisa.

Zipo dalili za wazi kabisa nchi inaenedeshwa pasipo kufuata sheria bali utashi wa mtu na hii si dalili nzuri hata kidogo.
 
Pasco uko sahihi sana kuhusiana na hoja kuwa Madikteta huwa wanaanza na character assasination, lakini nadhani hauko sahihi kwa mifano uliyotoa. Character assasination haitumii risasi za Moto wala Firing Squad, inavofika level hiyo sio character assasination. Character assasination hutumia siraha kama maneno au kalamu, na vyombo kama magazeti, redio na Tv huweza kutumiwa.

Kwa mfano mfanyakazi mwenzio anaweza akajenga mazingira mbayo yatakufanya usiaminike na mwajiri k.m vile akatengeneza mazingira ya kuwa wewe ni Mwizi na Muongo hivo anakuwa amekuua maana huwezi kuaminika tena kitu kama hicho tunakiita character assasination.

Mwajiri akikufukuza kazi kwa kosa ambalo halijathibitishwa maana yake amekutengenezea mazingira ya kutokuaminiwa na waajiri wengine ili uje uombe kazi nyingine, katika mazingira kama hayo tunaita mwajiri amekuua kihaiba, character assasination.

Sasa Madikiteta huwa waanza kwanza kuwaua kihaiba watu wanaowapinga waonekane hawafai kwenye chama chao au kwenye serikali, watu hao waonekane kuwa sio watu wanaoweza kuaminika. Baada ya hapo hao watu wakirudi kwenye jamii wataitwa wasaliti, wanafiki n.k. na haya tumeyaona Korea, China, Iran, Iraq, Libya wakaitwa wasaliti wa Mapinduzi.

SAS alishindwa Kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2005 baada ya wapinzani wake kumuua kihaiba kwa kuandika makala mbali mbali kwenye magazeti zikichora picha ya upande mbaya wa SAS, Character Assasination
 
Mkuu Pasco bandiko lako si rahisi mtu kulielewa ikiwa atakimbilia itikadi.Jana nilikuwa nimealikwa mahali,kikao kilikuwa na watu kama 50 hivi lakini nilishangaa kila mtu alikuwa akiijadili serekali ya Dr yaweza kutupeleka ambako ndiko siko kabisa.

Zipo dalili za wazi kabisa nchi inaenedeshwa pasipo kufuata sheria bali utashi wa mtu na hii si dalili nzuri hata kidogo.
Mpaka mama lishe wanasema nchi haina mwelekeo.....vurugu,kutukanana,ulevi wa viongozi,uchumi mgumu,kutofata sheria,bunge laivu,kuingilia mahakama....

.
 
Maelezo yako yote yamehitimishwa na paragraph ya tano.

Tanzania ilipofika na mazingira yaliyopo hatuwezi kufika huko unakodhani. Huu ni woga ambao ulitegemewa kwa sababu kinachofanywa na Rais kwa sasa kiko nje ya comfort zone za baadhi ya watu.

Ninafahamu ni wachache sana waliamini kama Rais Magufuli anaweza kumtumbua Kitwanga achilia mbali kumtumbua kwa aina kama ile huku Ikulu ikitoa Press Release yenye paragraph mbili ambazo ni fupi.

Hii imekuwa ni shock hasa ikichuliwa kuna wengine walisha bet na kusema watavua nguo au watatembea uchi kama Kitwanga atafukuzwa kazi.

Watu wanaomfahamu kwa karibu Rais Magufuli hawashangai kwa kile anachokifanya.

Ninakuhakikishia subiri mahakama ya mafisadi ianze utashangaa watakao kamatwa na kushitakiwa.

Hizi unazoziita character assassination itabidi wazizoee na njia ya kuepuka fanya kazi kama mkataba wako unavyotaka au achana na public sector na ingia kwenye private huku ukifuata sheria za nchi.

Kwa sasa kuna watu hali zao kifikra ni mbaya sana kwa sababu hawafahamu hatima yao kutokana na madhambi yao.

Rais Magufuli ni mtu anayechukia sana uonevu na uzembe lakini anaheshimu sana watenda mema kwa jamii hasa ya chini.

Kama kuna watu wanadhani wanaweza kupambana naye ili kumkwamisha ni bora wasahau hilo wazo kwa faida ya freedom zao.
Waangalie watu watatu hawa,Magufuli,Agrey Mwanri na Lyatonga mrema,compare and contrast,anything common amon them? Kuna jambo utagundua tu.
 
ImageUploadedByJamiiForums1463988156.479696.jpg

Kwa wenye uwezo wa kusoma sura za watu. Sisi tuna bahati sana maana inaonyesha kwa sura hii kijana huyu alikuwa na maisha ya "furaha" sana enzi hizo.
Au mie sijui kusoma sura?
 
Magufuli hana udikteta wowote. Hata mimi huwa natamani sana siku moja kuwa na dikteta lakini siyo kwa demokrasia hii. CCM bado ipo intact kwahiyo Magufuli ataendeleza sera za chama na si vinginevyo. Hizi ngonjera za kufukuza mawaziri ndiyo mnaziita udikteta? Hivi mbona vitu vya kawaida tu.
Ya kawaidaa????
Aina hii ya utumbuaji kwa kiasi kikubwa inawadhalilisha watu kwa hiyo ukiiangalia ni aina fulani ya udikteta ulio mwema!!
 
Cha ajabu na hii nchi ni kua ulichoandika hapa ungeandika facebook ambapo kuna jina lako, ungefungwa na makosa ya mtandao ati umemuita Rais dikteta.

Hii nchi inaenda kijinga huo ndio ukweli, na kwazile kiki za mwanzoni na kawaida ya bwana mkubwa kua na speech kali za kumtoa nyoka pangoni watu wamekua kama in compulsion vile hawaoni makosa hata yakifanyika, wao kila kitu anachofanya wanaona ni perfect.
 
Back
Top Bottom