Wazo Fyatu: Ukali wa Mbwa Humtegemea Mwenye Mbwa...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Na. M. M. Mwanakijiji

Unaweza ukakuta mbwa asiyebweka; unaweza kukuta mbwa anayebwekabweka tu lakini hang'ati. Kuna mbwa mwingine ukimtazama tu unajua huyu "shughuli". Na unaweza kukuta mbwa wanaopenda kucheza cheza; hawafoki, hawabweki, wapo wapo tu ila wanaona raha kuita "puppy, puppy"!

Siyo kila mbwa anaweza kubweka; na siyo kila mbwa anaweza kuwa wa kulinda. Wengine wapo kwa ajili ya mapambo tu kama tule tu 'chiuhahua'. Vimbwa vile vina makeke mengine lakini ndiyo hivyo ni vya kupet pet tu. Huwezi kulinda nyumba na hivi vijibwa. Kuna vingine ni vya mashindano tu; yaani unavipendezesha tu ilimradi watu waseme "she is so cuuuteeee".

1668015619456.png

(Chiuhauha)

Na wapo mbwa wengine kazi yao ni kuwinda si kulinda; kuna hao wanaitwa 'greyhounds'. Wanakimbia hawa, wanafukuza lakini mara nyingi hawali! Watakamata kasungura watakusubiri ukawahi! Wao wanakimbiza hata karatasi kwenye upepo.. alimradi waoneshe uwezo wao wa kukimbia!

Lakini inasemekana ukitaka ulinzi mzuri na mbwa anayetii na kufuata amri na akawa mzuri hata nyumbani hakuna anayependwa zaidi kama German Shepherd au mchanganyiko wake. Na wengine wanawapenda wale Doberman. Haya bana ukikutana nayo lazima ujibane ukitembea!

1668015486502.png

(Doberman Pinscher)

1668015549942.png

(German Shepherd)
Lakini vyovyote vile ukali wa mbwa humtegemea mwenye mbwa. Kama mbwa analelewa kwa kuruhusiwa kuchezewa chezewa tu, kushikwa shikwa tu hata kama ni mbwa kwa asili ni mkali anaweza kuwa kama pets wengine tu! Sasa ukifika mahali ukakuta mtu anasema ana mbwa mlinzi halafu watu wanakuja na kuiba kila kukicha na yeye anajisifia mbwa aliyenaye ni mzuri kwa vile anaweza kufoka tu basi ujiulize.

Ndio maana hawa FFU na mbwa wao wale; akimwambia "kamata".. lazima amuachie! hawezi kumwambia kamata halafu akaendelea kumshika kwani na yeye ataburuzwa!

Somo la leo: Ukali wa Mwenye Mbwa humtegemea Mwenye Mbwa.... kama mbwa hang'ati, hafoki, hapigi mkwara hata kuja hadi getini tu... watu wakaogopa.. tatizo yumkini si mbwa.... tatizo ni .....

a. Mbwa
b. Kola ya Mbwa
c. Chakula cha Mbwa
d. Mwenye Mbwa
z. Magufuli.
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Somo la leo: Ukali wa Mwenye Mbwa humtegemea Mwenye Mbwa.... kama mbwa hang'ati, hafoki, hapigi mkwara hata kuja hadi getini tu... watu wakaogopa.. tatizo yumkini si mbwa.... tatizo ni .....
Mkuu Mzee Mwanakijiji, its nice to hear from you, it has been a long, long time!, Welcome back to JF baada ya likizo!. Kule nyuma niliwahi zungumza jinsi barking dogs seldom bite!. 2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite", Tusiishie Kubweka Tu, Tung'ate!
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom