Chanzo halisi cha binadamu (Origins of mankind)

Afrocentric view

JF-Expert Member
Jun 19, 2022
1,373
2,267
Tsup! Leo tuzamishe kidole gumba kwenye bahari -bahari ambayo ni hii mada ihusuyo chanzo halisi cha binadamu.

Hii story (History😅) ni very complicated na ndefu ila nataka niandike kwa ufupi sana nisije nikajaza page 200, so without further'a do, let's dive into it.

Creation theory
Kabla ya 1800's watu wengi waliamini katika creation theory (special creation) ambayo waliamini kuna Mungu aliumba kila kitu ulimwenguni kama kilivyo sasa kwa siku saba tu. Yani aliumba binadamu akiwa kama binadamu wa sasa na wanyama wote wakiwa kama walivyo sasa. Pia hii imani ya uumbaji iliambatana na imani ya new Earth, yani ulimwengu ni mchanga, kwamba Mungu ameumba dunia miaka michache iliyopita (roughly 6000 yrs ago) akaumba na binadamu na viumbe wote kwa pamoja.

Johann Friedrich Blumenbach
Miaka ya late 1870's to early 1880's huyu mjerumani Blumenbach ndio alikuwa mtu wa kwanza kufuatilia kisayansi chanzo cha binadamu na kupitia kazi zake anatambulika kama founder wa Zoology na anthropology.

JF_Blumenbach.jpg

Blumenbach Alichukua mafuvu ya races mbalimbali na akaanza kuya'study kwa kufuatilia tofauti zake, kwa kuangalia shape ya vichwa vya mafuvu ya watu mbalimbali duniani. Aligawanya binadamu katika race 5 ambazo ni Caucasian(wazungu+ waarabu +wapersians), Mongolian(Watu wa Asia ya kati na mashariki kama wachina, Wajapan nk.), Malayan (watu wa asia ya kusini na visiwani kama philipino, indonesia, malaysia nk.)American(wale native amercans kama red indians), Ethiopian(Negroids, watu weusi, African, sisi)
Blumenbach aliamini katika story ya creation kwenye biblia, kwamba Mungu aliumba Adam na Eva wakiwa kama caucasians na waliishi pale mesopotamia( Iraq )na uzao wakwanza wa binadamu ulikuwa hapo mpaka pale ambapo waliamua kujenga mnara wa babeli wakatanywa kwenye uso wa dunia na kutengeneza hizi races zote zilizopo sasaivi(Monogenism)..Kadri walivyoenda mbali kutoka Iraq ndipo walizidi kubadilika kutokana na mazingira, magonjwa na tabia.Mfano Waafrika wakawa weusi kwasababu ya joto, mongolians wakawa na sifa zile kwasababu ya baridi nk. Nk.

Lakini ukiangalia fuvu la caucasian lipo symetrical kuliko yote, kwahyo aliamini mungu ndio aliumba binadamu akiwa caucasian.

IMG_20221114_234329.jpg


Samuel G. Morton
Huyu mmarekani alikuja kutumia Idea za blumenbach kupima ukubwa wa ubongo wa kila race kati ya hizo tano na akasema caucasian ndio wanaongoza kuwa na ubongo mkubwa na Ethiopians/Negros ndio wa mwisho.katika kitabu chake miaka ya 1830's Akahitimisha kuwa binadamu walitokea independently katika maeneo mbalimbali ya dunia (polygenism) na kuleta hizi races tunazoziona leo. Na wenye ubongo mkubwa ndio walio intelligent hivyo haiwezekani kubadilika.

Screenshot_20221115_000343.jpg


Kwahyo mpaka hapo ilitokea debate kati ya monogenism Vs polygenism ipi ni sahihi?
Monogenism:Imani kuwa race zote na watu wote duniani tumetokana na chanzo kimoja (in this case kwa Adam na Hawa)

Polygenism:Imani kuwa binadamu tumetokana na vyanzo mbalimbali katika maeneo mbalimbali

Darwin theory of evolution
Mwaka 1859, muingereza Charles Darwin alichapisha kitabu chake 'on the origin of species' ambapo alielezea theory yake ya evolution. Alisema viumbe wote duniani ni ndugu, wametokana na chanzo kimoja ila kutokana na mazingira na ushindani basi kukafanya viumbe wabadilike kuendana na mazingira hivyo husababisha kutokea kwa specie mbalimbali. Kwahyo Darwin aliiprove Monogenism ila sio ile ya Adam na Eva. ikatambulika kuwa binadamu wote tulikuwa na chanzo kimoja.

Lakini kwasababu evolution ni very slow process, haiwezi kuwa tumetoka kwa Adam na Eva miaka 6000 iliyopita ikabidi watabiri miaka malaki kadhaa binadamu alitokea sehemu fulani na kusambaa dunia nzima.

images-37.jpeg


Out of Africa theory
Darwin baada ya kuwa'study apes(tumbili, sokwe, nyani) wa Africa alihitimisha kuwa binadamu tumetokea Africa, Alisema kuwa huenda miaka ya zamani binadamu na hawa apes walikuwa na baba mmoja ambapo walievolve na kutuleta sisi.

Lakini kipindi Darwin anasema hayo hakukuwa na sayansi ya archeology (ya kufukua mafuvu ya kale na kuyapima umri) wala Genetics.

Baadae archeologists Kina dr. Leakey na wengine waligundua kuwa kweli binadamu wa kale waliishi East Africa around miaka laki 2 iliyopita. Na pia kupitia genetics walithibitisha kuwa sisi na hawa apes tulikuwa kitu kimoja takibran miaka million 7 iliyopita.

Kwahyo hii out of africa theory inasema, miaka laki2 iliyopita binadamu wa sasa(homo sapiens) alianza kuwepo hapa East Africa, na miaka 60,000 iliyopita akatoka Africa na kuitawala dunia na ndipo hizi races tofauti zikatokea.

images-38.jpeg

Pan African theory
Hii ni very recent, wanasayansi wamegundua kuwa kumbe sio East Africa tu bali ni karibia Africa nzima ndipo binadamu alipotokea, maana kuna mafuvu yamepatikana North Africa, West Africa na South Africa yanayoonesha kuwa binadamu wa kale zaidi (homo habilis, Naledi nk.) walikuwepo huko na walichangamana ili kumpata huyu binadamu wa leo (homo sapiens).

Binadamu wa aina nyingine
Kupitia Archaeology, wanasayansi wamekuja kugundua kumbe kulikuwa na binadamu wa aina nyingine(hominids) ambao sio homo sapiens. Tena inaonekana hata miaka 70, 000 tu iliyopita kulikuwa na species za binadamu zaidi ya 7 hapa duniani. Ntataja za muhimu.

Neanderthals: hawa wamegundulika walikuwepo sanasana Ulaya na waliishi kati ya miaka laki 7 mpaka 60,000 iliyopita. binadamu wote (kasoro waafrika) wanaonesha kuwa na vinasaba vya DNA ya Neanderthals.
images-34.jpeg

Denisovans: Hawa waligundulika huko Serbia maeneo ya Asia huko na waliishi around miaka 30,000 mpaka 14500 iliyopita.

Homo fluorensis: Hawa walikuwepo huko indonesia mpaka binadamu walipoenda huko miaka 50,000 iliyopita na kuwafanya wapotee
images-36.jpeg

Homo Naledi:Hawa wamegundulika south Africa na inaonekana waliishi miaka 335,000-230, 000 iliyopita
images-35.jpeg

Wapo homo wengine wengi.


The big picture (My conclusion)
Kupitia ushahidi mbalimbali wa mafuvu, genetics, molecular biology, Paleontology nk. Tunaweza ku'summarize hii story kwa kifupi hivi.
Binadamu tulianzia hapa Africa kwa staili hii (still debatable)

Miaka Millioni 7 iliyopita: Binadamu (Homo) na sokwe(chimpanzee) wakaachana na kukatokea homo habilis, homo erectus na homobwengine

Miaka million 2 iliyopita: Homo habilis alifanikiwa kutoka Africa na kwenda ulaya na Asia
Miaka laki 7 iliyopita: Huko ulaya akatokea Neanderthal
Miaka laki 3 iliyopita: Baada ya homo wengi kuungana(sex) kwa muda mrefu hapa Africa ndio homo sapiens (sisi) akaanza kupatikana...lakini pia homo wengine waliendelea kutoka nje ya Africa.

Miaka laki 2 iliyopita: tukaanza kutumia tools mbalimbali ambazo zimegundulika Olduvai gorge na sehem zingine za Africa. (Muda huo huo kule Asia na Ulaya wale homo habilis wameevolve kutengeneza Denisovans, Homo fluorensis na wengine)

Miaka 60,000 iliyopita: Homo sapiens (sisi) tukaanza kutoka Africa na kwenda ulaya na Asia ambapo hao waliotoka walikutana na homo wengine kina Neandarthals, Denisovans na wengine na wakafanya nao ngono wakazaa wazungu, wachina na race zingine..Huku sisi waafrica tukabaki hapahapa.

Miaka 6,000 iliyopita: (kipindi hiki hawa Homo wengine wote wameshapotea duniani) Binadamu (homo sapiens) wakawa wameanza kupata akili na kutengeneza miji, Lugha,maandishi, Art, Music, agriculture na ndipo tukaanza kupata Dini (Hindu, Zorastrianism,) na ndipo ukawa mwanzo wa kumbukumbu zote tulizonazo leo kuhusu historia ya nchi, empires, tawala na falme mbalimbali kwasababu hapo ndipo tulipogundua kutunza kumbukumbu kupitia maandishi na lugha.

Miaka 4000 mpaka 1400 iliyopita: Uyahudi, ukristo na uislam ukaanza ambao ukainfluence historia yote iliyopita na kutufanya tuamini sisi tumetengenezwa juzijuzi tu (miaka 6000 iliyopita) kwa nguvu kutoka angani isiyoonekana.

(oh, by the way..zile data za Samuel Morton kuhusu ukubwa wa ubongo na akili zilikuja kugundulika kuwa zilipikwa. Huyu jamaa alikuwa racist hivyo alipika data ili ziendane na ideology yake, hivyo endeleeni kuwa na imani na Mama)
IMG_20221114_234329.jpg
Screenshot_20221115_000343.jpg
images-34.jpeg
images-35.jpeg
images-36.jpeg
IMG_20221114_234329.jpg
Screenshot_20221115_000343.jpg
Screenshot_20221115_000343.jpg
images-37.jpeg
images-34.jpeg
images-35.jpeg
images-36.jpeg
images-38.jpeg
JF_Blumenbach.jpg
 
Yawezekana sio Morton tu aliyepika data peke yake labda na wenzake pia walitupikia data ambazo sio sahihi
Yeah racist bias ilikuwa kubwa kipindi kada ya Archeology inaanza.
ila Blumenbach pamoja na kuwa wa kwanza kuziclassify hizi race 5 hakuamini kama waafrika ni inferior.
Lakini walikuja watu wengi wakatumia kazi zake kujustify kuwa wazungu ni superior race.

Btw, ilishagundulika kuwa ukubwa wa ubongo sio ukubwa wa intelligene.
Saivi kinachomata ni ile brain to body size ratio.
Ukiwa na mwili mkubwa na ubongo unakuwa mkubwa kuukidhi.
Kwahyo ukiaccount hiyo factor ya Brain to body size ratio...race zote zinakuwa kama zinarange the same.
 
Mkuu hivi haiwezekani kuwa common ancestor wa sisi na Neanderthals alikuwa nje ya Afrika? Halafu baadae akarudi Africa, watoto waliobaki Ulaya wakawa Neanderthals na walionde Africa wakawa homo sapiens?
Yes inawezekana pia...lakini hatujui common ancestor wetu na Neanderthals aliishi wapi, bado hatuna evidence za kutosha, ila currently imani ni aliishi Africa. ila inaweza kuwa sehemu yoyote duniani.
Consensus ni aliishi Africa, watoto wake kina Neanderthals waliwahi kutoka na kwenda Ulaya na baadae wajukuu kina Homo sapiens nao wakatoka na kwenda ulaya kukutana na hawa Neandethals.
 
Yes inawezekana pia...lakini hatujui common ancestor wetu na Neanderthals aliishi wapi, bado hatuna evidence za kutosha, ila currently imani ni aliishi Africa. ila inaweza kuwa sehemu yoyote duniani.
Consensus ni aliishi Africa, watoto wake kina Neanderthals waliwahi kutoka na kwenda Ulaya na baadae wajukuu kina Homo sapiens nao wakatoka na kwenda ulaya kukutana na hawa Neandethals.
Waliweza vipi kusafiri kwenda huko ulaya na mabara mengine ilhali kipijdi iko tec ilikua chini sana mkuu??
 
Waliweza vipi kusafiri kwenda huko ulaya na mabara mengine ilhali kipijdi iko tec ilikua chini sana mkuu??
Walitembea tu mkuu. Halafu utambue sio kwamba tunaposema walisafiri hatumaanishi ilikuwa safari ya siku moja au kizazi kimoja. Inaweza kuchukua miaka hata maelfu. Yani wewe na familia mnaenda kuishi kenya, Watoto wanenda kuishi somalia, wajukuu wanasogea mpaka Ethiopia, vitukuu wanafika egypt na kadhalika na kadhalika.

Kumbuka hali ya hewa ya kipindi hiko sio kama ya leo.
Sahara hapo zamani ilikuwa rainforest hakukuwa na jangwa ilikuwa ni mapori tu, hivyo walisafiri bila shida. Afrika, ulaya mpaka Asia zimeungana (kumbuka hata hii suez canal ilijengwa recently tu) Kwahyo walivuka mpaka ulaya na Asia bila shida ya kuvuka maji.
Labda swali ni Australia walifikaje?
Ukumbuke kuna kipindi ilikuwa Ice age ambapo baridi lilikuwa kali sana mpaka maeneo ya bahari yaliganda, na maji yalishuka sana level (sealevel ilikuwa chini sana) almost mita 400 chini ya hii ya leo, kwahyo kuna visiwa kama Philipines, indonesia havikuwa visiwa bali ilikuwa nchi kavu tu imeungana (hakukuwa na maji) yani ilikuwa land imeungana mpaka huko Australia.
main-qimg-c1c007c6244cbaf0966970c61ac22674-lq.jpeg

Kwahyo mkuu homo wa zamani walivuka tu bila shida.
Lakini recently around 50,000 years ago, homo sapiens (binadamu) walivuka mpaka Australia kwa kutumia mitumbwi maana Homo sapiens ni mnyama mwenye akili na inaaminika walivuka kwa mitumbwi.

Hata sasa joto la dunia linaongezeka kwasababu ya global warming na kussbabisha barafu ya antarctic kuyeyuka na usawa wa bahari unazidi kuongezeka...Usije kushangaa baada ya miaka 30000 ijayo Australia isiwepo, ikawa imefunikwa na bahari na hata Hapa Africa baadhi ya nchi zilizo karibu na bahari zikapungua ukubwa. Unakuta bahari imefika dodoma.
 
Kumbe watu wameanza kuzamia mtoni kitambo tu kutoka Africa
Kusepa bongo kumbe ni utamaduni tu wa toka kitambo apa nikuzamia ulaya tu haya mambo hayajaanza juzi kumbe
😂😂😂yameanza miaka millioni 2 iliyopita. Hakuna nchi ya mtu hapa duniani...Kwahyo hata wanavyopigania mipaka Urusi sijui Ukraine ni ujinga tu.
Miaka ijayo hakutakuwa na nchi inaitwa Urusi wala ukraine kwenye ramani na huenda sis sote binadamu wa leo tukawa tumeshasahaulika kama hata tuliwahi kuwepo...Kama tulivyosahau binadamu wengine kama Neanderthals.
 
Yes inawezekana pia...lakini hatujui common ancestor wetu na Neanderthals aliishi wapi, bado hatuna evidence za kutosha, ila currently imani ni aliishi Africa. ila inaweza kuwa sehemu yoyote duniani.
Consensus ni aliishi Africa, watoto wake kina Neanderthals waliwahi kutoka na kwenda Ulaya na baadae wajukuu kina Homo sapiens nao wakatoka na kwenda ulaya kukutana na hawa Neandethals.
Hivi hawa Neanderthals, sio kwamba walipochangamana na homo sapiens ndio kukapatikana hizi race za wazungu wenye akili?? Mbona sisi Africa bado sana hata kiuwezo wa kufikiria?🤣🤣
Tunawaza ngono tu
 
Hizi hadithi za mwanzo wa binadamu zipo nyiiingi kiasi kwamba naamini baba na mama ndio waumbaji wangu kwa mifano hai kua na mimi kuna nilio wa umba! Inshort wale ndio Mungu wa pili hapa duniani na mimi ni Mungu wa pili kwa nilio waumba Bhasi.!

Hayo maswala ya nyani sijui ngedere watajuana nayo wenyewe! Nimemaliza
 
Hizi hadithi za mwanzo wa binadamu zipo nyiiingi kiasi kwamba naamini baba na mama ndio waumbaji wangu kwa mifano hai kua na mimi kuna nilio wa umba! Inshort wale ndio Mungu wa pili hapa duniani na mimi ni Mungu wa pili kwa nilio waumba Bhasi.!

Hayo maswala ya nyani sijui ngedere watajuana nayo wenyewe! Nimemaliza
Usifuate hadithi...fuata ushahidi unapokupeleka. Hizi sio hadithi by the way kama za kwenye biblia.
 
Back
Top Bottom