Sasa kama John Tendwa ndio muhusika mkuu, hata usipomtambua itasaidia nini?
Ni sawa na kusema natambua nchi ya Tanzania ila simtambui rais wa Tanzania,
maana hata ukisema taasisi ikae basi huyo Tendwa lazima awepo na atatoa naye maamuzi vilevile, so hata kama ni muafaka utafikiwa uleule, huyo ni kama representative wa taasisi nzima..
Hakumtambua rais sasa hamtambui na huyu Jamaa, mwisho wa siku hatomtambua mtu yeyote sasa...
Afu watu wanaongea kwa uhakika sana na 2015, vipi mmeoteshwa ka babu wa Loliondo nini??
Nenda vijijini ujionee, kuna wamama wababa wakaka wadada hata CDM hawajui ni nini, wao ukiwaambia vyama watakwambia chama si ni CCM, hawajui kama vipo vingine, mfano kuna mgombea mmoja uchaguzi uliopita, wameenda kumuhoji mama yake kijijini, kumuliza mwanao ni chama gani, mama akajibu "kwani sio CCM, mi najua CCM" can you imagine???
Bado sana, labda mfikirie 2020, M4C imefika maeneo mengi ndiyo, lakini kiukweli sio mbali ki hivo, na unavoona wanaenda sehemu vijana wanajaa wengi, asilimia kubwa si wapiga kura, tafuta kama hata kadi wanazo, tusichukue statistics kwa macho tu, tuone ukweli uko wapi, kila mwaka CCM wanashinda, unadhani ni wizi? watu hawajui kama jamaa wengine wana exist kabisa, ye akienda ni CCM tu, anajua ndio kilikuwepo toka enzi zileeeee, Nyerere alisikika hadi kijijini bna, kuna sehemu hawamjui yeyote toka CDM wala chama kingine hadi leo, unataka mfano uliza nikupe ipo mingi tu