Changamoto za kuwa uchumi wa kati ni maumivu ya kodi kuwa juu

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Wakati tunashangilia kuingia Uchumi wa Kati basi ujue Tulikuwa tunashangilia yafuatayo;

1.Nchi kuhama kutoka kupewa mikopo nafuu na ya mda mrefu na kukopeshwa mikopo ya Kibiashara.

2.Kukoma au Kupungua kwa misaada ya wahisani.kama misaada ya kibajeti nk

3.Kuanza kujitegemea kwa kila kitu.Sasa Ili ujitegemee manake utafute vyanzo vipya vya mapato.

Hizo ni baadhi tuu ya faida ambazo kinyume chake ni hasara, yaani ukishakuwa mkubwa lazima ukome kulelewa nyumbani.

Sasa ongezeko la kodi nk ni matokeo ya Hali hii, unfortunately tuna serikali ambayo inashindwa kuwaambia watu ukweli kwamba vya bure havipo tena lazima kufunga mikanda kujikwamua wenyewe.

Hapa Sasa ukiwa na Serikali inayotaka kufurahisha kila mtu ndio mwishowe nchi itajikita imekopa parefu mzigo wa madeni mkubwa na uchumi unaanza kuyumba.

Kwa Nchi yetu ilipofikia kodi za Juu hazitakwepeka tena na mikopo haitakwepeka ila tusipokuwa makini na mikopo tutakuja kujuta,unakopa kibiashara unawekesa sgr Mwanza mwisho wa siku hakuna tija afu tunaanza kupandishiana kodi za kulipa.

Mfano wangu unamaanisha lazima mikopo iwekezwe kwenye sekta zenye tija tuu ambazo zitakuza uchumi kwa haraka.

Kwa maelezo zaidi ya haya niliyoandika someni hotuba ya bajeti/Hali ya Uchumi 2021/2022 👇👇

Screenshot_20210807-075127.png


Screenshot_20210807-075210.png
 
Kwa hiyo tunatakiwa kuvumilia hatuna namna lazima tugharamie miradi yetu kwa kodi za jasho letu.
 
CCM walivyojikausha huwezi kuamini kuwa ndio walikua wanashanga
Walitakiwa wawaeleze wananchi hasara na faida Ili hata tukipandishiwa kodi tuulize inaenda kufanya kitu gani, maana hii nchi kwenye mind za watu kumejengeka misaada sasa usipowaeleza wanajua ni upigaji.

Ndio maana watakwambia mbona miaka mingine haikuwa hivi na mambo yalikuwa yanaenda,kwa nini leo?
 
Walitakiwa wawaeleze wananchi hasara na faida Ili hata tukipandishiwa kodi tuulize inaenda kufanya kitu gani, maana hii nchi kwenye mind za watu kumejengeka misaada sasa usipowaeleza wanajua ni upigaji.

Ndio maana watakwambia mbona miaka mingine haikuwa hivi na mambo yalikuwa yanaenda,kwa nini leo?
Tanzania tunatumia Sera ambazo hazina tija watu wachache wanajifungia na kuandaa Sera 'ineffective policies' with no guiding principles
 
Back
Top Bottom