Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Can u try talking anything new sometimes?
Just one new thing...a single!..huh!


PJ huyo Kibunango ameshakunywa maji ya bendera ya kijani hata umwambie nini atakufa na skafu ya CCM shingoni.
 
hiki chama kimeshaanza kuonesha kina Walakini, hivi kweli kama kuna wapiganaji wa kweli kwenye hichi chama inakuwaje mpaka sasa wanashindwa kujiweka wazi, kwa nini wanakuwa mguu ndani nje?, nadhani kila mtu amwamini mwenzie,
viongozi wenye nia mbilimbili hawatufai Tanzania,

usiwe na haraka kumwona mwali
 
Hakuna wa kutoka ndani ya CCM wewe ndugu yangu. ila wanatazama na kuangalia upepo unakwenda vipi maana utaona siku zinavyokwenda mbele. hawa jamaa mimi naona kama kweli kama kweli wana nia ya kweli juu ya mambo haya ya upinzania Tanzania
 
Mimi naona ni bora wakaingia ndani ya vyama vipivyopo katika CHADEMA na vyama vingine kama CUF, TLP na vingine kama kweli wana nia ya dhati kwetu. Ila ni danganya toto to
 
Mimi naona ni bora wakaingia ndani ya vyama vipivyopo katika CHADEMA na vyama vingine kama CUF, TLP na vingine kama kweli wana nia ya dhati kwetu. Ila ni danganya toto to
Walishajifunza kwa kilichompata Mrema NCCR-Mageuzi.
 
Walishajifunza kwa kilichompata Mrema NCCR-Mageuzi.

Hivyo vilivyopo mi naona kama vyote ni scandalous!

CHADEMA - SKENDO YA U'KANDA
NCCR MAGEUZI- KIMESHADHIBITIWA FULLY, NA WANATANGAZA SERA ZA CCM SASA
TLP - ANOTHER CCM!
CUF- Full udini!

Kuna haja ya uanzishwaji wa chama kipya kabisa!

Tuangalie Kenya jinsi walivyofanikisha jamani!
Fastafasta walianzisha na kuua na kuunganishaunganisha mavyama hadi wakafikia muafaka, na kuchukua nchi!

Sasa hivi tusiangalie chama, tuangalie watu..huh!
 
Mimi huwa kwanza siangalii sana watu nani kiongozi kama ni kuangaliana kwa sura mbona CCM wanaongoza kwa kuwa na watu wenye sura nzuri kwa nje lakini kwa ndani ni tofauti kabisa.

Nimeisoma katiba ya CCJ yote kitu kilichonifurahisha na kuikubali ni maneno yao ya
Kuilinda hifadhi ya jamii,
Kuzilinda rasilimali zote za Taifa zisiangukie mikononi mwa wageni,
kupinga UFISADI kwa nguvu zao zote na
kuheshimu misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa letu J K Nyerere.

Kwa kweli kama ni katiba kuandikwa vizuri imeandikwa baada ya hapo ndipo nasubiri ni nani atakayebeba bendera ya CCJ kama baba wa Taifa alivyosema kiongozi mzuri atapimwa kwa matendo yake na ukimwangalia unasema kweli huyu ni kiongozi.
 
Hivyo vilivyopo mi naona kama vyote ni scandalous!

CHADEMA - SKENDO YA U'KANDA
NCCR MAGEUZI- KIMESHADHIBITIWA FULLY, NA WANATANGAZA SERA ZA CCM SASA
TLP - ANOTHER CCM!
CUF- Full udini!

Kuna haja ya uanzishwaji wa chama kipya kabisa!

Tuangalie Kenya jinsi walivyofanikisha jamani!
Fastafasta walianzisha na kuua na kuunganishaunganisha mavyama hadi wakafikia muafaka, na kuchukua nchi!

Sasa hivi tusiangalie chama, tuangalie watu..huh!

Kwa maana hiyo nawewe unatumika kuendesha propaganda za ccm?
 
Yawezekana siko sahihi,lakini habari za ujio wa chama kipya cha siasa, Chama Cha Jamii (CCJ), zimenipa hofu hasa kwa namna zilivyopokelewa mithili ya habari njema.

Kwanza,kuna ulinganifu unaofanywa kuhusu kuzaliwa kwa CCJ na utabiri wa Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM.Pamoja na heshima kubwa niliyonayo kwa Baba wa Taifa,lakini mie na wewe tunafahamu kuwa Mwalimu alikuwa binadamu na si malaika, hivyo utabiri wake haumaanishi usahihi wa asilimia 100. Lakini la muhimu zaidi ni mchango wa Mwalimu katika kutufikisha hapa tulipo sasa. Sote tunakumbuka kuwa Nyerere alimpigia debe la nguvu Ben Mkapa kuwa rais wetu. Sihitaji kuingia kwa undani kuhusu namna Mkapa alivyolipeleka mrama taifa letu, huku akijitengenezea utajiri mkubwa kwa mgongo wa kubeba wawekezaji.

Je Mkapa alivaa ngozi ya kondoo kiasi kwamba Nyerere hakujua kuwa huyo ni mbwa mwitu? Lakini si Mkapa pekee. Takriban kundi lote la mafisadi, with exception of kizazi kidogo kilichojitokeza baada ya utawala wa Mwalimu, ni watu waliokuwa karibu sana na Baba wa Taifa. Kingunge, swahiba mkubwa wa Mwalimu, ni mwanasiasa aliyetuaminisha kuwa ni Mjamaa halisi lakini sote sasa twajua kuwa lile lilikuwa changa la macho.Je Mwalimu alikuwa naive kuwaamini watu hawa?Nadhani hilo litakuwa jibu rahisi kwa swali gumu. Kitu kilicho bayana ni ukweli kwamba Mwalimu alikuwa akipenda sana kusikilizwa,na wakati huohuo akichukia sana kupingwa. Wajanja walilifahamu hilo,wakamsapoti kwa kila alilosema, naye akawaamini kama vijana wake. Kumbe wao walikuwa wakisubiri wakati mwafaka wa kutunisha misuli na kutoa makucha yao, huku wakishibisha akaunti zao nje ya nchi. Si kweli kwamba ufisadi ni phenomenon iliyochipuka ghafla bali ni matokeo ya mfumo uliolelewa kwa muda mrefu tangu tupate uhuru.

Kufupisha mjadala, kwa mantiki hiyo,hata kama kuzaliwa kwa CCJ ni kutimia kwa utabiri wa Mwalimu, haimaanishi kwamba tutarajie mapya sana kutoka kwa chama hicho kwa vile historia inatuonyesha kuwa si kila aliloamini Mwalimu lilizaa mema kwa taifa.

Pili,habari kwamba wengi wa waasisi wa CCJ ni vigogo wa CCM inapaswa kutufanya sote tukiangalie chama hicho kipya kwa jicho la mashaka. CCM, kama tunavyofahamu wengi, imegeuka kuwa kama Al-Qaeda. Imetanuka kutoka taasisi ya kisiasa na kuwa kama itikadi, na ndio maana leo hii ukijiuliza chama hicho kinafuata itikadi gani utapata majibu ya ajabu ajabu. Kama ilivyo kwa ujamaa,CCM imekuwa mithili ya mfumo unaoamini kiongozi yuko sawa muda wote, uheshimiwa wa kiongozi, kulindana, na kudumisha ufisadi in the name of umoja wa kitaifa. Je vigogo hawa wa CCM ambao sasa wameamua kuja na chama chao si sehemu ya mfumo huohuo tunaoupigia kelele?

Kinachonipa hofu zaidi ni ukweli kwamba vigogo hao wako mguu mmoja ndani mguu mmoja nje katika mahaba yao na CCM.Wanaogopa hata kujiweka wazi hadharani. Tayari baadhi ya wachambuzi wa siasa zetu (na wako wengi kweli hasa msimu huu wa uchaguzi) wanadai kuwa vuguvugu la CCJ ni shinikizo tu kwa JK kuchukua hatua dhidi ya mafisadi. Kwa lugha nyingine, uhai au ustawi wa CCJ unategemea actions from JK. Yaani hatma nzima ya chama mbadala inatarajia matendo ya mtu ambaye ni katika taifa la aina yetu tu bado yuko madarakani kwa uongozi wake hafifu na uliokosa mwelekeo. What if akiamua "kutuzuga" sie na hao jamaa wa CCJ kwa kuchukua hatua tulizokuwa tukipigia kelele kila siku? Kwa taarifa tu, wanasiasa wanaogombea nafasi za uongozi hupendelea kuja na ajenda za kuwaridhisha wapiga kura kwa mfumo wa ahadi au hata vitendo-vyote vikiwa ni vya muda mfupi, vitakavyomwezesha mwanasiasa husika kukubalika na hatimaye kuingia au kurejea madarakani. Na kwa vile katiba yetu haitoi upenyo mzuri wa kumwajibisha kiongozi huyo pindi akiamua kutotekeleza ahadi alizotoa wakati tunamwomba atuchague,basi ni dhahiri anakuwa na fursa nzuri ya kuendelea na usanii wake akishaingia/rejea madarakani.

Tatu, jambo moja ambalo wengi wetu hatulitilii maanani ni nafasi ya vyombo vya dola katika kuhujumu demokrasia.Na si kosa la makusudi kwa vile shughuli hiyo hufanyika kwa siri kama ambavyo nature ya vyombo hivyo ilivyo.Tayari kuna tetesi kuwa baadhi ya vigogo wanaosemekana kuwa waasisi wa CCJ wameshaanza kuhojiwa na vyombo vya dola. Changanya hilo na habari kwamba JK anadai hayuko tayari kuiona CCM ikimfia mikononi mwake, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na CCJ iliyopandikizwa vibaraka watakaopelekea yaleyale ya NCCR Mageuzi. Si ajabu pia CCJ ikawa kiini macho na usanii wa taasisi flani ku-deflect attention yetu kwenye vita dhidi ya ufisadi na kupata tumaini hewa kuwa "aaah sasa CCM lazima iwe tumbo joto kwa vile ikicheza tu inaondolewa na CCJ". Huu unaweza kuwa mchezo wa kuigiza, trust me!

Nne, hata kama CCJ is a real and genuine thing, si habari njema sana kwa akina sie tunaodhani kuwa kuna vyama pinzani, kama Chadema ambavyo angalau vimetuonyesha dhamira na uwezo wa kuchuana na CCM. I don't think CCM-B (tafsiri yangu ya CCJ) inaweza katika muda huu mfupi uliobaki kufanya yale tunayotarajia kutoka kwa chama cha upinzani. As I mentioned earlier, CCM ni zaidi ya chama, ni mithili ya mfumo uliotapakaa nchi nzima na hadi nje ya nchi. Kuna sehemu kadhaa hasa vijijini ambako ugumu wa kutenganisha CCM na serikali ni zaidi ya ule wa kutenganisha atom kijiweni (wanasayansi wanaelewa hilo). Kwa chama kinachozaliwa miezi michache tu kabla ya uchaguzi kujipanga kisawasawa kuung'oa mfumo ulio katika shepu ya chama (CCM) inaweza kuhitaji zaidi ya mbinu za kisiasa.Na kwa vile Tanzania ni quasi-military/security state, tutake tusitake ni lazima CCJ ikubalike miongoni mwa taasisi hizo vinginevyo itaendelea kuwa kwenye top list ya hujuma dhidi yake kutoka kwa taasisi hizo.Na hilo si rahisi kwa vile wengi kwenye taasisi hizo bado wanaishi kwenye fikra za chama kimoja,na kwamba upinzani au tishio lolote kwa CCM is tantamount to kutishia uhai wa taasisi hizo.

Mwisho, CCJ inakuja kugawa kura za Upinzani. Na hiyo si habari njema kwa wanaotaka kuona CCM inaondoka madarakani. Ni habari mbaya zaidi kwa vile umaarufu wa CCJ (kama itaupata) unaweza kuwa si kwa vile ni chama kinachotarajiwa kuleta mabadiliko ya kweli (forget the katiba thing, ni maneno tu kama yalivyo kwenye katiba ya CCM) bali ugonjwa unaotafuna Tanzania na pengine sehemu kubwa ya Afrika wa siasa za haiba. Kuna waliompigia kura JK kwa madaia kuwa ni handsome pasipo kuhoji uwezo wake.Ni katika mtizamo huohuo, CCJ inaweza kupata umaarufu kutokana na u-"kipya kinyemi" wake sambamba na majina yatakayotengeneza safu za chama hicho. As before, uwezo na commitment za viongozi zitakuwa overshadowed na haiba za viongozi husika na hivyo kurejesha kitu kilekile kinachotusumbua na CCM ya sasa.

As I said before, I might be wrong lakini....
 
CCM kusambaranyikaa!

Baadhi ya wana-CCM wameshikwa na tumbo la kuhara baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa baadhi ya vigogo ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejiengua na kuanzisha chama kipya ambacho kimeazimia kumsimamisha mgombea wa kiti cha Uraisi mwaka huu.

Wakizungumzia hofu yao wana-CCM hao wamedai kuwa kitendo cha wabunge hao kufikia hatua hiyo kinaashiria kuwapo kwa makundi ndani ya chama hicho.

Wana-CCM hao wamefikia hatua hiyo baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, jana kupokea barua ya maombi ya kusajili chama kipya kitakachojulikana kama Chama Cha Jamii (CCJ) kinachodaiwa kinahusiana na kumeguka kwa chama tawala.

Wamesema ni afadhali kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuchunguza taarifa hizo na kuchukua tahadhari mapema.

Kada mmoja wa CCM, na ambaye ni diwani wa mojawapo ya kata za Dar es Salaam, amesema kama habari hizo ni za kweli, basi zinatisha. "Ni bora kamati ya Mwinyi ikafanya uchunguzi na kuweka mambo hadharani kunusuru mpasuko ndani ya chama,"

Wamesema kuwa ili kuepuka kutokea kwa mpasuko zaidi ndani ya chama hicho ni bora kamati hiyo, kwa kushirikiana na NEC, ikafanya vikao vya haraka na kutoa maamuzi magumu kwa manufaa ya chama.

Wamedai hali hiyo inaweza kusababisha kuwapo kwa malumbano katika kura za maoni na kumsimamisha mgombea asiyekubalika ambaye matokeo yake atashindwa.

Awali Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema licha ya kuwapo kwa msuguano ndani ya chama, chama hicho kina mizizi imara katika ngazi zote kwa hiyo hakitaathirika.
 
Hivyo vilivyopo mi naona kama vyote ni scandalous!

CHADEMA - SKENDO YA U'KANDA
NCCR MAGEUZI- KIMESHADHIBITIWA FULLY, NA WANATANGAZA SERA ZA CCM SASA
TLP - ANOTHER CCM!
CUF- Full udini!

Kuna haja ya uanzishwaji wa chama kipya kabisa!

Tuangalie Kenya jinsi walivyofanikisha jamani!
Fastafasta walianzisha na kuua na kuunganishaunganisha mavyama hadi wakafikia muafaka, na kuchukua nchi!

Sasa hivi tusiangalie chama, tuangalie watu..huh!

Chama kipya ni sawa na kuruka mkojo kukanyaga mavi. Wazushi tu hao
 
Mimi nilivyosikia "Julius Miselya" tu nikachoka.
 
Ndugu mlalahoi your analysis ni swaafi. Ingekuwa ni assignment kwa ajili ya dissertation basi ningekupa A+. Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Hiyo CCJ ni kama ulivyosema ni CCM B. Unajua nchini Tanzania wengi wetu tumekuwa sehemu ya kizazi na kwa njia hiyo we are bonded to the system of TANU/CCM. Oxygen tunayoivuta ni ya CCM. Mimi naipenda kuitambua kuwa ni Yanga/Simba syndrome. Kama vile club zetu za mipira zinavyoshahabiana na Yanga au Simba, vivyo hivyo siasa za Tanzania vyama vyote vya upinzani ni part and parcel of CCM. Wanaenda upinzani kwa sababu wana malalamiko au manun'guniko. Hata hoja wanazotoa za kumlaumu JK za kitoto kweli. Just imagine kwenye ile kongamano ya MNF pale Karimjee zile hoja za kitoto. Mzee mstaafu analalamika kuwa hasikilizwi. Hii maana yake wanataka attention. Usipowasikiliza basi jawabu ni kulia na kupiga kelele. Haya tuone mambo yatakavyokwenda huko mbeleni.

Kwani Nyerere aliposema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM alijua anasema nini. Mmesahau kuwa Edwin Mtei alikuwa CCM na akaunda CHADEMA. Na ndiyo maana Nyerere aliipenda CHADEMA.

Kuingoa CCM labda baada ya vijiji vya Tanzania kuwa urbanised. Otherwise peasants wengi ni proCCM kutokana na conservatism yao. Upinzani uko mijini kwa sababu watu wa mjini ni enlightened. So I agree with you CCJ is not a panacea for removing CCM
 
Ndugu mlalahoi your analysis ni swaafi. Ingekuwa ni assignment kwa ajili ya dissertation basi ningekupa A+. Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Hiyo CCJ ni kama ulivyosema ni CCM B. Unajua nchini Tanzania wengi wetu tumekuwa sehemu ya kizazi na kwa njia hiyo we are bonded to the system of TANU/CCM. Oxygen tunayoivuta ni ya CCM. Mimi naipenda kuitambua kuwa ni Yanga/Simba syndrome. Kama vile club zetu za mipira zinavyoshahabiana na Yanga au Simba, vivyo hivyo siasa za Tanzania vyama vyote vya upinzani ni part and parcel of CCM. Wanaenda upinzani kwa sababu wana malalamiko au manun'guniko. Hata hoja wanazotoa za kumlaumu JK za kitoto kweli. Just imagine kwenye ile kongamano ya MNF pale Karimjee zile hoja za kitoto. Mzee mstaafu analalamika kuwa hasikilizwi. Hii maana yake wanataka attention. Usipowasikiliza basi jawabu ni kulia na kupiga kelele. Haya tuone mambo yatakavyokwenda huko mbeleni.

Kwani Nyerere aliposema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM alijua anasema nini. Mmesahau kuwa Edwin Mtei alikuwa CCM na akaunda CHADEMA. Na ndiyo maana Nyerere aliipenda CHADEMA.

Kuingoa CCM labda baada ya vijiji vya Tanzania kuwa urbanised. Otherwise peasants wengi ni proCCM kutokana na conservatism yao. Upinzani uko mijini kwa sababu watu wa mjini ni enlightened. So I agree with you CCJ is not a panacea for removing CCM


siku ya siku ikifika msijifiche, waulizeni jirani zetu, kenya (KANU), Zambia ( UNIP), Uganda(UPC), Malawi ( MCP ) Zimbabwe (ZANU-PF Japo mugabe kakataa kushindwa)
 
Mlalahoi,
Hawa watu wametugawanya na kututawala kwa miaka "hamsini" kwa muundo wa Chama kimoja. Kitu kilichowaunganisha ni Chama na itikadi yake ya CCM. They existed, and they did what they wanted to do for my life time.. Anything which conspired in between among themselves kilizimwa, kwa kizingizio cha AMANI. They had moral values. BUT a big but, these guys had power to steal, to kill and to decide our future as long as they had that constitution on their favour and that they are a majority in the 300 (almost) in that parliamentarians etc.

Any party which comes to netralize this I wouldn't be sckeptical as long as they will reduce the powers of CCM. Frankly speaking I am not a fun of CUF but if CUF can netraulize the CCM powers will be happy as CCM can get serious. They are not serious because they do not have an alternative. We can get serious politicians and people will be accountable for what they do.Any changes which make CCM netraulised should hailed as good news.
 
Mwalimu Nyerere hakukianzisha Chama cha CCJ. Isipokuwa hawa watu walioanzisha CCJ wanamtaja Mwalimu katika Katiba yao, wanamweka Mwalimu katika Katiba yao, kama njia ya kupata baraka ya Watanzania.

Hawajajitokeza,kwa nini tusisubiri wajitokeze kabla ya kutoa maoni kuhusu CCJ. Tusibiri. Tunachoweza kusema tu sasa,hatuoni hitilafu yoyote katika jinsi hiki Chama kipya kinavyoanzishwa.

Sisi hatujafaidika sana na uongozi wa Jakaya Kikwete. Tunadhani kwamba viongozi ni lazima wawe watu of high moral calibre.Uongozi wa juu lazima wawe people of high moral calibre. We will not complain kama hatutapata nafasi ya kushiriki katika kuipora Nchi. Lakini at least we hope that there can be peace in our day to day life. Lakini yule kiongozi wa juu,akiwa siyo Mheshimiwa, in the real sense of the word,kwamba ni mtu anayefanya mambo ya heshima, ni mtu ambaye anataka kusikia mambo ya heshima yanafanyika katika himaya yake, basi, kutakuwa hakuna kipingamizi kwa minor official kufanya makosa, kama makosa ya kukiuka haki za binadamu.

Inakuwepo encouragement kwa watu wengi kufanya maovu wakati yule kiongozi wa juu anakuwa mtu of kukewarm morality.

Maadili mema yanapuuzwa, watu wanataka kushi maisha ya kidunia. Watu hawafanyi connection wanayotakiwa kufanya, kati ya ufisadi na hali yao duni ya maisha; tamaa za kutaka utajiri wa haraka, kuwasingizia makosa watu ambao hawana hatia, kwa sababu tu za kutaka kutajirika,au kwa sababu za kidunia, kuwatia hatiani watu ambao hawana hatia, matatizo yanayotokea kwa ajili ya ufuska na ukwere, mambo yote haya yanaonekana kuwa ni tofauti na dhiki zinazotufika katika Nchi. Kuzitakasa nafsi za watu ndio ufunguo wa maendeleo,siyo kitu optional. Haupaswi kuwepo huhur wa mawazo ambapo kila mtu yupo huru kufiria fiithy thoughts.

Kama Chama kipya kitaanzishwa na ahadi ya kuisafisha Nchi kwa nini wasiungwe mkono,kwa nini waitwe CCM B? Kwa hiyo tusubiri wiki chache tuone ni kina nani wanataka kuanzisha Chama kipya, na wana ajenda gani, na vyama vya Upinzani vilivyopo sasa hivi pia vina ajenda gani. Kwa sababu the time is nigh, Uchaguzi Mkuu ni lazima uanze sasa.
 
ogopa sana maishani kuishi kwa kudhania....kuamini au kutoamini ni juu yako heri kuwa katikati ya A na B kuliko kuwa mtu wa kudhani
 
Yawezekana siko sahihi,lakini habari za ujio wa chama kipya cha siasa,Chama Cha Jamii (CCJ),zimenipa hofu hasa kwa namna zilivyopokelewa mithili ya habari njema.

Kwanza,kuna ulinganifu unaofanywa kuhusu kuzaliwa kwa CCJ na utabiri wa Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM.Pamoja na heshima kubwa niliyonayo kwa Baba wa Taifa,lakini mie na wewe tunafahamu kuwa Mwalimu alikuwa binadamu na si malaika,hivyo utabiri wake haumaanishi usahihi wa asilimia 100.Lakini la muhimu zaidi ni mchango wa Mwalimu katika kutufikisha hapa tulipo sasa.Sote tunakumbuka kuwa Nyerere alimpigia debe la nguvu Ben Mkapa kuwa rais wetu.Sihitaji kuingia kwa undani kuhusu namna Mkapa alivyolipeleka mrama taifa letu,huku akijitengenezea utajiri mkubwa kwa mgongo wa kubeba wawekezaji.

Je Mkapa alivaa ngozi ya kondoo kiasi kwamba Nyerere hakujua kuwa huyo ni mbwa mwitu?Kufupisha mjadala,kwa mantiki hiyo,hata kama kuzaliwa kwa CCJ ni kutimia kwa utabiri wa Mwalimu,haimaanishi kwamba tutarajie mapya sana kutoka kwa chama hicho kwa vile historia inatuonyesha kuwa si kila aliloamini Mwalimu lilizaa mema kwa taifa.

Kinachonipa hofu zaidi ni ukweli kwamba vigogo hao wako mguu mmoja ndani mguu mmoja nje katika mahaba yao na CCM.Wanaogopa hata kujiweka wazi hadharani.

Tatu,jambo moja ambalo wengi wetu hatulitilii maanani ni nafasi ya vyombo vya dola katika kuhujumu demokrasia.Na si kosa la makusudi kwa vile shughuli hiyo hufanyika kwa siri kama ambavyo nature ya vyombo hivyo ilivyo.Tayari kuna tetesi kuwa baadhi ya vigogo wanaosemekana kuwa waasisi wa CCJ wameshaanza kuhojiwa na vyombo vya dola.Changanya hilo na habari kwamba JK anadai hayuko tayari kuiona CCM ikimfia mikononi mwake,basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na CCJ iliyopandikizwa vibaraka watakaopelekea yaleyale ya NCCR Mageuzi.Si ajabu pia CCJ ikawa kiini macho na usanii wa taasisi flani ku-deflect attention yetu kwenye vita dhidi ya ufisadi na kupata tumaini hewa kuwa "aaah sasa CCM lazima iwe tumbo joto kwa vile ikicheza tu inaondolewa na CCJ".Huu unaweza kuwa mchazo wa kuigiza,trust me!

Nne,hata kama CCJ is a real and genuine thing,si habari njema sana kwa akina sie tunaodhani kuwa kuna vyama pinzani,kama Chadema ambavyo angalau vimetuonyesha dhamira na uwezo wa kuchuana na CCM.

Mwisho,CCJ inakuja kugawa kura za Upinzani.Na hiyo si habari njema kwa wanaotaka kuona CCM inaondoka madarakani.As I said before,I might be wrong lakini....

red ya kwanza, hata Yesu alijua kuwa yuga angemsaliti, ila mkapa alirubuniwa na utamu wa madaraka, akarubuniwa pia na sumaye.

red ya pili, hili linatia mashaka hasa ukirejea vigogo wa ccm waliopoteza maisha katika mazingira ya utata. lazima hawa wa sasa wawe na mikakati mbadala kama wanavyofanya.

red ya tatu, hilo linawezekana ila kwa vile ni ccm itavunjika, hata ccm itakosa kura nyingi sana na probably zitaenda ccj
 
Kwa Tanzania hata CCM ingawanyike mara kumi, CCM Asili haitatoka madarakani. Kuiangusha CCM si kazi ya siku moja, inahitajika mfumo utakaoweza kuua mizizi ya CCM. na mizizi ya CCM ni hao viongozi wa huko kwenye matawi na mashina. ambao wametandaa nchi nzima.

CCJ na Vigogo wake saa ngapi wataweza kufika huko chini kabisa kwa watanzania wa kawaida kuwashawishi kuwa CCM halisi haiwafai?

Tumewaona CHADEMA wamejitahidi vilivyo kwa Operation Sangara iliyoleta mwamko Mkubwa wa mageuzi lakini je walishinda wapi? hiyo inamaanisha walitakiwa kufanya zaidi ya hiyo operation ya mpito, kwamba ni lazima wawe na viogozi na ofisi tambulika huko huko kwa hao wananchi wa chini kabisa.

Kura zinazowapa CCM Ushindi ni za watu ignorants dont cares na bahati mbaya sana watanzania wengi walalahoi ndio wapo kwenye hilo kundi. Wamesharidhika na hali ya maisha ilivyo na washajichokea. Wengine wanaipa kura CCM tena kwa wingi ni wale watanzania wanaoishi kiujanja ujanja wanatumia madhaifu yaliyopo katika System kujinufaisha binafsi. Hii aina ya watu kuwabadilisha withing miezi 8 si kitu rahisi hivyo.

Ili kuiangusha CCM, lazima kuishinda kwanza huku chini kabisa kwenye ngazi za halmashauri.
 
Back
Top Bottom