Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Wanabodi,

Hapa simzungumzii mtu yoyote bali nazungumzia hulka za watu wenye tabia za udikiteta katili, kitu kinachoitwa "character assassinations" ndio "modus oparandi" ya madikiteta wote duniani, na huanza kwa kuwa populist kwa kuonyesha heroick actions hivyo kushangiliwa sana kama mashujaa na kupendwa sana na watu!.

Hulka hizo za udikiteta zinatokana na kitu kinachoitwa "deep rooted neurosis" kwa madikiteta hawa kuwa waliteswa sana utotoni!, baadhi yao walikataliwa ndani ya familia, na hii hutokea baba kuhisi mtoto huyo sii wa kwake kwa kumhisi mke alichepuka, mama kamwe hawezi kukiri kuchepuka hata kama ni kweli alichepuka, hivyo baba anakuwa anamtesa sana mtoto, na mama hawezi kuingilia!, mtoto wa aina hiyo anakuwa amekulia katika usongo mkubwa wa mawazo, unaomtia hasira kusoma kwa bidii na huku ana visasi ili kuonyesha mateso hayo ni jambo la kupita tuu, na kweli wengi hufanikiwa, na wakiishafika at the top!, ndipo ile "deep rooted neurosis" ya kumbukumbu ya mateso iliyohifadgiwa kwenye "sub conscious mind" inaibuka na kupelekea kumfanya mtu huyo kuwa katili!, kwa ku inflict pain kwa njia za character assassinations, anaumiza ukiumia yeye ndio anapata furaha!.

Madikiteta wa Roma ya kale, waliandaa michezo ya kupigana ya ma gladiators mnapigana hadi mmoja afe!. yule gladiators mwenye nguvu kuliko wote, anakuja kuletwa pale kwenye Colosium (stadium) na kusakiziwa simba watatu wenye njaa ya siku 7, huku watu wamejaa kushuhudia jinsi binadamu anavyoraruwa na simba huku watu wanashangilia!.

Adolf Hitler yeye alikuwa akinyoosha mistari ya jeshi lake kwa risasi za moto, anayepindisha tuu, anakula hapo hapo!. Idi Amini Dada yeye alikuwa anatumia kikosi kinachoitwa "firing squad", lengo ni kuogofya!.

Hivyo wandugu, tusije wote tukawa washangiliaji wa hiki kinachoendelea tukitaraji tutafika mwisho na wote watanyooka, kumbe huu ukawa ndio kwanza ni mwanzo tuu wa makubwa yajayo!.

Naomba kumalizia kwa msisitizo, kuna aina mbili za madikiteta!. Kuna Madikiteta Katili na Masikiteta wazuri!. Mada hii inawazungumzia madikiteta katili!, hivyo nawaomba wachangiaji msije kuchanganya madawa mkaanza kuwadhania watu humu!.

Namalizia kwa swali, jee wote tunaoshagilia hizi character assassination za sasa, ambazo we take them as "the sweet", jee tuko tayari to "swallow the bitter with the sweet" wakati wa vidonge vichungu ukifika, au tutaendelea tuu kuchagua vidoge vitamu ndio tumeze, lakini vichungu tuteme?!.

Nawatakia Jumatatu Njema.

Pasco
Pasco awamu hii kazi ya upambe kwishney...tafuteni kazi za kufanya la sivyo mtaishia kutoa laana hewa,dua la kuku halimpati mwewe.Mzee wako Lowasa kwa sasa kakata tamaa ile hela aliyokuwa anawapa mumkusanyie makundi ya kumshawishi agombee uraisi zimekata.Pole sana najua unapitia hali ngumu.Buni miradi ya kilimo na ufugaji utatoka tu.
 
Kwa kumtumbua Kitwanga sasa naamini JPM means business.

Tunachokitaka sasa ni

1. Bunge Live
2. Mahakama ya mafisadi
3. Mipango kamambe ya Uchumi
4. Sauti za wananchi kuheshimiwa kwenye chaguzi ( yaliyotokea Zanzibar ni aibu, kamwe yasitokee tena)
Kwani aliyesema bunge lisiwe live ni Nani?
 
Watu mtatunga mashahiri mpk yaishe , mtajifanya wasamalia kutetea mafisadi mpk povu liwatoke , serikali ya Magufuri ni kazi tu hakuna kuremba , ! Chezea kazi yako unatunguliwa hata uwe nani , lazima adabu irudi nchi hii , mafisadi mtalima kwa meno watu wameishajitoa sadaka kuwatumikia wanyonge
 
uko wazi Sana kuelezea uchungu wako "character assassination ". Lakini huna historia ya assassins . Pia huna historia ya victimized characters.
Nchi yetu haijafikia huko kwenye character assassination . The assassins you refer is neither an assassin but an upright personality in malformed personality. Deviant character ,that is what they are! (Majizi, mafisadi, maongo, malevi, Mazinzi etc )
or
Mafisadi kushika hatamu
What do you call this?
Negative attribute
Hayo ni majipu tu .
Yatumbuliwe ili true character ya yule anaye tumbuliwa ionekane.
Kweli yatumbuliwe. Nayo ni:-
1. Lugumi
2. Escrow IPTL
3. Kivuko Chakavu
4. Nyumba za umma
5. Kiwira
6. Richmond Dowans
7. Meremeta
8. Fedha za Barabara Wizara Ujenzi na Tanroads
9. Kuhamisha na kubadili matumizi ya fedha za umma kinyume na sheria kanuni na taratibu za nchi.
10. Kupuuza sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa umma.
11. Kubaka Katiba ya Wananchi (Katiba ya Warioba).

Chama Cha Majipu (CCM) kina Kansa ya Rushwa na Ufisadi.
 
Wanabodi,

Hapa simzungumzii mtu yoyote bali nazungumzia hulka za watu wenye tabia za udikiteta katili, kitu kinachoitwa "character assassinations" ndio "modus oparandi" ya madikiteta wote duniani, na huanza kwa kuwa populist kwa kuonyesha heroick actions hivyo kushangiliwa sana kama mashujaa na kupendwa sana na watu!.

Hulka hizo za udikiteta zinatokana na kitu kinachoitwa "deep rooted neurosis" kwa madikiteta hawa kuwa waliteswa sana utotoni!, baadhi yao walikataliwa ndani ya familia, na hii hutokea baba kuhisi mtoto huyo sii wa kwake kwa kumhisi mke alichepuka, mama kamwe hawezi kukiri kuchepuka hata kama ni kweli alichepuka, hivyo baba anakuwa anamtesa sana mtoto, na mama hawezi kuingilia!, mtoto wa aina hiyo anakuwa amekulia katika usongo mkubwa wa mawazo, unaomtia hasira kusoma kwa bidii na huku ana visasi ili kuonyesha mateso hayo ni jambo la kupita tuu, na kweli wengi hufanikiwa, na wakiishafika at the top!, ndipo ile "deep rooted neurosis" ya kumbukumbu ya mateso iliyohifadgiwa kwenye "sub conscious mind" inaibuka na kupelekea kumfanya mtu huyo kuwa katili!, kwa ku inflict pain kwa njia za character assassinations, anaumiza ukiumia yeye ndio anapata furaha!.

Madikiteta wa Roma ya kale, waliandaa michezo ya kupigana ya ma gladiators mnapigana hadi mmoja afe!. yule gladiators mwenye nguvu kuliko wote, anakuja kuletwa pale kwenye Colosium (stadium) na kusakiziwa simba watatu wenye njaa ya siku 7, huku watu wamejaa kushuhudia jinsi binadamu anavyoraruwa na simba huku watu wanashangilia!.

Adolf Hitler yeye alikuwa akinyoosha mistari ya jeshi lake kwa risasi za moto, anayepindisha tuu, anakula hapo hapo!. Idi Amini Dada yeye alikuwa anatumia kikosi kinachoitwa "firing squad", lengo ni kuogofya!.

Hivyo wandugu, tusije wote tukawa washangiliaji wa hiki kinachoendelea tukitaraji tutafika mwisho na wote watanyooka, kumbe huu ukawa ndio kwanza ni mwanzo tuu wa makubwa yajayo!.

Naomba kumalizia kwa msisitizo, kuna aina mbili za madikiteta!. Kuna Madikiteta Katili na Masikiteta wazuri!. Mada hii inawazungumzia madikiteta katili!, hivyo nawaomba wachangiaji msije kuchanganya madawa mkaanza kuwadhania watu humu!.

Namalizia kwa swali, jee wote tunaoshagilia hizi character assassination za sasa, ambazo we take them as "the sweet", jee tuko tayari to "swallow the bitter with the sweet" wakati wa vidonge vichungu ukifika, au tutaendelea tuu kuchagua vidoge vitamu ndio tumeze, lakini vichungu tuteme?!.

Nawatakia Jumatatu Njema.

Pasco
Mimi dikteta yeyote kwangu mimi ni Sawa as long ananyoosha mambo yanakwwnda Okay ni Sawa tu. Maana mambo YALIKUWA mabaya
 
na bado alisema ni bora akafukuza watu elfu 50 ili watu milion 50 wanufaike na nchi yao. kwa hiyo hata 1/8 bado. hao wanajifia kwa madhambi yao
 
Yote hayo hayana maana yoyote bila katiba bora inayo akisi maoni ya Wananchi.
katiba bora ndio nini. katiba bora imekuwepo tangu uhuru na imekuwa ikiboreshwa mwaka hadi mwaka kulingana na matakwa ya wadau. tatizo ni yule anayesimamia katiba anamaanisha au ? upinzani umekuwepo bungeni tangu mwaka 1992 nini umefanya kuhusiana na katiba. umeshindwa kujenga hoja za msingi ili baadhi ya vipengele muhimu vibadilishwe basi ukiwa kama utaratibu tuliouzoea. sawa katiba mpya inatoa mwelekeo mzuri wa jumla wa namna ya kuendesha nchi lakini pia inategemea anayeongoza nchi ni wa aina gani. mi nadhani katiba iliyopo pia ni nzuri kwa sehemu kubwa lakini sio vipengele vyote. ni wajibu wa wabunge sasa kuchambua vipengele kimoja baada ya kingine kufanyia amendment kama ambavyo imekuwa ikifanyika huko nyuma. cha msingi tujenge nchi sasa tusipoteze muda kuzungumza mambo ya katiba mpya. kiongozi wa sasa ni zaidi ya katiba mpya. chukueni mifano ya nchi zilizopiga hatua kama China. najiuliza hivi hawa maendeleo yao yaliletwa na katiba mpya au ni sheria kali tu walizojiwekea kuongoza nchi.
 
Pasco ana msongo wa Mawazo baada ya Jamaa yake kuTumbuliwa Mwaka Jana....

Anyway!..
Tulikuwa tunamtaka raidi dikteta tumeshampata.... Tulimsema sana JK kuwa ni dhaifu.
 
Samahani, nilichogundua na kwa mtu yeyote mwenye fikra pevu ni unafiki uliorembwa na kujificha katika uzi wako. Para ya mwisho inai-cancel para ya kwanza na rangi zako zinadhihirika waziwazi. Licha ya kipaji maridhawa cha uandishi sina shaka unatumiwa na kikundi cha watu kama character assasin kwa malipo. Unayemlenga ni dhahiri. Take care, wengi wana uchungu na walikotoka na sasa wanaona mwanga japo kidogo at the end of the tunnel.

Tabia hii ya kumwatack MTU personal anapolaza hoja hapa janvini inadumaza sana uwezo wa watu kudadavua mambo.
Wengi inaonekana bado mna mawenge ya kampeni.
Rai yangu tuwe watulivu hata kama anayezungumziwa ni mtu umpendae sana.
Watanzania hawana MTU wa kudumu ila wana Taifa la kudumu
Mleta Uzi ni great thinker. Tafakuri jadidi inahitajika.
Vilevile Historia ni mwalimu.
 
Na madikteta wote Duniani huwa wanaamini ni wao tu ndo wenye uwezo wa kuongoza wengine. Hawashauriwi na maamuzi yao ni sheria kamili..! Na kwa vile utawala wa dikteta yeyote hujenga hofu kwa jamii,kundi kubwa hujikuta linamshangilia dikteta.
 
wadada wa mjini wanasema upele umempata mkunaji......same to tz,watu waliomba tumpate kiongozi mwenye kuthubutu haya sasa.....
 
Kweli yatumbuliwe. Nayo ni:-
1. Lugumi
2. Escrow IPTL
3. Kivuko Chakavu
4. Nyumba za umma
5. Kiwira
6. Richmond Dowans
7. Meremeta
8. Fedha za Barabara Wizara Ujenzi na Tanroads
9. Kuhamisha na kubadili matumizi ya fedha za umma kinyume na sheria kanuni na taratibu za nchi.
10. Kupuuza sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa umma.
11. Kubaka Katiba ya Wananchi (Katiba ya Warioba).

Chama Cha Majipu (CCM) kina Kansa ya Rushwa na Ufisadi.

Safi
 
Mie nahofia sana utawala huu, ni hatari sana kuufikiri kwakina.
Hauna msingi imara wa kulinda usalama wa taifa letu.
Uimala wa kuhimili misukosuko ya kiutawala. Jambo ambalo huhitaji busara, hekima, subira,kusikiliza ushauli na uvumilivu. Vyote hivyo kwenye awamu hii havipo

Ajali za kiutawala hutokea Siku zote kwa kukosa vitu muhimu kama nilivyovitaja hapo juu.

Hebu fikili kama moja kati ya haya moja wapo litatokea;

1, jaribio la kweli na lililoshindwa la kupindua nchi.

2. Jaribio la kweli la kumdhulu mkuu wa nchi na lililoshindwa

3.Tishio la kweli la kanchi Jilani has a katika migogoro ya mipaka.

4.Maandamano makubwa ya umma yaliyishilikisha taifa lote.

Mimi naamini uwezo wautawala huu kuyahimili haya ni MDOGO sana.
Hii inatokana na uendeshaji wa nchi kwa mfumo wa jeshi la MTU mmoja.
Hivyo uwezekano wa taifa letu kupata ajali na sintofahamu ni mkubwa zaidi kuliko wakati wowote.
Nawasilisha.
 
Hapo kwa Hitler umedanganya pasco hakuna ushahidi wowote wa Hitler kumpiga mtu yeyote risasi kwa mikono yake!hata wayahud waliouawa ma manazi
 
Back
Top Bottom