Mwalimu Nyerere hakukianzisha Chama cha CCJ. Isipokuwa hawa watu walioanzisha CCJ wanamtaja Mwalimu katika Katiba yao, wanamweka Mwalimu katika Katiba yao, kama njia ya kupata baraka ya Watanzania.
Hawajajitokeza,kwa nini tusisubiri wajitokeze kabla ya kutoa maoni kuhusu CCJ. Tusibiri. Tunachoweza kusema tu sasa,hatuoni hitilafu yoyote katika jinsi hiki Chama kipya kinavyoanzishwa.
Sisi hatujafaidika sana na uongozi wa Jakaya Kikwete. Tunadhani kwamba viongozi ni lazima wawe watu of high moral calibre.Uongozi wa juu lazima wawe people of high moral calibre. We will not complain kama hatutapata nafasi ya kushiriki katika kuipora Nchi. Lakini at least we hope that there can be peace in our day to day life. Lakini yule kiongozi wa juu,akiwa siyo Mheshimiwa, in the real sense of the word,kwamba ni mtu anayefanya mambo ya heshima, ni mtu ambaye anataka kusikia mambo ya heshima yanafanyika katika himaya yake, basi, kutakuwa hakuna kipingamizi kwa minor official kufanya makosa, kama makosa ya kukiuka haki za binadamu.
Inakuwepo encouragement kwa watu wengi kufanya maovu wakati yule kiongozi wa juu anakuwa mtu of kukewarm morality.
Maadili mema yanapuuzwa, watu wanataka kushi maisha ya kidunia. Watu hawafanyi connection wanayotakiwa kufanya, kati ya ufisadi na hali yao duni ya maisha; tamaa za kutaka utajiri wa haraka, kuwasingizia makosa watu ambao hawana hatia, kwa sababu tu za kutaka kutajirika,au kwa sababu za kidunia, kuwatia hatiani watu ambao hawana hatia, matatizo yanayotokea kwa ajili ya ufuska na ukwere, mambo yote haya yanaonekana kuwa ni tofauti na dhiki zinazotufika katika Nchi. Kuzitakasa nafsi za watu ndio ufunguo wa maendeleo,siyo kitu optional. Haupaswi kuwepo huhur wa mawazo ambapo kila mtu yupo huru kufiria fiithy thoughts.
Kama Chama kipya kitaanzishwa na ahadi ya kuisafisha Nchi kwa nini wasiungwe mkono,kwa nini waitwe CCM B? Kwa hiyo tusubiri wiki chache tuone ni kina nani wanataka kuanzisha Chama kipya, na wana ajenda gani, na vyama vya Upinzani vilivyopo sasa hivi pia vina ajenda gani. Kwa sababu the time is nigh, Uchaguzi Mkuu ni lazima uanze sasa.