Afrocentric view
JF-Expert Member
- Jun 19, 2022
- 1,373
- 2,267
Bonobo!
Canis Lupus Familiaris ndiyo jina la hii specie tunayoijua na kuipenda..Almaaruf kama Mbwa!!
Wengi mkiulizwa mbwa wametokea wapi kwa haraka haraka mtasema waliumbwa na Mungu.
Lakini kama maswali mengi kwenye hii dunia, majibu yake huwa sio rahisi kihivyo. Leo tuingie deep zaidi ya hapo tujue hawa mbwa wametokea wapi hasa. Chukua popcorn kabisa, it's history time.
Miaka laki 2 iliyopita, binadamu (Homo sapiens) alianza kuwepo huko Africa,(unaweza kufuatilia pia Chanzo halisi cha binadamu (Origins of mankind))
Miaka laki 1 mpaka 50,000 iliyopita hawa binadamu wa kale wakaamua kuondoka Africa na kwenda Ulaya na Asia kutafuta maisha bora.
Kwakuwa kipindi hiko binadamu kazi kuu waliyokuwa wanaifanya ilikuwa kuwinda na kukusanya matunda (Hawakuwa na kazi kama madaktari, Mainjinia, Wanamziki na maslay queens)
Walipofika Asia (hasahasa Siberia) walikutana na adui mkubwa sana ambaye aliwakwamisha katika kazi yao kuu ya uwindaji..Naye si mwingine bali ni..........(drumroll please🥁).........Canis Lupus (Grey wolf) kwa kizaramo anaitwa Mbwa mwitu
Hawa wanyama waliwasumbua sana watu. na pia, watu waliwasumbua sana hawa mbwa mwitu..Tuwaite Wolves.
Hawa wolves waliwachukia sana binadamu maana walileta competition kwenye kutafuta chakula. Wolves waliona Hawa viumbe wapya waliokuja huku Siberia walikuwa wanauwezo mkubwa sana wa kuwinda kwa kuweka mitego na kushirikiana kwa hali ya juu kuliko wao mbwa mwitu(Wolves).
Kwa msiojua, mbwa mwitu pia huwa wanawinda kwa kushirikiana na kutengeneza plan za kumshambulia/kumvizia au kumkibiza adui mpaka achoke. ni ngumu sana kwa Mbwa mwitu kuwinda peke yake.
Wale mbwa mwitu waliofukuzwa kwenye ukoo (Packs) kutokan na tabia zao mbovu walikuwa wanaishi kwa kuwinda vimnyama vidogovidogo. Lakini kutokana na ujio wa huyu kiumbe mpya (binadamu), competition ya chakula ikawa kubwa, hata hawa wanyama wadogo wadogo ikawa ngumu kupatikana tena.
Wale mbwa mwitu waliofukuzwa na ukoo wakawa wanapata tabu kupata chakula, wakawa wanaishi kwa kutafuta makombo. Kwakuwa Binadamu walikuwa wanaishi kwenye makambi na wanakula nyama na kutupa mifupa (since hawana meno makali ya kutafuna mifupa.)
Hawa mbwa mwitu wasio na packs wakawa wanawavizia binadamu wakitupa makombo wao wanakula. Na hapo ndo ikawa mwanzo wa interaction kati ya binadamu na wolves.
katika wale wolves waliokuwa wanakuja kutafuta makombo, Binadamu wakawa wanachagua wale wasio tishio kwao (wapole, wenye miili midogo, watiifu) na wakagundua kuwa wanaweza kuwatumia kwa faida yao.
Wakaanza kugundua kuwa hawa wolves wanaweza kutumiwa kama walinzi akija Adui wanawahi kumsikia, kwahyo binadamu akaamua kuwa anakaa na hawa wolves ili apate kuzitumia faida zake, with time wakaanza kugundua faida nyingi za hawa wolves ikiwemo kunusa mbali na hata kujua wapi kuna wanyama wa kuwinda, Kupambana na dubu na wanyama wengine wakali, kuchunga mifugo nk.
Watu wakaanza kuwa wanachukua wale wolves wenye tabia na sifa wanazotaka na kuanza kuwabreed wao kwa wao. Hiki kitendo cha kuchagua mbegu za kufuga/kulima zenye sifa unazotaka na kuzitenga ili kupata matokeo unayotaka inaitwa Artificial selection.
Kwa hiyo kati ya miaka 30,000-23,000 iliyopita.. watu walikuwa wanachukua wolves na kuchagua sifa wanazopenda.
Watoto wakizaliwa na hizo sifa zinazotafutwa (Za kimbwa) ndiyo wanafugwa na kuwa bred tena na tena... Hivyo wolves wakawa wanabadilika, na wakibadilika wanachukuliwa tena wale wenye sifa zinazotafutwa mpaka tukafikia kupata mnyama anayeitwa leo Mbwa.
Lakini hizi breed tofauti tofauti za mbwa tunazojua leo zimetengenezwa less than miaka 400 iliyopita.
Hiyo hiyo formula ya artificial selection watu waliitumia (Na bado wanaendelea kuitumia) kutengeneza breed tofuti za mbwa wenye sifa tofauti wanazozitaka.
Unataka mbwa mwenye mbio? Chukua wale wenye miguu mirefu uwabreed wao kwa wao na watoto watakaozaliwa unawachagua wale wenye mbio tu na kuwafuga.
Unataka mbwa mwenye nguvu?? Tafuta wenye sifa hizo na kuwabreed pamoja na watoto wasio na nguvu unawatupa pembeni. Unaendelea na wale wenye nguvu
Je, untaka mbwa wa kukaa naye na kumchezea?
Ukitaka mbwa mwenye sifa mbili labda Awe na nguvu na Manyoya mengi, Unachukua mbwa wawili wenye sifa Hizo na kuwabreed pamoja huku ukichukua wale watoto wenye sifa unazotaka na kuwabreed hao tu.
Mpaka leo mbwa na Wolves wanaweza kuzaa pamoja lakini yule mtoto hawezi kuzaa.
Ule mstari unaowaunganisha kama specie moja umeshakatika.
Ipo siku mstari unaowaunganisha German shepherd na Bulldog unaweza kukatika vikaonekana kama viumbe viwili tofauti..
Hii artificial selection haijatuletea Mbwa tu, imetuletea pia Ndizi, Matikiti, Maparachichi, Kuku wa kisasa, Ng'ombe wa kisasa Nk. Nk.