Stories of Change - 2023 Competition

jayboy

Member
May 26, 2023
19
15
UTANGULIZI.

Uchumi wa kati ni hali ya nchi kupiga hatua ya maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kitamaduni,hivyo nchi huweza kujiimarisha yenyewe katika sekta muhimu za uzalishaji mali Kama viwanda,Kilimo, biashara na uchumi na kuongeza pato la nchi kwa haraka,hivyo kuachana na hali ya utegemezi wa misaada ya chakula ,madawa,matibabu, wataalamu, vifaa,mikopo na vitu vingine.

Nchi zilizoendelea duniani zimepiga hatua kubwa ya mafanikio kupitia mipango mikakati ya maendeleo ya miaka mitano hadi kumi ili kuimarisha vyema uchumi wa ndani, kupitia Sera na mipango madhubuti za uzalishaji katika maeneo ya kilimo,biashara na uchumi na viwanda.

Nchi mbalimbali zilizoendelea duniani Kama vile China, Japan, Marekani na Afrika kusini kwa upande wa Afrika zilifanya jitihada za makusudi katika kuhakikisha kuwa wanajiimarisha vyema kiuchumi ili kusaidia kuunga mkono harakati za kuboresha hali za wananchi wao kutokana na harakati za kuboresha hali za wananchi wao kutokana na umaskini, njaa Kali, magonjwa, miundombinu mibovu,migogoro ya ardhi,vita na machafuko ya kisiasa.

Kwa ufupi nchi zilizoendelea zimepambana katika kutatua vikwazo vya kiuchumi Kama vile solo huria,mlundikano wa kodi na ushuru wa bidhaa bandarini,usisadi,rushwa na matabaka katika hali ya kiuchumi.

Uchumi wa Kati ni hali ya kiuchumi ambayo nchi inakuwa na pato la Kati,kawaida nchi ya uchumi wa Kati watu wake wanauwezo wa kumudu kiasi cha matumizi dola 10,00 hadi dola 12,000 kwa mwaka kwa kila mwananchi,Nchi ya uchumi wa Kati inakuwa na uchumi unaokua na kuendelea kutoka uchumi wa nchini(low -income economy) kwenda uchumi wa juu(high income economy) kwa kupitia uchumi wakati.

Uchumi wa Kati unaweza kuelezea kupitia viashiria Kama vile Kama vile maendeleo ya viwanda,madini,kilimo,biashara, uchumi,ukuaji wa pato la nchi(GDP),kukuza kwa pato la mtu binafsi (percal income), makazi bora kwa watu,afya na upatikanaji wa huduma za kijamii katika vile maji safi na salama, chakula bora elimu,matibabu, na miundombinu ya usafirishaji na uchukuzi Kama vile barabara,reli,usafiri wa anga,huduma za kifedha(benki) na huduma za posta.

Katika mtazamo wa kiuchumi, nchi zilizoendelea, ni zile ambazo zinafursa nyingi za ukuaji wa uchumi na Maendeleo ya kijamii kwa sababu ya kuwa na vyanzo vya uzalishaji na rasilimali, nchi hizo zinaweza kufaidika kutoka kwa wataalamu wa uchumi wa kimataifa na kutoaTanzania wa ukuaji wa uchumi duniani.

Katika upande wa Afrika nchi zenye uchumi wa Kati ni pamoja na Botswana, Gaboni,Afrika kusini,Namibia,Tunisia, Algeria,Libya,Guinea,Misri,Moroko,Angola,Ghana,Kenya,Ivory cost,Nigeria,Kameruni,Kongo,Senegari na Tanzania lakini katika upande wa Afrika Mashariki nchi zinazoongoza kuwa na uchumi wa Kati ni pamoja na Tanzania, Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi na Sudani ya Kusini.

IMG_20230531_195354.jpg

Picha hii inasadifu maudhui ya uchumi wa Kati ,imechukuliwa kutoka mtandaoni.

Malengo ya kufikia uchumi wa Kati nchini Tanzania yalianzishwa mwaka 2015 na Raising wa awamu ya tano,Dkt,John Pombe Magufuli. Malengo haya ni pamoja na kuongeza uchumi wa nchi,kupunguza utegemezi na misaada ya kifedha kutoka nje, kuongeza fursa za ajira na kuimarisha mabadiliko kwa ujumla. Tanzania imekuwa ikiteketeza mipango mbalimbali ikiwemo kukuza uchumi wa viwanda,kuboresha uchumi wa elimu na afya,kufanya uwekezaji katika miundombinu na kuboresha mazingira ya biashara.

IMG_20230531_195909.jpg

IMG_20230531_204341.jpg

Picha inayoonsha uwekezaji unafanywa katika biashara na viwanda nchini kutoka mtandaoni.

Serikali pia imechukua hatua za kuongeza utalii ,kukuza kilimo cha kisasa na kukuza sekta ya nishati ili kusaidia kufikia malengo ya uchumi wa Kati,haya hivyo kume kuwa na changamoto za upungufu wa miundombinu sawa Kama vile barabara na umeme,migogoro ya ardhi ,ukosefu wa wataalamu wa kutosha na rushwa.Serikali imeendelea kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hizo kwa kuboresha miundombinu ,kuimarisha utawala bora, kupunguza urasimu,kusimamia uwajibikaji na kuweka mfumo wa uwazi katika huduma za wananchi,serikali pia inaendelea kuwezesha wanafunzi kupata elimu na mafunzo ya kuwaongezea ujuzi na kujenga uwezo wa kujitegemea.
IMG_20230531_195242.jpg

Picha hii imechukuliwa kutoka mtandaoni ikionesha wanafunzi wakipewa mafunzo ya kujitegemea.

Katika kukuza sekta ya utalii,serikali imechukua hatua ya kusimamia miundombinu ya utalii Kama vile kujenga hoteli I,kuboresha huduma za usafiri katika vituo vya utalii,pia serikali imeendelea kufanya utafiti wa vivutio vipya vya utalii ili kuongeza aina ya huduma zinazitolewa kwa watalii.
IMG_20230531_222728.jpg

Picha kutoka mtandaoni ikionesha hatua ya serikali katika kuboresha viwanja ndani ya hifadhi ya utalii ya Serengeti,

Katika sekta ya afya,serikali imewekeza katika ujenzi na ukarabati wa zahanati,vituo vya afya na hospitali ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za afya,Aidha,serikali imeendelea kuhamasisha wananchi umuhimu wa kujenga afya bora kwa kutoa elimu na mafunzo kuhusu lishe bora na afya ya uzazi wa mpango.

IMG_20230531_235707.jpg

Picha hii imechukuliwa kutoka tovuti ya wizara ya afya na ujenzi ili kuonesha miradi mbalimbali inayotekelezwa katika sekta ya afya mkoani Ruvuma jirani na nchi ya Msumbiji.

Kwa upande wa kilimo ,serikali imechukua hatua za kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kutoa ruzuku na mikopo kwa wakulima, kuboresha miundombinu ya kilimo Kama vile kujenga miundombinu ya umwagiliaji na kuboresha huduma ya ugavi kwa kutoa mafunzo na elimu kwa wakulima hali imesaidia kuongeza uzalishaji wa mazao Kama vile mpunga,mahindi,maharage na mashudu na hivyo kuimarisha usalama wa chakula na kukuza uchumi wa nchi .
IMG_20230531_222934.jpg
IMG_20230531_222911.jpg

Picha hizi zimechukukiwa kutoka tovuti ya wizara ya kilimo ilkionesha miradi mikubwa ya kilimo inayotekelezwa na serikali katika mikoa ya Iringa,Mbeya na Njombe.

Pia serikali imefanya juhudi kubwa za kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji kwa kujenga na kukarabati barabara, reli na bandari.Hali hii imesaidia kukuza biashara na ukuaji wa uchumi kwani bidhaa zinasafirishwa kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
IMG_20230531_223037.jpg

IMG_20230531_223006.jpg

Picha hizi zimechukuliwa kutoka tovuti ya wizara ya ujenzi ili kuonesha miradi mbalimbali ya uchukuz na usafirishaji inayotekelezwa na serikali.

Kwa ujumla ,serikali ya Tanzania imefanya juhudi kubwa za kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya uwekezaji na biashara,mfano sheria na Sera zimefanyiwa marekebisho ili kuvutia wawekezaji na kuboresha mazingira ya biashara. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Tanzania imejitokeza kuendeleza sekta ya utalii. Sekta hii ya utalii imekuwa na manufaa makubwa kwa uchumi wa nchi na kuleta ajira kwa maelfu ya Watanzania, serikali imefanya jitihada za kuendeleza vivutio vya utalii Kama vile hifadhi za Taifa,fukwe nzuri na maeneo ya utamaduni.
IMG_20230531_222842.jpg

Picha hii imechukuliwa kutoka chaneli ya wanyama inayorushwa na kisimbuzi cha star times katika kutangaza utalii ,picha hii imechukuliwa kutoka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Licha ya juhudi hizi,bado kuna changamoto nyingi zinazikabili sekta ya uwekezaji na biashara nchini,miongoni mwa changamoto hizi ni pamoja na rushwa na ufisadi, wawekezaji wengi wanakabiliana na changamoto hizi mara kwa mara hivyo hutozwa michango msingi ili kupata vibali vya uendeshaji wa biashara nchini ,hali hii inaongeza gharama za uendeshaji na kuleta ugumu katika shughuli za uendeshaji wa biashara zao kwa ufanisi.

IMG_20230531_222650.jpg

Picha hii imechukuliwa kutoka chombo cha habari cha milldayo ili kuchagiza maudhui ya rushwa inavyokwamisha uwekezaji nchini.

Mbali na hilo pia iwawekezaji wanakabiliwa na changamoto za miundombinu inayohitaji ukarabati na uboreshaji Kama vile barabara, reli na viwanja vya ndege,hali hii inaongeza gharama za usafiri na kupunguza ufanisi wa biashara, pia kuna ukosefu wa utayari wa serikali katika kufanya mabadiliko ya kisera ambayo yatawezesha uwekezaji wenye manufaa zaidi kwa jamii na uchumi.

Changamoto nyingine ni pamoja na ukosefu wa rasilimali watu wenye ujuzi wa kutosha kutoa huduma bora kwa wawekezaji. Elimu na mafunzo ya ufundi yanajukumu muhimu katika kuwawezesha watu kutimiza mahitaji na uwezo wa wawekezaji.
IMG_20230531_195159.jpg

Picha hii imechukuliwa kutoka mtandaoni kuonesha ukosefu wa wataalamu wa kutosha kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.

Pia kuna tatizo la usalama na utulivu katika baadhi ya maeneo nchini hali ambayo inaweza kuzuia uwekezaji na biashara ,hivyo kuathiri wawekezaji wanaotaka kuendesha shughuli zao kwenye maeneo hayo na kuongeza habari ya uharibifu wa mali na vurugu.

Picha hii imechukuliwa mtandaoni ili kuonesha kundi la watoto nchini ya umri wa miaka 18(panya road) wanavyojihusisha katika vitendo vya uvunjifu wa amani nchini.

Vile vile, baadhi ya nchi za Afrika zinafanya biashara na nchi nyingine ambazo hazina sheria Kali kuhusu mazingira na haki za wafanyakazi ,hali huwawezesha wawekezaji kudhibiti gharama za uwekezaji lakini inaweza pia kusababisha madhara kwa mazingira na kutowapa wafanyakazi haki zao na mazingira mazuri ya kufanya kazi.Pia wawekezaji wanaweza kukabiliana na changamoto za ukosefu wa miundombinu sahihi Kama barabara salama na ufikiajibwa teknolojia, hali hii inaweza kuwaathiri wawekezaji wa ndani na wamataifa, kuzuia fursa za kibiashara na maendeleo ya kiuchumi. Changamoto nyingine inayowakabili wawekezaji ni kushuka kwa thamani ya saradu na matatizo ya kifedha.

Hali inaweza kupungua kwa biashara na kuongezeka kwa viwango vya riba,vilevile wawekezaji wanaweza kukabiliana na Changamoto za kisiasa na kiusalama Kama migogoro ya kikabila ,ugaidi ,rushwa na utawala wa sheria duni.Migogoro ya kisiasa inaweza kusababisha kufungiwa kwa biashara,kupanda kwa gharama za usafirishaji na kulipa fidia kwa wafanyakazi ambao hawawezi kufikia kazini.

Kuwekeza pi kuna kabiliwa na hatari za kibiashara Kama vile mabadiliko katika mahitaji ya wateja na ushindani kutoka kwa washindani wengine, hali inaweza kusababisha kupungua kwa mauzo na mapato husika,vile vile biashara.Mbali na hayo, wawekezaji wanaweza kukabiliana na hatari za kiuchumi Kama mabadiliko ya kuoanda na kushuka kwa thamani ya sarafu, mfumuko wa bei na hali mbaya ya uchumi wa nchi husika,vilevile wawekezaji wanakabiliana na Changamoto za kiutawala Kama vile kukosa taarifa sahihi za kifedha au ukwepajibwa kodi na sheria za kifedha, ili kukabiliana na hatari na hatari Kama hizi,wawekezaji wanapaswa kuchukua hatua za kuzuia kupunguza hatari zinazowezekana kupitia kufanya utafiti wa kina kabla ya kuwekeza ,kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa uwekezaji, kutathmini kiwango cha hatari ambacho wanaweza kubeba na kudhibiti mapato na matumizi yao kwa makini.

Wawekezaji pia wanahitaji kuwa na uelewa mzuri wa mazingira ya biashara na sheria za uwekezaji za nchi husika na kuzingatia mambo Kama vile usalama wa mazingira, haki za kazi na maadili ya biashara, wawekezaji wanahitaji kuwa tayari kuchukua hatua iwapo wanakabiliwa na hatari ambazo hazikutarajiwa.Hii inajumuisha kuwa tayari kupunguza uwekezaji au kuondoka kabisa ikiwa ni lazima ,kudumisha mawasiliano mazuri na wawekezaji wengine ili kufanya kazi kwa karibu na serikali na mashirika mengine ya kisheria ili kuhakikisha kuwa wanafuata sheria ,kanuni na taratibu zinazofaa.

Mwisho,katika kukabiliana na Changamoto za hali ya uchumi wa Kati nchini Tanzania, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina budi kuboresha uwajibikaji na utawala bora kupitia kuweka mifumo mizuri ya uwajibikaji na uongozi Katika Seka mbalimbali za uzalishaji mali Kama vile kuongeza muda wa kazi kutoka masaa nane hadi kumi katika siku sits kwenye wiki ili kuongeza uzalishaji, kujenga uzalendo wa kununua bidhaa za ndani ili kulinda soko la bidhaa za ndani, pia kuanzisha mfumo wa malipo ya kodi kupitia mfumo wa alama za vidole(fingerprint) ili kuzuia wizi wa kodi, pia serikali inapaswa kuwekeza katika vyanzo visivyokuwa rasmi vya uchumi ili kuongeza pato la nchi, kufufua viwanda vya ushirika ili kupunguza tatito la ajira nchini, kutumia dola katika biashara mbalimbali ili kuongeza thamani ya biashara kwenye solo la duniani,vilevile kununua zabuni za tenda ya mazao ya kilimo kupitia Vyama vya ushirika ili kunguza ulanguzi katika biashara,Katika kutekeleza mapendekezo haya serikali inaweza kutataua changamoto mbalimbali zinazoikumba katika kufikia uchumi wa Kati ifikapo 2025.
 

Attachments

  • IMG_20230531_222934.jpg
    IMG_20230531_222934.jpg
    110 KB · Views: 4
  • IMG_20230531_223037.jpg
    IMG_20230531_223037.jpg
    85 KB · Views: 5
  • IMG_20230531_222842.jpg
    IMG_20230531_222842.jpg
    66.9 KB · Views: 3
  • IMG_20230531_195159.jpg
    IMG_20230531_195159.jpg
    54.4 KB · Views: 4
  • IMG_20230531_223141.jpg
    IMG_20230531_223141.jpg
    59.9 KB · Views: 3

Similar Discussions

Back
Top Bottom